Elections 2010 KUANGUSHWA: Jinsi Samwel Sitta alivyotoswa kwenye Uspika

Nashukuru sana ndugu ulichoongea lakini pia Naomba Mwongozo wa MODS
Je haiwezekani kumburn mtu yeyote anayechangia ishu ya dini katika kila mada kuanzia sasa, maana hii imekuwa too much sasa, mpaka tunafika mahali tunaanza kuogopa kufungua JF. kama watu wanataka kujadili dini wapewe sehemu huko ya kufanya hivyo lakini siyo kila topic ikija hapa lazima tuzungumzie dini zetu, tunaanza kupoteza lulu ya JF

Naomba sana mods waangalie hili linataka kutupeleka pabaya. inaniumiza sana kwa kweli tunaacha kujadili issues tunajadili dini! hao mafisadi wote wanatoka dini mchanganyiko so let us attack them na si huu ujinga mwingine (MODS I am so hurt)
 
Ushauri wa bure kwa Kaka mh.Sita

atafute chama kingine makini hiyo sisiemu awachie wenye nao nec.

ccm ni chama cha ajabu sana, sikuzote mtu hupewa nafasi ya kutetea kiti chake, sasa kulikoni huku kwa Sita ama ndo ule mchezo wetu waku..............!!!???
Wana JF nisaidieni
 
Wajumbe 26 waislaamu , 11 wakristo nini vigezo vya kamati hii kuwa na uwiano huo?
 
Wajumbe 26 waislaamu , 11 wakristo nini vigezo vya kamati hii kuwa na uwiano huo?

Gwaje hataki kuelewa bado analiendeleza lilelileeeeeee.....!!! tunalolipigia kelele na sasa anatafuta uhiano.

Kazi kweli kweli!!

wana JF msaidieni Gwaje
anahitaji msaada mkubwa wa mawazo
 
sasa jamani nini itakuwa feature ya Mh.sita, mama ni kama vile chama kimemwambia kaa pembeni, yeye mwenyewe sijui anakiangaliaje chama chake kwa sasa,
 
Wajumbe 26 waislaamu , 11 wakristo nini vigezo vya kamati hii kuwa na uwiano huo?

Sasa kama uko serious na mambo ya usawa usiisheie kwenye dini tu. Endelea kunyambulisha

  • Mchamgamunuo wa kabila( Wazanaki wahaya wachaga wakwere, Waha, etc)
  • Mchangamunuo wa mikoa wanayotoka
  • Mchangamunuo wa Age ( 21-25 26-35, 36-45, 46-55 etc )
  • Mchangamunuo wa Jinsia ( Female, Male ,gay, Lesbian, Bisexual. teh teh teh )
  • Mchangamuno wa Ability na disability ( Viziwi Albino, Vipofu ,walemavu)
Otheriwise usiwe great sinker kuwa great thinker.
 
Ni kamati ya Mafisadi! but poa watakwisha na kuangamia! watanzania tupo nyuma ya SITTA.

Sita sasa amedhiirisha kuwa ni mpenda masilahi ya nchi, maana watu kama hao hawatakiwi ccm wanawataka wale wa kufunika funika ukweli!!!

wale wa kutetea masilahi ya chama na siyo Tanzania
 
@ Ntemi kazwile: asilimia ya wakristo tanzania ni less than 40% na waislam ni more than 60% according to census. Sasa kama ktk hiyo kamati ya ccm wametumia kigezo cha udini itakua wakristo wamependelewa maana ilibidi wapate chini ya 40%. Hata hivyo si dhani kama ccm waliangalia vigezo vya udini ktk hiyo kamati.
 
@ Ntemi kazwile: asilimia ya wakristo tanzania ni less than 40% na waislam ni more than 60% according to census. Sasa kama ktk hiyo kamati ya ccm wametumia kigezo cha udini itakua wakristo wamependelewa maana ilibidi wapate chini ya 40%. Hata hivyo si dhani kama ccm waliangalia vigezo vya udini ktk hiyo kamati.
 
Sitta kutoswa uspika sioni ajabu kwani nilitarajia itakuwa hivyo.

Nasema hivi kwani Sita kupata uspika kulitegemea zaidi kamati kuu (CC) ya CCM kuliko kura za wabunge. Ukiangalia wajumbe wa CC karibu wote ni watuhumiwa wa ufisadi, hivyo kwa Sitta kupita hapo isingekuwa rahisi.
 
Kama ni hivyo si wangemtonya asichukue fomu ili ionekane hakutaka kuendelea? Watakuwa wamemdhalilisha sana maana aligangamala sana kumtafutia Kikwete kura mpaka alidiriki kutaka kufanya mdahalo na Dr Slaa ili kutolea ufafanunuzi wa sera za CHADEMA dhidi ya za CCM.
 
Nionavyo mimi spika sita speed yake na viwango vingebaki palepale hata walipotishia kitumbua chake kwani ingeleta maana zaidi miaka mitano ya mabadilko kuliko miaka mingi uovu ukifichwa, huko watanzania wakibaki gizani pasipo kuufahamu ukweli.Martin Luther Jr na Patrice Lumumba twawasoma leo ingawa wameishi duniani kwa muda mfupi.Hata hivyo tunadhamini ulipotufikisha tuombe Mungu atake chukua kijiti aongeze standard na speed.MSIMAMO UNAMAANA MAISHANI HASA PALE UNALOLISIMAMIA LIKIWA NA UKWELI
 
Ni kweli jamaa alijitoa sana kumtetea JK but hayo ndo malipo toka ccm! KWELI MAFISADI NI JITU AMBALO KULITOA IPO KAZI!
CCM IMEINGILIWA NA UFISADI NA KUUTOA NI KUING'OA YOOTE HAKUNA MSAFI PALE! WASAFI HAWATAKIWI KWENYE CHAMA KABISAA!
 
mh. sita huenda akapewa uwaziri mkuu mnaonaje hii wa JF si anafaa au.......??
 
@ ntemi kazwile: Asilimia ya wakristo tanzania ni less than 40% na waislam ni more than 60% according to census
katika sensa ya taifa 2002 , hakuna swali la dini lililoulizwa wewe unazungumzia sensa gani ?

Wewe mdini sana wewe enhee
 

Kumbe kwenye kikao hicho alikuwepo Mh. Sitta!!!! Kwa hiyo na yeye kumbe kajichakachua mwenyewe!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…