Wafuasi wa Chadema wameanza kuikodolea macho ACT wazalendo baada ya kuona hatma ya Chama chao imeanza kuota mizizi na haina tofauti sana na ile iliyopelekea CUF kuvurugwa na kuchawanyika pande mbili.
Ni wazi sasa Chama kikuu kinaelekea kuwa zamu ya ACT Wazalendo maana tayari Chadema inakatwa kichwa ,kwani ilikuwa ni Joka la mdimu linalotishia uhai wa Mfalme CCM.
ACT jipangeni kupokea viongozi waandamizi wa CHADEMA ,naiona Tanzania itakayokuwa na vyama viwili hadi vitatu vya siasa.
Kile Chama kimoja juzi kiongozi wake mkuu ameonyesha kuwa na mori wa hasira(NCCR) ,hivi hawa wamekasirika au wamekasirishwa ?