Kuamini CCM itaboresha hali ya kisiasa 2029/2030 tofauti na ya 2024/2025 ni kujipa matumaini hewa

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Sehemu yoyote ile duniani haijawahi kutokea walioshika madaraka ya kisiasa wakakubali kuyaachia au kudhibitiwa(checked) tu bila uwepo wa mifumo huru, upinzani wa nguvu, shinikizo kali kuwaonyesha kwamba wao kuendelea kung'ang'ania hayo madaraka itakuwa ni gharama zaidi kuliko faida.

Tukirijelea katika tume ya Chande aliyowasilisha leo ni wazi kwamba taarifa ya tume ni dhaifu sana. Imeshindwa kubainisha na kujikita katika mzizi mkuu wa chanzo cha matatizo ya October 29 na imeshindwa kubainisha waliowajibika. Nimeshangaa sana utekaji unaohusishwa na siasa ukipuuziliwa mbali na tume hiyo pamoja na kelele kubwa zilizopigwa kuhusu utekaji na upotezwaji watu wa kisiasa.

Hii tume ilikutana na ambao ndugu zao wametekwa na kupotezwa? Imekutana na TEC? Kwa nini sauti zao za haki hazisikiki kwenye ripoti ya tume?

Mwenye ripoti yake naye anasema mapendekezo ya tume ya maridhiano ndio yataenda kwenye katiba mpya, tunarudi kulekule kuibadilisha jina NEC kuwa INEC tu, ni mvinyo ule ule ila chupa tofauti, sheikh yule yule ila kanzu tofauti.

Maridhiano ya serikali ya CCM na CCM pamoja na vyama shikizi/rafiki vya CCM na BAKWATA hayataleta muafaka wowote tofauti wa kisiasa.
 
Kazi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom