Wadau,
Kama sikosei ni mwaka jana mwanzoni au mwaka juzi, Rais JK alikwenda Urambo Mashariki kuzindua Ofisi ya Mbunge. Kulikua na malalamiko kwa nini ile ofisi ya Urambo Mashariki ichukue fedha nyingi na iwe ya kisasa na kubwa zaidi kupita ofisi za majimbo mengine, ila kwenye hotuba yake mwenyewe Sitta siku hiyo na niliisikia na kumuona kwenye TV akisema, alidai ya kwamba wamejenga kwa kiwango hicho kwa kuzingatia ya kwamba yeye ni Spika. Nauliza swali, je hata kama alikua ni spika, ina maana alikua na uhakika gani ataendelea kua spika siku zote? Na je, ofisi ya spika inajengwa kwenye jimbo la mbunge husika au inajengwa kwenye makao makuu ya nchi? Na ingekuaje kama asingekua mbunge? Na je, ndiyo tusema hata ofisi za wabunge walio mawaziri nao zijengwe kwa viwango tofauti kwa vile nao ni mawaziri...
Kwa kweli kwa hilo CCM walichemsha, ni bora wangetumia hizo fedha au hiyo "change" kwa ajili ya kuimarisha hospital ya Urambo Mashariki kuliko hizo fedha walizochezea kwenye ile ofisini. Ona sasa, Sitta siyo spika, je ofisi ya nini tena??