Kuamka asubuhi ni changamoto

Kuamka asubuhi ni changamoto

Nauliza tu kwa nyie wanajamii wenzangu, hivi hii inasababishwa na nini asubuhi kuamka kwenda kazini yaani uvivu wa ajabu yaani natamani kurudi kitandani nilale.

Kuna muda nilidhani labda nachelewa kulala maana huwa nalala saa sita usiku basi hata nikilala saa nne usiku bado nahisi sijalala vya kutosha.

NOTE: Siku hizi nakaa uswahilini, je inawezekana kwamba kuna ndumba zinafanyika?
Kula chakula chepesi na kunywa maji ya kutosha mapema, saa mbili mwisho kula. Maisha ni mipango sahihi sio kukurupuka tu. Ndumba ufanyiwe ya nn sasa mkuu
 
Unakula unashiba vizur hilo ndo tatizo...hauna njaa ya hela
 
Mimi sipatagi usingizi kabisa yaan wewe una raha sana ndio maana huna majukumu yoyote hio ndio sababu ungekua una majukumu usingekua unapata usingizi kabisa yaan hata kulala kwako ingekua tabu

Jipe majukumu ya kutosha tafuta pesa, matajiri wote unaowajua kuanzia MO na wengineo hua wanaamka saa 10 au 11 asubuhi mapema kabisa, sasa wewe mwenzangu na mimi unanogewa na usingizi kiasi hicho una raha gan kwa mfano?

Pole sana

Napita..
 
Endelea kulala mkuu ukiamka utakula ulichoota
 
Sisi wengine hata ucngizi hatuna kisa hatuna kazi

We sema ALHAMDULILLAH
 
Back
Top Bottom