Kuamini Google na ufinyu wa maarifa: Teknolojia ina faida chache ila hasara kibao

Ha haaa acha bwana kunichekesha.
Ndo hivyo halina hisia hata ulitukane
Leo asubuhi nikaliambia nimekata tamaa na maisha nataka kujiua likanibembeleza mara ooh sijui tafuta msaada wa haraka kwa rafiki anayetegemeka, mtu wa familia au mtaalamu wa saikolojia πŸ˜€
 
Bwana weee unanivunja mbavu🀣🀣🀣.
Haya ukuje rafiki yangu nikushauri.
Ngoja nikuje niufanyie kazi ushauri wake πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ nisije nikajitia kitanzi bure tena nimechelewa maana alinishauri tangu asubuhi
 
Bado upo kizamani, google imepitwa na wakati, sasa hivi watu tupo kwenye Open AI chat gpt.

Mbona umechelewa sana kijana? Nenda na wakati.
 
Mkuu unajua google ni nini na inafanyaje kazi? Ebu jaribu kufikiria kidogo... Anaeenda kutafuta jibu kwenye search engine kubwa kama google ni anatafuta jibu lenye majibu ya kiwango cha kimataifa... Nikianza kukueleza jinsi google inafanya kazi, itabid nikueleze na chatGPT, alafu hapo hapo nikueleze github alafu nikwambie mambo ya databases alafu tuje server na mambo mengi ambayo we ni mweupe, na wewe sio mtu wa technology so ntakutesa tu, tafuta namna google inafanya kazi alafu ulete jibu... Mfano swali rahis unadhani kwanini ukiandika Tanzania inakwambia hii nchi iko wapi na haikosei? Alafu kitu kingine unadhani google inatumika kote sio? China, north na south korea na Russia hawatumii google kama search engine yao... Unadhan vile unavyovisearch vinajijia tu mzee watu wamechapa code za javaScript na typescript pamoja na html na css zikaelewa sababu wewe mtumiaji wa mwisho ukaona ni uongo au sio? Google has 2.5B visitors per month mzee hawa wote hawana akili ila wewe kamanda... Umetisha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…