Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Ndugu zangu,
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 Freeman Mbowe aliutangazia ulimwegu jinsi alivyohusudu utawala mpya wa Jakaya Kikwete huku akiwaponda wanasiasa wengine kama Prof. Lipumba aliyelalamikia madhaifu ya tume ya uchaguzi. Mbowe na CHADEMA walirukaruka kama ndama wakifurahia Serikali mpya ya "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania"
Wakati Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani mwaka 2015 siku 100 za mwanzo aliibuka Salum Mwalim akaitangazia Dunia kuwa Serikali ya "Hapa Kazi Tu" kwa asilimia 100 ilitekeleza sera za UKAWA.
Na sasa ndani ya siku mia moja za Rais Samia makamanda ghafla wanalazimisha kuonekana wenye furaha, wakigonga tano wakiamini Serikali ya "Kazi Iendelee" inatekeleza sera zao.
Vituko haviishi hadi kufikia tarehe 1.7.2021 tutaanza kuona na kusikia mitambo ya matusi ikiwashwa upya dhidi ya Serikali ya Rais Samia (CCM) na hapa rasmi Chongolo na Shaka nao wataanza kusakamwa na makamanda kama ilivyokuwa Dr. Bashiru na Polepole walipotekeleza majukumu ya kuhakikisha CCM inaendelea kushika dola.
Muda utasema!