Thuwaiba Habibu
Member
- Oct 8, 2024
- 8
- 5
Msanii maarufu wa kimataifa Stevie Wonder mwimbaji na mwandishi wa nyimbo kutoka Nchini Marekani mwenye ulemavu wa macho ambaye pia ni mjumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa, ameweza kusikika akisema."Mtu kuwa na matatizo ya kuona haina maana kwamba hawezi kuona matatizo tunayopaswa kuyatatua katika ulimwengu".
Nukuu hii inabeba simulizi ya Jamila Borafya Hamza 26, mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya watoto watatu. na anaishi na mzazi wa kike Kwa bahati nzuri au mbaya mzazi wake kiume wametangulia mbele ya haki.
Jamilia anasimulia kuwa alipata tatizo la mtoto wa jicho akiwa mdogo jambo ambalo limepelekea ulemavu wa Uwoni.Suala hilo halijawahi kuzima ndoto ya Jamilia kuwa kiongozi alianza rasmi harakati za uongozi 2012 akiwa na miaka 13 katika skuli ya msingi Kisiwandui akishikilia nafasi ya Waziri Habari katika Serikali ya Wanafunzi.
"Ilianza kama masihara baada ya kuwambia wanafunzi wenzangu natamani kuwa kiongozi ila siwezi kumbe mwalimu alisikia na kuniambia nakupa fomu wewe ndio utaongoza huo mchakato” Ameendelea Kusimualia.
Safari hio alifungua njia yangu ya kuwa kiongozi kwani aliweza kushikilia nafasi mbali mbali za uongozi hapa Zanzibar.Mwaka 2015 akawa Mwenyekiti wa Klabu ya TUSEME inayowawezesha wanawake kuzungumza na kujiamini, na nafasi hiyo hiyo alipata shukilia 2016 lilipoanzishwa Baraza la Vijana Zanzibar nikawa katika ngazi ya shehia, Kamati Tendaji Wilaya, Jumuiya ya Wasiona Zanzibar (ZANAB) pamoja na Kamati ya michezo Zanzibar 2018.
Nyadhifa hizi ni dhahiri uwezo wake na uthubutu ni safari yenye mengi ya kujifunza “Jamii haiwaamini watu wenye ulemavu na husema hawauziki katika siasa ndio maana hatupewi kipao mbele ukilinganisha na wengine hivyo vyama na tasisi wanaamini wanakosa nafasi kupitia sisi" Amesema Jamila.
Safari yake ya kuanza kuwa kiongozi imeweka mazingira mazuri ya Jamilia kupenda kuongoza na kuwa kwenye masuala mengi ya kijamii.
Takwimu kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali Zanzibar inaonesha kuwa hadi mwaka 2023 Zanzibar inajumla ya watu wenye ulemavu 8,100 ikijumuisha ulemavu wa ngozi,maskio,akili na mengineyo.
Mwaka 2020 Jamila aligombea nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo la Mwanakwerekwe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini hakubahatika huku mwaka 2021 akagombea Baraza la Vijana Zanzibar katika ngazi ya juu kabisa ya Watendaji wa baraza ambao ni saba tu kwa Unguja na Pemba na miongoni mwa hao mimi nilikuwa mtu pekee mwenye ulemavu pia nilikuwa Katibu wa UWT katika jimbo langu ambazo nafsi hizi nahudumu mpaka sasa.”
Najiona kama Baraka na nashkuru kuwa nina uwezo wa kuwa kiongozi licha ya kuwa na ulemavu” Amemaliza Jamila.
Upande mwengine pia kuhusu Jamilia ni Mtunzi na msomaji wa mashairi na kwa sasa amestaafu katika Chama cha Ushairi (CHAKUWAZA) akiwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi.
Yumna Mmanga Omar 32 mwenye ulemavu wa ngozi ni mtoto wa saba kuzaliwa katika famila ya watoto 9 anaishi na wazazi wote wawili.Alianza kuwa kiongozi akiwa shuleni kama kiongozi wa darasa na hiyo ilimuongezea uwezo na ujasiri hadi kidatu cha nne mwaka 2014 ambapo alishikilia nafasi ya Waziri wa Elimu
AmesomaAbdurahman AL-Summait Chuo kilichopo Zanzibar ambapo yeye na mwenzake walianzisha Tasisi ya Geographia ambayo hajawahi kuwepo bali zilikuwepo tasisi nyengine kama kiswahili.
"Ndani ya Taasis nilikuwa nashughulikia masuala ya tafiti na miradi” Amesema Yumna.
Baada ya kumaliza masomo alianzisha Chama cha watu wenye Albino akiwa Mwenyekiti (All About Albinism Zanzibar) ambapo ilikuwa ni kwa mara ya kwanza kuwepo hapa visiwani.
”Ilikuwa ndoto yangu na wazazi wangu wanikataza kuingia katika siasa wakati nasoma walitaka nikimaliza ndio nijihusishe na siasa.” Amesema
Yumna ambaye mwaka 2020 aligombea nafasi ya Ubunge Viti Maalum upande wa watu wenye Ulemavu Mkoa wa Mjini na ndani ya Chama Cha Mapinduzi -CCM akitaka kuwa Mjumbe kamati ya Taaluma
“Jamii inaamini kuwa hatuna uwezo wetu kutokana na hali zetu za kiuchumi hatumudu harama za kampeni na hata matumizi ya lugha za alama kwa sababu wao hawaelewi.” Ameendelea kusema.
"Wajumbe wanatutaka tuwafuate moja moja kufanya kampeni kama ukiwa ni mtu wenye ulemavu wa viungo au wa uwoni inakuwa ni ngumu kutokana na mazingira si rafiki” Yumna amesema.
Sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 inaonesha kuwa jumla ya watu wenye ulemavu Zanzibar ni 167,302 wanaume 72,219 na wanawake 95,083.
Licha ya wingi huo kuwepo lakini bado ushiriki wao katika vyombo vya maamuzi ni mdogo kwa kukoseshwa nafasi kutokana na dhana pofu ya jamii ya kuwaona hawezi kuongoza.
Ussi Khamis Debe ni Katibu Mtendaji wa Baraza La Taifa la Watu wenye Ulemavu Zanzibar, amesema saivi inaonekana idadi ya watu wenye ulemavu kushika nafasi za uongozi japo kwa kiwango kidogo katika mihimili yote mitatu ila haitoshelezi.
”Tunao viongozi wa juu wanawake takribani 6 ambao wameingia katika nafasi hizo kwa kuteuliwa na kupitia vyama vyao vya siasa ila bado haitoshi"
Ameongeza kuwa kusema ni vyema Tume ya Uchaguzi na mabaraza ya vyama vya siasa kuweka mazingira rafiki ya watu hao kupata nafasi hizo.
Umoja wa Mataifa katika kikao chake cha tarehe 20 Disemba 1948 ulipitisha Azimio Na. 27 (a) (III) ambalo linaeleza kwamba binadamu wote wamezaliwa huru wakiwa sawa katika haki na kustahili heshima.
Licha ya Azimio hili Umoja wa Mataifa pia lilipitisha maazimio kadhaa kuhusu haki na usawa wa fursa kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali lakini bado ushirikishi wao haupo ipasavyo katika shughuli za maendeleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA-ZNZ, Dkt Mzuri Issa, amesema licha ya jitihada zinazofanyika zipo changamoto wanazopata wanawake na watu wenye ulemavu kufikia malengo yao.
”Miongoni mwa changamoto hizo ni baadhi ya viongozi wa dini, jamii na vyama vya siasa hawajaweka umuhimu kwa wanawake na watu wenye ulemavu kupewa nafasi za makusudi za uongozi”
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu ulioanzishwa mwaka 2006 na kutumika tarehe 3 Mei 2008 umeeleza kuwa watu wenye ulemavu wanakabiliwa na ubaguzi na kunyimwa haki zao za kibinaadamu kote ulimwenguni.
Salma Saadat ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Walemavu Zanzibar (JUWAUZA) amesema vyama vya siasa vibadili misimamo yao na kuona watu wenye ulemavu wana haki sawa na wanaweza kugombania na kuwakilisha nchi kama watu wengine.
"Inawezekana jamii inamtaka ila chama kisimukubali lakini vyama vikiwataka ni rahisi kupata nafasi kwa sababu watawasaidia katika kampeni na kuwaelemisha wananchi juu ya kumpa nafasi mtu mwenye ulemavu kuwa kiongozi”