Kuanzia leo, biashara ya bar imeniogopesha


Sioni kitufe cha like ningekupa tano
 
Ukweli ni.kwamba Biashara zetu nyingi sana zinakosa Customer Care hasa pale tunapopata wateja
 
Usiogope mkuu, hakuna biashara inalipa kama pombe duniani, sema Jacaranda mwenyewe kafa (if am not mistaken), mbona kona bar, barakuda, yenu, mawenzi, pazi, hongera (kwa uchache) zipo hadi leo na zinafanya vizuri tu, sema usimamizi tu ndo muhimu na wanywaji wa Kinondoni huwa wanafuata upepo wapi iko mpya ndo wanajazana.
 
Hili swali la msingi, na kuna ukweli wengi wanaofungua bar huwa wanaenda singida au manyara kufuata manyara sijui kwa nini......
Hujui kwa nchi hii wasichana wakali wanatoka singida?
 
kwa nini wanatokea ukanda huo?? Au ni kama ambavyo mahausi girl wengi inasemekana wanatokea Iringa??

Haswaa...ipo hivyo mkuu pia usisahau wana rangi ya mtume mkuu!
 
car paking pia ni factor especially bar za pembeni ya barabara.kuna bar inaitwa calabash ile haitakaa ife itasumbua sana hapa town kwa muda mrefu

Ni sawa mkuu ila mbona hata hiyo jacalanda ipo pembezoni mwa barabara kama calabash na paking ni kubwa tu?
 

Kinondoni na kufuata upepo. mnaikumbuka shentemba hata mawaziri tulinawa nao
 
Walevi huwa hawana mwamana...kuhama hama ni jadi yao...

Pia kama jikoni haupo vizuri tegemea kufunga baa tu
 

uko sawa mkuu hapo kwenye wahudumu waliojazia jazia atile mkazo hswaaa
 
Fungua baa, weka mademu warembo...na wanaojali wateja


Duu! Ivi wanawake wao wanafaidi nini? Make hao wanawake wazuri itakua kwa ajili ya wanaume,
Mbinguni kuna bikra 72 kwa ajili ya wanaume.



BTW, mwanzisha mada hajatuambia alienda tarehe zipi apo awali, assume alienda mwisho wa mwezi mara ya kwanza, afu akaenda jana, lazma tofauti iwepo.
 

White wizard you are partly right ila kivutio kwa pombe bado ni wanawake believe me. Mimi si mteja wa hiyo kitu ila niko kwenye business so nakuwa na interest kufuatilia waliofanikiwa ili nijue ni nini kimefanya wafanikiwe. Nilichokiona kwa Kisuma ( By the way wako share jamaa watatu) ni kwamba wanacheza na akili za wateja. Wao wana bar tatu wako mbioni kufungua ya nne, wanachofanya ni kuwazungusha bar maids kwenye hizo bars kwa transfers za mara kwa mara so maids wanakuwa wapya kila siku kiasi wateja hawawachoki. Na wakiongeza hiyo ya nne mchezo kwao ndio utakuwa mrahisi zaidi.
 
hizo bar watu wamezikimbia kutokana na wimbi la kuibiwa unawekewa madawa unazima wanakuibia mpaka chu.pi,pia mateja na mashoga kupiga vibomu na kuganda watu,achana nao wale.misheni.town wanaojifanya stori nyingi ili wakiombe bia.

True, me huwa nashindwa kuelewa Mtu anawezaje kunywa pale kwa hali kama hiyo ya usalama mdogo (kwa ujumla Kinondoni yote).............pilikapilika za mashoga na Wahuni!!
 
Wanaominyaminya mabega ya mteja wakisubiri maagizo,

koma kabisaa, wahudumu wenye mazowea ya faster ndiyo mwanzo wa kujitongozesha na kupiga mizinga. mhudumu anatakiwa awe mchangamfu lakini asiwe na mazowea yasiyo na msingi, binafsi nikiingia bar huwa napendelea kuhudumiwa na mhudumu wa kiume.
 
Biasharaa ya bar ni huduma ya uhakika, jiko la maana, wahudumu wa bashasha na kujua aina ya wateja unaotakaa.
Otherwise ni biashara yahitaji sana kukuna kichwa na kutokubweteka asilanii.
Vp rose garden dar badoo inabambaaaa??
 
Ukitaka Bar idumu ajiri Meneja ambaye anajiheshimu na asiyetembea na wahudumu wake ili awe na sauti ya utawala juu yao. Ajiri wahudumu wanaofahamu nini maana ya kazi, wanaofahamu huduma kwa mteja ninini, wasioendekeza ngono maana ngono hupelekea wivu na magomvi kwa mteja hasa akifika mahali hapo na mke wake au ndugu/jamaa yake wa kike. Mwisho wake muhudumu huanza kutoa huduma kwa kinyongo au asitoe kabisa. Mwisho walipe vizuri kulingana na hali ya maisha ilivyo ili waishi kama binadamu wengine.

Kwa uzoefu wangu bar na ikifikia wahudumu kuonea wivu mwanamke yeyote anayeingia baa na mteja, na bado meneja asilione hilo hapo lazima ifungwe. Mameneja makini hugundua mapema na kuondoa generation yote hiyo na kuajiri wengine....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…