Yes,View attachment 3680238
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limeanza operesheni maalumu ya kuwabana waendesha bodaboda na bajaji wanaokiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.
Operesheni hiyo, inayoanza Septemba 29, 2026 na kutekelezwa nchi nzima, inalenga kuongeza utii wa sheria na kupunguza makosa yanayoweza kusababisha ajali, majeruhi na vifo.Miongoni mwa mambo yanayolengwa ni matumizi ya kofia ngumu, idadi ya abiria na utaratibu wa kukaa ndani ya bajaji, pamoja na makosa mengine ya usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP William Mkonda, ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya madereva wa pikipiki na bajaji pamoja na viongozi wa wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.
SahihiWakague na leseni kama hata wanazo!!😁
Kweli aiseee ,bodaboda wamekufa sana barabarani kwa kutofuata sheria ,Bodaboda wa Rwanda wamenyooka kama Rula hawavunji sheria hata kidogo ,ili kuwakomesha polisi wasiwachekee yaani wakivunja sheria ni kamata pikipiki na dereva weka ndani.
Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani limeanza operesheni maalumu ya kuwabana waendesha bodaboda na bajaji wanaokiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.
Operesheni hiyo, inayoanza Septemba 29, 2026 na kutekelezwa nchi nzima, inalenga kuongeza utii wa sheria na kupunguza makosa yanayoweza kusababisha ajali, majeruhi na vifo.Miongoni mwa mambo yanayolengwa ni matumizi ya kofia ngumu, idadi ya abiria na utaratibu wa kukaa ndani ya bajaji, pamoja na makosa mengine ya usalama barabarani.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP William Mkonda, ametoa maelekezo hayo wakati akizungumza na viongozi wa vyama vya madereva wa pikipiki na bajaji pamoja na viongozi wa wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam.
Asilimia kubwa ya boda hawana leseni,mtu anajifunza pikipiki mtaani leoKweli aiseee ,bodaboda wamekufa sana barabarani kwa kutofuata sheria ,Bodaboda wa Rwanda wamenyooka kama Rula hawavunji sheria hata kidogo ,ili kuwakomesha polisi wasiwachekee yaani wakivunja sheria ni kamata pikipiki na dereva weka ndani.
Boda wa mamaMaafisa usafirishaji tiali wameshageukwa na mbogamboga 🤣