DHANA YA “UJAMAA NA MAENDELEO YA VIWANDA” PAMOJA NA DHANA YA IPO SIKU TUTAITUMIA KWA MAENDELEO ENDELEVU
Kama ilivyo wanadamu tuna mahitaji mengi ya msingi na tukiwa tumetimiza miaka 19 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, ni vyema tukatafakari kama taifa lenye watu wapatao 59,000,160 litawezaje kujikimu katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kiutamaduni. Hapo ndipo utangundua ni ukweli usiopingika kuwa muda wa serikali kutekeleza falsafa ya ujamaa ulioboreshwa umefika ili kutengeneza ajira, na nchi kupiga hatua kubwa kuelekea uchumi wa kati 2025.
Ili kufikia dira hiyo, kwa kipindi cha miongo kadhaa watanzania imekuwa ikijikita kwenye uchumi wa kutoa huduma badala ya uzalishaji mathalani uchumi wa nyumba za kupanga, bodaboda, simu n.k. Hali iliyopelekea vijana wengi wasomi wakiwa mitaani bila ajira pamoja na kuwa tegemezi kwa jamii. Kutokana na hali hiyo, kuna haja kwa viongozi kuweka mazingira yatakayofanikisha sera ya ujamaa pamoja na sera ya ubepali kutumika ili kufikia azma ya serikali ya viwanda na kufanya miundombinu ya reli na barabara kutumika ipasavyo. Madhalani, Serikali inaweza tumika taasisi zake ikiwemo NHC kujenga jamii zenye nguvu (Communities) kwa kujenga nyumba (miji) yenye tija katika maeneo ya uzalishaji na kuajiri vijana kama ilivyoanzishwa taasisi ya Kilimo (Mbeya) na Mpwapwa (Dodoma).
Utekelezaji makini wa Sera ya
Mixed Economy nchini kutasaidia kuondoa tatizo la ajira kwa vijana wa kiwango cha
medium zone pamoja na kuongeza uzalishaji utakaosadia kuongeza bidhaa, utulivu wa shilingi, utulivu wa kisiasa na kudumisha amani nchini.
“hivyo ni vyema wanasiasa mkasaidia maandalizi ya kuanzisha vituo vya uwekezaji kulingana na mahitaji ya eneo na wakati husika” kwani ni ukweli usiopigika kuwa tatizo la ajira linaathari siyo katika jamii ya Tanzania pekee pia hata nchi zilizoendelea hivyo ni wakati wa kufunga mkanda (
Benjamini Willium Mkapa) kwa maendeleo endelevu.
TATIZO LA VIJANA WALIOWENGI NI NYUMBA (kulipa kama bia kuelekea kwenye umiliki wake) + TRACTOR
MORE STRATEGIES (attached)