Kamanda jikite kwenye hoja sasa,Rais Samia ni CCM
Kwa vile umeona ujikite kwenye hoja sasa ni jambo la kheri. Tatizo ni kuwa hata kwenye mambo serious mnaweka ushabiki na hata bila ya kujali athari zake.
Hii nchi tusingeweza kweli kuvuna sote yaliyo bora zaidi? Kwani watanzania wote ni mashabiki wa vyama vya siasa kama wa Namungo tu?
Nikikurejea kwenye hoja kumbuka zaidi sana ya uCCM na uChadema, kuna na watanzania wazalendo pia ambao ni wengi tu. Kiasi kuwa nani alijiunga lini wapi inakuwa na maana labda kwako tu, kama ungali na wenge la msiba kuliko wafiwa wenyewe.
Baada ya kukupa utangulizi huo mfupi, napenda sasa nikupe msingi wa hoja kama nilivyokuwa nimekupa pale awali:
"Kwa utabiri wako ungemalizia kwa kusema 'asema nabii Tito' ungeeleweka vizuri zaidi.
Ila wewe kama si nabii huyo si mbaya ukiyajua haya bayana:
Hadi sasa mama kama binadamu anakwenda vizuri. Akiendelea hivyo ataendelea kuungwa mkono zaidi na zaidi.
Tusitegemee mama kuzinguliwa na waungwana unaowalenga kama ataendelea kusimamia haki, uhuru na zaidi sana asiposahau kutoa mrejesho na kuchukua hatua stahiki kwenye:
1. Ripoti za CAG zikiwamo za TPA na BOT za Mar 2021.
2. Ripoti ya tume ya wataalamu kuhusiana na Corona.
3. Lile kundi dhwalimu lililotaka kumzimia yeye urais.
Akitufikisha kwenye hatima ya mzizi wote wa fitina, yaani kupatikana kwa katiba muafaka mbona mama atastahili mitano tena baada ya 2025 iliyo ya heshima na taadhima kubwa?
Eeh mola wetu hebu ukamjalie hekima na busara rais wetu aendelee kuyaumbua manyang'au haya yasiyomtakia yeye na nchi hii taratibu mema."
Ni hayo tu mkuu. Karibu.