Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Raimondo aliwahi kuwa “nyundo” ya kukandamiza China. Wakati alipokuwa Waziri wa Biashara wa Marekani, zaidi ya makampuni 200 ya China yaliwekwa kwenye “orodha nyeusi” ya wizara yake. Radio ya Kitaifa ya Marekani NBC ilitangaza mahojiano yaliyofanywa kwa njia ya video na Raimondo.
Wakati huo, alisema, “Fikiria ikiwa kuna mamilioni ya magari ya China yanayoendeshwa kwenye barabara za Marekani, Wachina wataweza kukusanya data za Wamarekani kila dakika, na Beijing itaweza kuyazima magari hayo yote kwa wakati mmoja.” Matamshi yake hayo yalimfanya hata mwanahabari wa NBC awe na shaka, lakini alisisitiza kuwa ni matamshi kwa ajili ya “usalama wa taifa” wa Marekani.
Hata hivyo, baada ya kuondoka madarakani, Raimondo anaonekana kubadili mtazamo wake. Tarehe 11 mwezi huu, katika Kongamano la Teknolojia na Ubunifu la KPMG, Raimondo alipotoa maoni yake kuhusu ushindani wa China na Marekani katika akili bandia (AI), alisema, anaelewa kwamba China ni mshindani wa kimkakati wa Marekani, lakini Marekani inapaswa kudumisha mawasiliano na China, ama sivyo inaweza kusababisha maamuzi yasiyo sahihi, na kuongeza kuwa, ushirikiano kati ya China na Marekani katika sekta ya AI ni kwa maslahi ya pamoja ya nchi zote mbili.
Pia alimlaumu rais Donald Trump wa Marekani, akisema, wakati China inajenga barabara kuu nchini Kenya, Marekani yenyewe inafanya nini? Marekani inapoteza imani kwa kutoza ushuru wa machafuko. Zaidi ya hayo, Raimondo alipinga wazi sera za Marekani za kukandamiza China akisema, kujaribu kuizuia China ni hatua isiyo na mantiki, na ni sawa na mashindano ya mbio, kwani unaweza kuvuta shati la mpinzani wako, lakini kitendo hicho hakiweza kuleta ushindi. Ili kudumisha ushindi, inapaswa kukimbia kwa kasi zaidi, na huo ndio ufunguo wa mafanikio.
“Kuamka” kwa Raimondo kumeonesha Marekani imekuwa na ugonjwa sugu wa kisiasa dhidi ya China. Misimamo mikali dhidi ya China imekuwa kichocheo cha bei rahisi cha kisiasa, na kushangiliwa mara moja kwa kupigiwa makofi na pande mbalimbali.
Kama matokeo, fikra za kimantiki zimefutiliwa mbali, uamuzi wa kimantiki umezuiwa, na maafisa wanatembea kwa tahadhari, wakihofia kuwa wanaweza kulaumiwa kuwa “laini kwa China” na kuwa na hatari ya kupoteza nyadhifa zao. Lakini ugonjwa huo wa kisiasa sio kama tu unatia sumu kwa mahusiano ya China na Marekani, bali pia unadhoofisha msingi wa maslahi ya muda mrefu ya Marekani.