Emmanuel J. Buyamba
JF-Expert Member
- May 24, 2013
- 1,168
- 656
Mkuu,wewe ndiyo umeanza kuyajua haya!? Msome Yericko Nyerere hapa kwa kifupi ktk kitabu chake cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.Mkuu umetoa Siri za watu wa deep state, unapaswa kushughulikiwa lakini pia umetufumbua macho kumbe yanayowapata matajiri akina (zacharia, ruge, manji,MO, iqram, huenda atafuatia jeetu,) ni mpango wa kuwanyanganya utajiri kwa nguvu??
NADHARIA TATA YA MAUAJI NA UTEKWAJI WA WATU.
Leo nataka nikufundishe dhana moja ngumu kidogo hasa kama ni mgeni katika ulimwengu wa kijasusi, Nilipoanza chuo katika masomo ya Forensic Psychology niliona ni masomo mepesi nikahisi huenda nimechagua mchepuo wakitoto, lakini kadili ninavyopanda na kuingia katika uwanda uliopevuka, najifunza kitu kikubwa ambacho huenda sisi huku Afrika tunajipunja kwakuwa hatuyatafuti maarifa haya na kufunza vizazi chetu.
Kwa hakika hili ni pigo kwetu, Naaam, ukisoma kitabu cha Ujasusi wa kidola na Kiuchumi Sura ya 2, Ukurasa wa 306 nimeeleza juu ya Kinga za Kijasusi, nimeeleza kuwa, Kwenye nchi yoyote ile duniani katika mambo ya utawala na uongozi, kuna kitu kinaitwa National Intelligence na kingine kinaitwa State Intelligence.
National Intelligence huwa ipo kisheria (Legal), na State Intelligence huwa haipo kisheria (illegal au unauthorised). Wanaweza kufanya kazi moja, mahali pamoja, nk. Tofauti yao nikuwa kimoja Natinal Intelligence kinafanya kazi chini ya miiko na taratibu za kisheria kwa nchi husika, na State Intelligence hakitambuliwi na sheria yoyote zaidi ya (decree) na mara nyingi huwa hakifahamiki na wengi katika serikali, huenda katika nchi kikafahamika na watu watano au sita tu. Baadhi ya nchi, kila rais au Waziri Mkuu wa nchi huiingia madarakani na watu wake wa State Intel, Katika nchi za kiafrika si lazima wote wawe wamepata mafunzo ya kijasusi, wanaweza kuwa ndugu zaidi, wafanyabiashara, marafiki zaidi nk, ilimradi wanakuwa wapambe wa kiongozi husika. Kazi za kikosi hiki huwa ni hujuma kwamaana ya kuua, kuteka, kuiba katika mabenki ya ndani au ya nje, kupindua serikali yoyote au kumweka madarakani rais/waziri mkuu yoyote katika nchi yoyote, inategemeana na matakwa ya mmiliki wa kikosi husika.
Nchini Marekani ndani ya shirika la ujasusi la CIA, kuna kikosi kinaitwa Special Activites Division (SAD), Hiki huendesha shughuli zenye maslahi ya rais, chafu, mbaya na pia dhalili zenye maslahi kwa nchi na muda mwingine kwa maslahi ya wakuu katika nchi au katika vikosi husika. Uwepo wacho hautambuliwi na katiba wala sheria yoyote.
Nchini Israel, serikali ya Tel Aviv chini ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ina kikosi cha siri kiitwacho Kidon, au kwa lugha ya kiswahili kinaitwa ncha ya mkuki, hiki ni kikosi kisichotambuliwa na sheria yoyote ndani ya Israel, na hata utambulisho wa maafisa wake hakuna aujuae. Sehemu kubwa ya shughuli zake ni mauaji na hujuma kwa yeyote anayepinga au kuukosoa utawala wa Tel Aviv, awe wa ndani au wa nje ya Israel. Kikosi hiki kimefanikiwa kuzima harakati zote za kiarabu na makundi yote ya kiislamu yenye msimamo mkali kwakuua mmoja baada ya mwingine.
Nchini Urusi nako ikulu ya Kremlin chini ya Vladimir Vladimirovich Putin ina kikosi ndani ya jeshi kitwacho Spetsnaz ambacho ni cha makomandoo walioiva zaidi kabisa katika ardhi ya Urusi, na kazi yake kubwa ni hujuma za kinchi, oparesheni maalumu za kinchi na kudhibiti wapinzani wa kisiasa na wanaharakati nchini Urusi, kikosi hiki kipo ndani ya jeshi la Urusi lifahamikalo kama Red Army japo kinaundwa zaidi na maafisa wengi kutoka shirika la Ujasusi la nchi hiyo la FSB, sehemu ya shughuli zake (activities) hazitambuliwi kwa sheria yoyote ndani na nje ya Urusi. Alipoingia madarakani Putin alikitumia kikamilifu kikosi hiki kuwadhibiti kwakuwapoteza wapinzania wake nchini pia alifuta matajiri wote aliowakuta na kisha kutengeneza matajiri wengine wanaokuwa royal kwake. Kuwafungulia kesi na kuwaua kwa sumu ni moja ya mbinu inayoaminiwa kwa kiwango kikubwa na mamlaka za Kremlin. Rejea mauaji ya 23 Novemba 2006 ya Alexander Valterovich Litvinenko, na jaribio la mauaji ya 04 Machi 2018 ya jasusi kicheche (double agent) wa Urusi na Uingereza bwana Sergei Viktorovich Skripal na bintie Yuri.