Elections 2010 KUANGUSHWA: Jinsi Samwel Sitta alivyotoswa kwenye Uspika


Mhe nimekuelewa ni busara hiyo.
 

Mhe nimekuelewa ni busara hiyo.
 
Kwa niaba ya Malaria Sugu.
 

niliwahi kusoma profile fulani mwanzoni mwa miaka ya tisini iliyoonyesha kuwa madikteta wengi wa africa, Latin America & Asia walikuwa gaduate au waliwahi kuhudhuria mafunzo Havard University.
 
Dhambi hii ni kama kula nyama ya mtu na ukiisha ila huta acha.Tunataka mapinduzi ndani ya CCM,yatakayo leta uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika kuboresha maisha yao.
 
Shairi umelileta, mwenyewe nimekubali,
Tena ni tamu sana, masikioni sikia,
Ndugu yangu sikusifiii, kwa hapo umepatia
Mafisadimafisadi, wa nini Tanzania?

Ni swali najiuliza, ni nani kawachagua?
Wamewekwa na mapesa, ya kifisadi nakuambia,
Ni wananchi wachache, wamewarudisha bungeni,
Mafisadi mafisadi, wa nini Tanzania?

Mfumo wa kifisadi, watawala Tanzania,
Twahitaji kuuondoa mfumo huu jamani
Naamini mwisho wake, ukaribu kufika.
Mafisadi mafisadi, wa nini Tanzania?

Sote tukiungana, mafisadi watatoka,
Elimu ni kitu bora, hasa kule vijijini,
Wimbo huu ufisadi, kwao bado ni mgeni,
Mafisadi mafisadi, wa nini Tanzania?

Beti haziendi mbali, maana hazina vina,
Ujumbe zimeubeba, nadhani mmesikia,
Kasi yetu iwe moja, mafisadi kuwang'oa,
Mafisadi mafisadi, wa nini Tanzania?
 
Unafanya makosa sana majina yao kuanzia na title ya NDUGU, ndani ya CCM neno hilo halina maana tena. Hao undugu na waTanzania walishaufuta siku nyingi sana.

 
nawaomba wana JF tusisimamie udini au ukabila. swala hapa ni ufisadi unao pelekea unyimwaji na unyang'anywaji wa haki ya mtu au watu, ambao utapelekea mtu au watu kusimamia masilai ya chama na siyo ya nchi.

hapa ndo pakusimamia. Nadhani si busara kusema Udini na Ukabila, kila mwana JF anatambua kuwa tunahitaji viongozi wazuri watakao simamia masilai ya nchi nasiyo chama,

HILI NI OMBI KWENU WANA JF.
 

Kamati hii inatakiwa iwe na ratio fulani ya wajumbe toka zanzibar , na kwa kuwa wenzetu kule ni waislamu ndo maana unaona idadi ya ni kubwa , nafikiri sio jambo la kuliangalia sana
vema tukiondokana na UDINI, ni hatari sana kwa Tanzania kuliko ubaguzi mwingine wowote ule
 
Mbona vibaragashia vingi sana kwenye hii kamati.

Poa wazee inabidi nirudi kubeba box, mchana mwema.

wewe vibaragashia vinakuhusu nini? unataka kuleta ubaguzi???????Rudi kabebe box...
 
CCM WOTE NI MAFISADI HIVYO BASI WANAOGOPA UOVU WAO UTAWAUMBUA:tape:
 

habari wana JF,
nimekuwa msomaji wa maoni kwa muda mrefu lkn leo naomba nifumbue mdomo. Naungana na kauli yako kwa kuongezea; mtazamo wangu kuwa maoni yanayotolewa hapa ni kwa ajili ya kuleta maendeleo ya watanzania wote. Anayejisikia kuongelea dini kwa kumsaidia kuna majengo yenye misalaba na mwezi na nyota akaongelee huko wala hakuna atakayemgusa.
 

jamani basi inatosha haya ya udini yawe :closed_2:
niwaulize wa JF sita hawezi kuama chama na kuamia Chadema??
 
Mkuu , mimi nimeweka wajumbe wa CC ya Chaka Chua Matokeo(kwa kifupiCCM),ambayo Six ni mjumbe

Ebwana eeeeeeeeeeeeeeh nimeipenda hii CHAKA CHUA MATOKEO(CCM), wamechakachua mpaka kura za kamati za kumteua 6 kuwa spika? Kweli kikulacho CCMkipo ndani ya CCM hio hio.
 
jamani basi inatosha haya ya udini yawe :closed_2:
niwaulize wa JF sita hawezi kuama chama na kuamia Chadema??
Kama ambition yake ni kuishia kwenye uwaziri tu , anaweza kuhama maana Chadema ikishinda ni rais kuupata kuliko kuachiwa agombee URAIS, lakini kama ni Urais sidhani akienda chadema anaweza kumpiku shujaa SLAA
Na kwa kuwa vita hii ni ya Urais 2015 , akitaka toka CCM atanzisha chake ili ajaribu karata yake

kuna nyakati ilisemwa semwa kwamba alikuwa mwasisi wa CCJ ( sina uhakika)
 
TanzActive,

kweli hili la CCJ namimi nililisikia lakini hiki chama cha ccj kilikua kweli chama au zilikuwa ni zile hadhi za manyoya!!??
 
😛eep:
 

Attachments

  • SITA NA CHENGE..jpg
    28.1 KB · Views: 80

Kaka kama unakerwa na udini uliopo humu!!! nakuomba usiingie ndani ya hii forum,,,, humu kuna GREAT THINKERS wachache mno kiasi kwamba inabidi uchukulie article wanazopost watu wengine kama unasoma folk stories. ni wengi ambao hawatumii bongo zao kutafakari bali wanatumia imani za mioyo yao(dini) kutafakari na kuamua.
Kila kitu humu ndani,wengi hukitafsiri kwa misingi ya chuki za kidini....
KAULI YANGU KWA WANA JF WOTE WENYE AKILI FUPI KAMA MAISHA YA FUNZA,, MNAOFIKIRI KWA MISINGI YA ITIKADI NA SI UZALENDO:-----
huwezi ukaifanya Tanzania kuwa taifa la kikiristo kamwe na wala huwezi kulifanya kuwa taifa la kiislamu kamwe kwani idadi yetu inalingana au kukaribiana sana. na isitoshe muingiliano wa kijamii baina yetu(kuchanganyika,kuoleana, kushereheka pomoja,kuhuzunika pamoja na hata kuzikana) ni mkubwa kiasi ambacho huwezi kututenganisha.
poleni wote mnaofikiri kwa kutumia makalio badala ya ubongo na poleni sana mnaofuga chuki mioyoni mwenu na kuwatenga watu kutokana na dini zao. nilisema na ninasema''''hata chuki za wazi dhidi ya Kikwete zimeegemea zaidi katika udini kuliko udhaifu wake kama kiongozi''''


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…