Elections 2010 KUANGUSHWA: Jinsi Samwel Sitta alivyotoswa kwenye Uspika

Elections 2010 KUANGUSHWA: Jinsi Samwel Sitta alivyotoswa kwenye Uspika

Wanawaonjesha utamu wa fedha ili wawabie kura zao next time2015 shauri lao lisemwalo lipo o laja
 
Wadau,

Kama sikosei ni mwaka jana mwanzoni au mwaka juzi, Rais JK alikwenda Urambo Mashariki kuzindua Ofisi ya Mbunge. Kulikua na malalamiko kwa nini ile ofisi ya Urambo Mashariki ichukue fedha nyingi na iwe ya kisasa na kubwa zaidi kupita ofisi za majimbo mengine, ila kwenye hotuba yake mwenyewe Sitta siku hiyo na niliisikia na kumuona kwenye TV akisema, alidai ya kwamba wamejenga kwa kiwango hicho kwa kuzingatia ya kwamba yeye ni Spika. Nauliza swali, je hata kama alikua ni spika, ina maana alikua na uhakika gani ataendelea kua spika siku zote? Na je, ofisi ya spika inajengwa kwenye jimbo la mbunge husika au inajengwa kwenye makao makuu ya nchi? Na ingekuaje kama asingekua mbunge? Na je, ndiyo tusema hata ofisi za wabunge walio mawaziri nao zijengwe kwa viwango tofauti kwa vile nao ni mawaziri...

Kwa kweli kwa hilo CCM walichemsha, ni bora wangetumia hizo fedha au hiyo "change" kwa ajili ya kuimarisha hospital ya Urambo Mashariki kuliko hizo fedha walizochezea kwenye ile ofisini. Ona sasa, Sitta siyo spika, je ofisi ya nini tena??
 
Kwa wanaoifahamu CCM, ilikuwa ni vigumu kabisa kwa Sitta kurudi kwenye uspika. Kigezo walichokitumia kumteua mwanamke ni siasa tu, lengo ilikuwa kumwondoa Sitta.
Huyu mama hawezi kuliendesha bunge, kumbukeni alishindwa kabisa kuhimili mikiki ya Marehemu Chacha Wangwe. Kuna Mahali Chacha akamwambia sisimami kwenye kiti kutokana na jazba za mama.

CCM wameamua kumteua huyu mama kwa ajili ya kulinda maslahi ya Waizi wa raslimali za nchi hii.
 
Wabunge wote wa cuf waliomo kwenye bunge la muungano wameagizwa kuwa ni lazima waiunge mkono spika wa ccm, ana makinda, maagizo hayo yametolewa usiku huu mjini dodoma, na tayari wabunge wa cuf wamesharifiwa.

Kwa hiyo wabunge wa chadema peke yao ndo watampigia mabere marando

maagizo haya ya serikali kwa cuf ni mwendelezo wa serikali ya mseto ya hivi karibuni huko zanzibar

Uliyosema yametimia
 
tunahitaji fikra yakinafu na si dharau, sasa waliobisha wanataka waseme ccm wameiba kura kwenye uspika? no data no right to say, fumbuen macho macho achen kutembea mmelala.
 
Leo kabla na baada ya Sitta kuapishwa kulikua na makofi kibao na mmoja wao niliyemuona akipiga meza ni Lowasa, Jamaa alikua anapiga makofi kweli au alikua anamsanifu muheshimiwa sita?? Nipeni maoni yenu wana Jamvi!
 
CCM = CUF

Matokeo ya muafaka hayo. Sasa hivi CUF haina meno TENA kwisha kazii.
 
ninajisikia vibaya sana kama BUNGE letu linatawalika na hawa jamaa wawili, yaani Lowasa na Rostam. Watanzania inabidi kujiamini ila bunge limeonyesha udhaifu kumchagua huyu mama, maana hamna kitu. suala la Lowasa na chenge kupiga makofi ni kuthibitisha kuwa wanaweza kufanya CHOCHOTE katika hii nchi pasipo mtu YOYOTE kuwafanya kitu.
Kwa wale waliosoma kitabi cha kuli (kiswahili O'level 90's) kuna kipengele cha mwisho kabisa alisema "" YANA MWISHO HAYA""
 
Leo kabla na baada ya Sitta kuapishwa kulikua na makofi kibao na mmoja wao niliyemuona akipiga meza ni Lowasa, Jamaa alikua anapiga makofi kweli au alikua anamsanifu muheshimiwa sita?? Nipeni maoni yenu wana Jamvi!

Asingepiga makofi nako ingekuwa story tu, so sijui angefanya nini? Hoja zingine ilimradi tuu!!!!
 
Ni mnafiki sana Lowassa na mafisadi wenzake. zama zao zitapita na hakika wataishia vibaya sana kuliko.
 
Makofi yao yametoka hapo hapo viganjani tu.
Kama kawaida Rostam na Lowassa wamefanikiwa kuweka wamtakaye.
Na kama haitoshi wameshamwekea zengwe mama Jenista Mhagama kwenye unaibu, nako wamepenyeza mtu wao.
Huyo Makinda akileta kauzibe Bungeni mambo yatapelekwa kwa WANANCHI kama alivyofanya Dr Slaa pale Mwembeyanga akiwa na mpiganaji Tundu Lissu.
 
Asingepiga makofi nako ingekuwa story tu, so sijui angefanya nini? Hoja zingine ilimradi tuu!!!!
Bora angejamba! Sisi binaadamu tuna matatizo sana ikiwa jua tunalalamika ikinyesha mvua tunalalama hata hatuna kheri!!!!
 
makofi ya Lowasa ni sawa kabisa kwani wamefanikiwa kumwondoa adui wa haki sasa usawa hamna
 
Back
Top Bottom