Kuanza project ya kuku Machi, 2023

dimple

Senior Member
Joined
Dec 6, 2016
Posts
103
Reaction score
134
EDITED
Nimeanza rasmi may 2 2023

Habari wapendwa mimi engineer by profesional pia ni mjasiliamali hua najishighulisha na kilimo na ufugaji tangu nimalize chuo sikuhitaji ajira kivile ingawa mwanzo tu nilipo graduate niliajiliwa kampuni moja binafsi ila sikukaa sana nikaacha nikaamua kulima. Nimeshalima mazao mbalimbali iñgawa nilipitia changamoto nyingi sana sikukata tamaa ila changamoto kubwa niliyojifunza ni Mtaji.

Kilimo ni PESA kama huna mtaji mkubwa acha kulima borà ununue mazao otherwise utatumia muda mwingi na nguvu nyingi kukusanya mtaji sabab si kila mwaka utapata mavuno yenye faida utajikuta unaanguka kila mara mwishoe ukate tamaa hata kama una pesa ya gunia 10 anza na kununua mazao weka stoo sahau izungushe hiyo pesa kwa muda fulan hadi itapokua nakwambia hivi sabab hakuna anaenunua mazao akaweka stoo anapata hasara hii ni uhakika 100% kupitia mm nkmelima sana hizi ekari 5 -10 tena nilijitosa mwenyewe front sikufichi ni ngumu sana kutoboa unatumia muda mwingi na nguvu nyingi sana kitu ambacho ungeswma ununue mazao ungekua na muda mwingi wa kufanya mambo mengine
Nimedundukiza mtaji nilianza na mpunga wa milion 40 kitu ambacho nimejikuta nanunua mpunga huku nina muda wa kuisimamia mwenyewe project yangu ya kuku wa mayai na kienyeji.

KUKU Wa KIENYEJI:sabab lengo kuu ikikua ni kuja kuwa mfugaji mkubwa niliamua kuanza kujifunza ufugaji wa kuku kwa vitendo ndo nikaanza kujifunzia kuku wa kienyeji
Hawa kuku ninao wachache kama 50 ikiwa chotara ni chotara na kienyeji pure.Hivyo kienyeji ninao haohao 50 ambapo kwa siku napata mayai 17 hadi 28 ya kienyeji na nauza moja 400 tray 12000 +kuku kwa kitoweo majiran wameshapazoea sana na hadi sasa wanajilisha wenyewe nimegundua hii siwezi kuiacha sabab hadi sasa nimeshazoeleka kwa wanaohitaji kuku wa kula na mayai ya kienyeji

KUKU WA MAYAI:
nina eneo la kutosha lina fance na limejitenga kwa maana kuna ukuta katikati kutenganisha uani kwangu na huo uwa wa pili ni kama 11m x 25m. Tulipozungushia ukuta mwanzon nilitaka kukata vyumba vya wapangaji ila baadae tukaamua na mr niweke kuku kwanza

Nilichukua kuku 600 wa mayai ila nimebaki nao 570
Nilianza na cage 2 za vifaranga kwa kuku wa siku 1 hadi siku 30 zilizo ni cost kama laki 9 kwa zote 2 na cage za local 2 za mbao zilicost kama laki 5 kwa kuku wa miez 2 na nusu hadi miezi 3 na nusu
Baada ya hapo nikanunua cage za kuku wakubwa 5 kila moja laki 8 na nusu nikajenga banda la kuingia cage 6 kwa gharama za milion 3 na kidogo hapo ndo mradi ukawa umeanza rasmi nakumbuka kuku walianza kutaga wakiwa na miez 4 na siku 26 almost mitano nimeanza na hivyo naendelea na namshukuru Mungu kwa hapa nilipofikia sabab na wao walishaanza kujilisha kitambo sana hapa nimeweka oda ya vifaranga 1200 kati ya may o june viingie.
Ninaendelea kutanua banda kidogo kidogo hadi kufikia kuku 2000 -3000 kwa hapa home.

Kwa maswali na ushauri kuhusu ufugaji wa kuku karibu niulize chochote

Nimeambatanisha pisha za stage tofautitofauti za kuku wa mayai na kienyeji View attachment 2908997View attachment 2908999View attachment 2909000View attachment 2909002View attachment 2909004View attachment 2909005View attachment 2909006View attachment 2909007View attachment 2909008
 
Fuga nyoka vuna sumu, utanishukuru baadae
Hayo ni maono MWENYEEZI MUNGU amekuonyesha kinachotakikana kwa upande wako ni uthubutu tu, yaani kuanza bila kupoteza muda mengine utajifunzia humo humo ndani ya project yako,ukitaka kuuliza kila kitu kabla utakwama,kikubwa jitahidi ujiunge na group za wafugaji wenzio kwa wasap kwa ushauri na kubadilisha mawazo, na utafute vet mzoefu wa maswala ya ufugaji, then Anza project yako huku ukimtanguliza MUNGU utafika tu,changamoto utakazo kutana nazo zisikutoe kwenye plan yako, changamoto ziwe daraja la kukuvusha ,kwa sababu mafanikio yamefichwa ndani ya changamoto, pambana pambana pambana bila kukata tamaa,Asante ,
 
Ushauri wangu. Tafuta mtu anaitwa malembo farm. Mcheki twitter. Nenda kamuone zungumza nae. Atakufundisha. Kama huna muda peleka staff unayemuamini amtrain. Gharama kubwa iko kwenye chakula cha kuku. Ukipewa mafunzo utaokoa asilimia 75 ya gharama ya chakula.

Utapata faida. Yeye anakupa mafunzo kwa vitendo. Achana na pdf na ushauri wa mtandaoni
 
Nashukuru kwa ushaur wako
 
Asante nitamcheki
 
Nakupongeza sana kwa hatua uliofikia, ufugaji wa kuku wa mayai ndo uliowapa utajiri wazazi wangu na kutusomesha watoto wote, tukiwa nyumbani kazi yetu ilikuwa kuokota mayai na kuosha vyombo vya kuku.

Wazee walikuwa wanauza bei ya kawaida hivyo wateja wengi wa jumla walikuwa wanajazana asa wale wakulya wa kuendesha Baiskeli, pia alikuwa na oda maalumu kwenye hoteli.

Jambo la kuzingatia ambalo niliojifunza kwao:

1. usimamizi wa karibu mno, yaani ni kuacha kazi ili ufanye kazi, akikisha unawapa majani, usitegemee madawa tu ya vitamini, ukitumia majani mayai yanakuwa na rangi nzuri na pia majani uwa ni dawa kwa kuku kwnye magonjwa mengine.

2. Kuku yoyote anayekufa, muite daktari ili amchunguze na kujua chanzo, hii inasaidia kuokoa mifugo iliyobaki na inakupa uzoefu wa kutambua ugonjwa huo ukitokea tena.

3. Zuia muingiliano wa watu kwenye mabanda yako kuokoa magonjwa.

4. Kuwa makini na chakula, maana inachangia sana kwenye ukuaji wa kuku wako.
 
Ushauri mzuri nimeupokea nitahakikisha naufanyia kazi.
Muingiliano hautakuwepo kabisa sabab nimeweka kabisa gate dogo nitahakikisha mtu kuingia ni wakat wa kuweka chakula tu.
 
Sema uandishi mbaya we kilaza mwenye kujifanya unajua wakati hujui kuliko mtoa nada. Hakuna maamuzi ya mwandiko kwa muandishi ktk tablet,computer au simu ya kawaida. Kwa Nini mnajifanya mnajua sana kuliko wenzenu wakati mmekariri tu kama wengine.

[emoji23][emoji23][emoji23] leo ndio mnasema hivyo mnapo kuja kunikosoa kwenye thread zangu mbona nakuwa mpole sana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kama hawa?
 
Zitambue changamoto Ili ujue jinsi ya kuzikabili mfano elewa formula za kutengeneza chakula na additives zake pia fanya tafiti zile farms zinazofanya vizuri wapo vijana pale unaweza kumpoza kidogo akakupa formula za chakula ambazo zipo konki ikakusaidia kuokoa ghalama za chakula Kwa kutengeneza mwenyewe,.pia upande wa disease control na biosecurity hapa mambo Kwa sasa yameadvance sana ukijitahidi hapa utafikia kiwango Cha 0% ya mortality rate ni vyema ujue dawa hii inatumikaje kama preventive na control certain disease Kwa umri upi wa kuku na Kwa muda Gani bahati mbaya vets shop nyingi wengi wanaouza dawa sio maexpert wa fani usika ,mwisho usisahau kutenga eneo la bustani Kwa ajili ya majani ya kuku angalau waweze kupata majani Kwa siku 4-5 Kwa siku.
 
Hongera kwa wazo zuri. Ukilitekeleza kwa ufanisi itakufaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…