Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

Kuanzia 2015 Tanzania itatawaliwa "kidikteta" Ukweli huu hapa

adolfhitlernazipropagandaeslebedeutschland.jpg

Kwa nini nimeamua kusema hivi? Kuna mambo matano (5) makuu yananilazimisha kusema kuwa:
"Tanzania itatawaliwa kidikteta"
Ni vigumu sana kwa mtu asiyeona mbali kunielewa kirahisi na pia ni rahisi sana kwa anayependa demokrasia kunibeza na kuniona kama naota.

1. Kwanza kuna uwezekano mkubwa Rais ajaye ataingia madarakani kwa utata nikimaanisha kutakuwa na mizengwe katika utoaji wa matokeo kwani hali halisi inajionesha wazi kuwa kuna mvutano mkubwa wa vyama viwili na hakuna kinachokubali kuwa kimeshindwa ki-haki.Endapo mgombea wa chama tawala akashinda basi chama kikuu cha upinzani kitatumia nguvu ya umma ili kupata sapoti wakati aliyejiona kashinda kwa haki atakimbilia ikulu na kushawishi dola kulinda ushindi wake kadri wawezavyo.Tukumbuke yaliyozikumba nchi za :LIBYA, IVORY COAST, LIBERIA, NIGERIA, ZIMBABWE, KENYA, VISIWA VYA COMORO, MISRI na TUNISIA.

2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.

3.Suala zima la maendeleo haliendani na kuwapa watu uhuru wa kukaa mijini na kuendeleza masuala kama ya kupiga debe, kutembeza vitu mijini, kuuza na kula madawa ya kulevya, polisi wa barabarani kupokea rushwa, maafisa wa TRA kusamehe kodi na kutoa vibali kwa njia za panya, viongozi wa serikali kutumia ofisi zao kama kampuni zao! Yote haya yatasababisha rais ajaye awe dikteta na mkatili kwa wazembe wote wanaokwamisha matarajio yake, ikiwa ni pamoja na kuwafurutisha vijana wote mijini na kuwafukuza kazi wazembe wote.

4. Suala zima la ushawishi wa dini, endapo ataegemea dini moja basi atajikuta yupo kwenye wakati mgumu kwani atajikuta amegeuka gafla na kuwa adui wa dini nyingine hivyo kujikuta akichukua maamuzi ya kibabe ili kukabiliana na upinzani kutoka dini fulani. Suala kujiunga na dini ya mashetani au "FREEMASONS" litakuwa jambo la kawaida na watu wengi wenye kupinga serikali watatoweka na wasijulikane wapo wapi.

5.Ushawishi wa nchi za magharibi; hili nalo ni tatizo ambalo nitafanya nchi isitawalike endapo Rais ajae ataamua kufuata matwakwa ya raia wake kwenye masuala la uwekezaji, ajira, ugawaji wa ardhi, kodi, na utaifishaji wa mali za umma kama viwanda, mashamba makubwa, n.k.na endapo atawageuka wananchi na kusikiliza matakwa ya nchi za magharibi basi atajikuta amepitisha sera ya ndoa za jinsia moja, biashara haramu ya siaha, urutubishaji wa nyuklia. Hali hii itapelekea wanachi waanze kumchukia na atajikuta anatumia nguvu za dola kulazimisha wananchi wakubali sera zake.

Pia kuna mambo mengine kama kuibuka vyama vya siasa vyenye nguvu vinavyotaka kumtoa madarakani kwa nguvu na atajikuta akiwasweka rumande wapinzani wengi ambapo itachafua hali ya hewa ya nchi. Pia utata wa mgawanyiko wa wabunge maana kuna kila dalili vyama viwili vyenye ushindani kugawana sehemu kubwa ya idadi ya wabunge na hivyo kumlazimisha Rais kuwa na wakati mgumu wa kuvunja bunge zaidi ya mara moja kwenye kipindi cha miaka mitano.

Pia suala la ajira litaendelea kutesa nchi na ongezeko la wasomi itakuwa pia tatizo hivyo itamlazimu kutumia sheria kali na za kibabe ili kuendesha utawala wake.

Vyombo mbalimbali vitanyimwa uhuru wa kutoa mawazo yao hii itapelekea vyombo vya habari vya magharibi kumuulika nchi na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Swali la kujiuliza, Rais ajaye atakuwa nani ?

Ni vigumu kupata jibu la moja kwa moja ingawa watu wengi wanatazamia kuona sura mojawapo kati ya hizi:
- Zito Kabwe,
- Dr. Willbrod Slaa,
- Dr. Asha Rose Migiro,
- Edward Lowassa.
- Samwel Sitta
- Prof. Ibrahim Lipumba.
- Bernad Membe, na
- John Pombe Magufuli
.

Kwanini Watanzania wengi wanategemea kati ya watu hawa mmoja wapo atakuwa Rais wa Tanzania mwaka 2015?
Jibu kubwa na la msingi ni suala zima la uwajibikaji na kujituma.

Kwanini nasema hivyo?
Ukiangalia sura zote ni watu wachapa kazi, wanajituma na wenye maamuzi magumu kwa masuala nyeti ya nchi. Ingawa kila mmoja ana mapungufu yake lakini ukweli bado unabaki pale pale wanauwezo mkubwa wa kulifikisha taifa pale Watanzania wanapotaka ikiwa watatekeleza majukumu yao ipasavyo.

Bado suala la wapinzani kuungana na kumsimamisha mgombea mmoja litakuwa ni ndoto. Kwanza utofauti wa sera na mawazo yao vinakinzana. Pia kuna suala zima la itikadi ya chama na mitazamo. Wapinzani wamejifunza mengi kutoka kwa jirani zao Kenya. Hivyo hawapo tayari kuungana na kuanza kung'ang'aniana madaraka ni bora kila mmoja ashiriki kwa nguvu zake na ashinde kwa nguvu zake.
Kumbe hiyo roadmap ilichorwa tangu 2012, ok! lakini mkae mkijua hiyo Mikakati ovu ya kulinda madaraka itatugharimu wote, kisiasa kijamii na kiuchumi, baada ya miaka 10 nchi itakuwa masikini sana
 
Kama baadhi ya mambo aliyosema yametimia asilimia mia basi na hilo litegemee mkuu huenda n muda tu, ila uyu alietoa uzi kama s mchawi basi ana maono ya mbali sana
mkuu,nilivyomwelewa jamaa amesema raisi ni either awe dikteta au mwenye maamzi magumu,na mm ninadhan huyu jamaa ni ama mchawi au ana mawasiliano na mbingu
 
jamaa alishaona uwezekano wa mkapa kumpitisha waziri jiwe..
na katika orodha aliyoitaja ni jiwe tu ndilo lililoonesha roho nyeusi yenye choyo kwa walionacho tangu akiwa waziri..
magamba alitoa utabiri akijaribu kufikiria nini kitatokea ikiwa mkapa atampitisha mvunja nyumba ya mamamkwe !
 
.2. Pili ni ahadi atakazozitoa hususani zile za kushughulikia "MAFISADI". Ili kupambana na aliyekuzidi kifedha lazima uchukue fedha zake kwa nguvu hivyo atataifisha mali za waliosemekana ni wahujumu uchumi au mafisadi. Akiwa yupo kwenye hali hiyo lazima watamwinda hivyo itamgharimu kuwa dikteta katika kupambana na mafisadi ikiwa ni pamoja na kunyonga baadhi yao ili kuweka fundisho. Pia atajikuta analipa kisasi cha mateso yote yaliyompata katika harakati za kuingia ikulu.
Mkuu umetoa Siri za watu wa deep state, unapaswa kushughulikiwa lakini pia umetufumbua macho kumbe yanayowapata matajiri akina (zacharia, ruge, manji,MO, iqram, huenda atafuatia jeetu,) ni mpango wa kuwanyanganya utajiri kwa nguvu??
 
Hapo ndo wengi wanakosea magufuli hakuja kwa bahati mbaya alikuja kurekebisha mambo flani flani ya nchi though hzo ni kama changamoto pia za mtazamo wa watu
Alafu shida ni kwamba wanaangalia haya yanayotokea kisha wana muatack magufuli personally,!

Hawaangalii urais kama taasisi..
 
Mkuu umetoa Siri za watu wa deep state, unapaswa kushughulikiwa lakini pia umetufumbua macho kumbe yanayowapata matajiri akina (zacharia, ruge, manji,MO, iqram, huenda atafuatia jeetu,) ni mpango wa kuwanyanganya utajiri kwa nguvu??
Exactly what's been clicking in my medulla.
 
Mkuu umetoa Siri za watu wa deep state, unapaswa kushughulikiwa lakini pia umetufumbua macho kumbe yanayowapata matajiri akina (zacharia, ruge, manji,MO, iqram, huenda atafuatia jeetu,) ni mpango wa kuwanyanganya utajiri kwa nguvu??
We huoni anayofanya/alivyofanya crown prince wa saudia,aliwaweka ndugu zake wa damu na matajiri wengine ambao anaona ni tishii kwake kizuizini kwenye 5 star hotel huachiwi mpaka utoe asilimia kadhaa ya utajiri wako same modus operandi anayotumia my nigga Jiwe minus the 5 star treatment tho coz this is africa.eidha ufilisiwe,upunguzwe nguvu ama utoe gawio endelevu.
 
Mkuu/Kiongozi wa hiyo taasisi ni nani?
Tena kiongozi wa hiyo taasisi kuna wakati amesema HAPANGIWI WALA HASHAURIKI.

kwa hali hiyo lazima watu wamshambulie yeye personally. Na sababu hasa ni yeye mwenyewe kujiamini kama ni taasisi bila washauri wake
 
Back
Top Bottom