The hammer
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,397
- 1,786
Jamani wana jf.Naamini humu ndani tupo tofauti tofauti na kila mmoja kajaliwa karama pekee na mola wetu.Kwa hivyo basi ujuaji wako ndo karama yako ya ufahamu wako..Sasa back to the topic ni kwamba ni kwamba rafki yangu kafiwa na shangazi yake,chanzo alianguka chooni wakati alipo enda kujisaidia..sasa baada ya kuanguka huyu marehem mama mdomo wake ulikaa upande akapelekwa Hospitali ya Temeke,akalazwa kwa matibabu.Baada ya wk mbili na nusu huyo Mama (marehemu sasa)akafariki.Sasa kinachonifanya niiwasilishe hii thread.,ni kuwa taarifa kama hizi kwangu mimi zishanishawishi niamini mtu akianguka chooni huku town basii huyo ni kifo tuu.Hebu basi wenye ufaham,ushuhuda kama huu na uelewa wa mambo kama haya au yanayohusiana na kuanguka chooni/bafuni baada ya hapo unaugua au kufa,basi tutiririke kuringana na ujuzi,uelewa na ufahamu tulio jaaliwa.Rest in Peace.Shangazi.
Hiyo ni presha kali wala hakuna kingine...moja ya dalili ya presha kali ni kupinda mdomo....fuatilia au oogle utaona...hakuna cha ushirikina wala mauza uza...presha ya namna hiyo inaweza kukutokea sehemu yoyote tu


