Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Kuanguka chooni/bafuni na kufa, kuna uhusiano gani?

Jamani wana jf,

Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako.

Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia.

sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.
Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.

Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.

Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.

Rest in Peace Shangazi.
 
Dah! Hyo ki2 ni ni swali ndan ya vichwa vya watu wengi,tena inakuwa kama ukidondoka hujafa basi utapoteza fahamu na hata kuumwa kwa muda...kuna mdada ilimtokeaga huku mtaani co watu wenye kuelewa ama wenye ujuzi mdogo 2fumbueni macho..
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Jamani wana jf.Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako..Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia..sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.Rest in Peace.Shangazi.

huyu ilikuwa ni siku yake ya kufa tu wala usiogope mkuu unaweza ukaangukia medula ukafa sababu ni sehemu sensitive mwilini kwa hiyo mkuu ondoa kabisa hizo fikra..
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Jamani wana jf.Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako..Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia..sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.Rest in Peace.Shangazi.

mkuu ni kweli 100% ya wanao anguka chooni hufa kwasababu kuanguka chooni huwa kunahusishwa sana na mambo ya kiswahili au kishirikina.
hii kitu ipo sana tu kwa hali ya kawaida kuanguka chooni ni ngum sana na kama ikitokea umeanguka mara nyingi ushilikina huhusishwa.
mm nilisha wahi msikia bibi 1 akisimulia kuwa dawa 1 wapo huduma ya kwanza ya kumpa mtu ambaye kadondoka chooni kabla hauja mtoa chooni mburuze au mnyanyue mpaka katikati ya mlango unamuweka katikati chini ya mlango na unamlisha kitu kisafi ambacho hakiendani na mazingira ya chooni .mfano wengi sana hutumia NDIZI unaimenya na kumlazimisha mpaka ale hata kama akiwa amefunga mdomo na mara nyingi watu waangukao chooni midomo yao hukaza huwa hawawezi kuachama kilahisi lahisi so jitahidi umlazimishe mpaka ale ndizi hiyo na kama alikuwa kaanza kukata kauli utaona anaanza kuongea na kuchezesha macho ikiwezekana kuongea kabisa.
then ndio mpeleke kwamatibabu zaidi.

mwenye swali ruksa kuuliza
 
huyu ilikuwa ni siku yake ya kufa tu wala usiogope mkuu unaweza ukaangukia medula ukafa sababu ni sehemu sensitive mwilini kwa hiyo mkuu ondoa kabisa hizo fikra..

kila kitu kitokeacho mkuu kinamaana yake na sababu yake mkuu.
vijana wa kleo kuna mambo mengi sana tunayapuuza na kuyazarau na huwa hatufuatilii kumbe ni ya msingi sana.
tunaangamia mkuu kwa kukosa maarifa.

ila sishangai koz wazee wanaishia chalinze
 
Hii issue iliondoa uhai mjomba wangu pia, alianguka uani na kupinda mdomo na mkono wa kulia kushindwa fanya kazi. Kwa miezi mitatu aliteseka sana baadae ndipo shida ikagundulika muhimbili kuwa kuna mshipa ulipasuka kichwani. Bahati mbaya ikawa too late!!!
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Kwa waislam tunaamini kuwa huko chooni kuna wadudu wabaya saana (mashetan) na maumbo yao yapo tafauti ..mfano mtu akianguka chooni..utamuona mdomo wake ..umekuwa upande
.au mokono haifanyi kazi..alimradi hatokuwa sawaa tu..sasa hao wadudu wanakuwa sura zao kama hizo nolizozitaja..mdomo upande n.k. NDio maana mashekhe zetu kila siku anatwambia tusome dua malaum unapoingia chooni na unapotoka salaama ..ili dua hiyo ikukinge na ballaa hilo..
 
huyu ilikuwa ni siku yake ya kufa tu wala usiogope mkuu unaweza ukaangukia medula ukafa sababu ni sehemu sensitive mwilini kwa hiyo mkuu ondoa kabisa hizo fikra..
Hapana bado hujanishawishi kabisa kuondoa fikra zangu hapo.kwa sababu huyu aliefariki sii mtu wa kwanza kusikia kaanguka chooni.ni wengi tuu ambao nilishawahi kuambiwa vifo vyao vilitokana na kunguka chooni.Yaani baada ya wiki/miezi au mwaka hadi miaka baada ya kuugua sana,unaambiwa marehem aliugua sana na mwisho akafariki lkn ugonjwa na umauti ulimpata baada ya kuanguka chooni/bafuni.
 
TAHADHARI;Tusihusishe/kufananisha haya mambo na yule msanii wetu tuliempenda,kwasababu hakuanguka chooni bali ni sebuleni kwa mujibu wa maelezo na pia sababu au chanzo cha kifo chake tulielezwa,japo sii wote waliopata taarifa za kuaminika.ingawaje baadhi ya wa tz wenzetu walipotoshwa kwa namna moja ama nyingine waamini ni MafundiHuru walihusika, ingawa chanzo cha kifo chake kilitajwa.
 
Pia tunatakiwa..tukisha maliza haja ufanye utoke ..pia mambo ya kuimba chooni ni mabayakabisa..kuna viumbe humo ndo makaazi yao..so unapomaliza toka..
Basi chooni sii mahala salama kama Kanisani,Msikitini,Bar's,Restaurant's,Casino's,Hotel's,Guest House's
nakadhalika Eeeeeh!..O.M.G
Mnazidi kunitisha.
Endeleeni kufunguka plz...!!
 
Nimewahi kusikia kuna mmoja alianguka lakini hakufa alfajiri ilkuwa na wakati wanampeleka hospitali alikuwa akilalamika kukutana na mtu mkubwa sana ambaye alimbana na kumuumiza sana alikuwa akiirudia hiyo kauli mara nyingi alikata kauli njiani na alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini

source; mama wa rafiki yangu ambaye ni ndugu wa marehemu
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Hahahahaha watu mna mambo nyie. Mbona bibi yangu alianguka chooni wakati anaumwa ila alipona tu?
 
  • Thanks
Reactions: 1gb
Aione MziziMkavu kwa ufafanuzi zaidi.....
Bibie charminglady Kuanguka kwa

chooni ni dalili ya ishara mbaya ya kupatwa na ugonjwa wa kiharusi kupooza kwa upande mmoja. Na Kama utaanguka

chooni kwa bahati mbaya na unaweza usipooze upande mmoja itakuwa ni bahati yako nzuri lakini wengi wao

wanaoanguka chooni huwa wanapatwa na maradhi ya kiharusi yaani Stroke na kama utapona basi utakuwa umepooza

upande mmoja kwa wanawake hupooza upande wa kulia kwa wanaume hupooza upande wa kushoto na ikitokea

umepoza upande mmoja basi kupona inakuwa tabu sana. Kwa imani zetu watu wa Miji ya Pwani yaani Bwagamoyo Dar,Tanga,Zanzibar,Pemba, Mtwara na Mombasa chooni kuna Shetani mbaya

unachotakiwa kwenda chooni utangulize mguu wa kushoto na usome dua fulani kwa kiswahili unaweza kusema hivi

(Ewe Mwenyeezi Mungu ninajikinga kwako kutokana na uchafu wa shetani).Ndio unaingia kwa kutumia mguu wako kushoto na wakati wa

kutoka unatoka na mguu wa kulia ndio unaotanguliza kwa kumuomba Mungu pia, kwa kumshukuru unasema hivi

(Ninakushukuru kwako Mwenyeezi Mungu) ndio unatanguliza mguu wa kulia wakati wa kutoka hayo ndio ninavyojuwa mimi sijuwi

wenzangu wengine mnajuaje tuelewesheni jamani.

Ni yapi makazi ya Majini?

Majini wanaishi katika mgongo wa ardhi, na wanapatikana kwa wingi katika majangwa na sehemu za takataka, sehemu zenye najisi, chooni na makaburini. Na hii ndio sababu hasa ya wale waganga ambao wana uhusiano na mashetani kupenda kuwashauri wateja wao kupeleka vitu vyao na uchawi wao katika maeneo hayo.


images


Shetani huyu ndio hupenda kukaa chooni au sehemu chafu chafu na pia hukaa majalalani.Na hupenda kunyonya Damu za watu.
 
Back
Top Bottom