Kuanzia sasa mimi na wanawake basi, inatosha!

Kuanzia sasa mimi na wanawake basi, inatosha!

Gol D Roger

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2023
Posts
2,316
Reaction score
6,082
Maybe haya mambo ya mahusiano sio fungu langu, maybe nalazimisha nisipopendwa, ila ninachojua ni kwamba, umri wa kuishi wa binadamu ni miaka 70, acha huu muda uliobaki ni-enjoy mwenyew bila stress.

Ningekuwa nina kilema ningejua sababu ni nn, ningekuwa maskini ningejua shida iko wapi, ila wapi, inatosha sasa maana stress ninazopitia zitanizeesha kabla ya muda wangu.

Haya mapenzi sio kwa kila mtu, nami nimekuja kukubali kwamba sina nafasi kweny kweny ulimwengu wa mapenzi.

Nimemlisha, nimemvisha, nimemtibu, nimemtibu mama ake na kukesha nae hospitali, nilimpa sweta langu alivosikia baridi, nilimpa soksi zangu alipo ng'atwa na mbu, nilimpendezesha akanawiri na kunukia vizur, nilimnunulia feni aliposikia joto, nilipambana apate kazi na akapata, ila hayo yote ni bure, kwasababu mwisho wa siku, mwanaume ndiye anayechukua lawama siku zote.

Nilijitahidi sana kumtunza, na kumheshimu, but nilichokuja kuambulia ni maneno ya dharau na kejeli.

Ni kweli nimepoteza muda na pesa nyingi, but yashapita na mimi nimekubali, kuanzia sasa huu muda na resources nilizokuwa nazo nitazielekeza kweny mambo yangu na mikakati yangu, from now on its going to be all about me, my growth and my happiness.

Kuanzia sasa sitakuwa na mpenzi, na wala sitakuja kuwa mke, na sio kwamba wanachukia wanawake, lahasha, wanawake ni watu poa sana labda mimi tu sina bahati.

"My life doesn't have to be Perfect, It just has to be reasonable"
 
ikitokea umependa Tena which is more likely kama hujaenda kuhasiwa

1.stop being "MR NICE GUY"
2.Stop showing that you need her ( Stop being needy)....you might want her but "need" stop that...hapa ndo madharau yanaanziaga hapa mtu anpohisi unamuhitaji zaidi ya anavyokuhitaji

3.lower your expectations...... expectations zako ndo zimeleta hili yowe lote hapa .....kama unamsaidia mtu kwa kumpenda msaidie siyo unamsaidia huku kichwani unawaza ipo siku atakulipa fadhila....mtu unayempenda na umempa vitu kwa kumpenda huwezi kuumia kama mkiachana maana umetoka kwa upendo hujatoka ili ulipwe kwa namba yoyote ile
 
Maybe haya mambo ya mahusiano sio fungu langu, maybe nalazimisha nisipopendwa, ila ninachojua ni kwamba, umri wa kuishi wa binadamu ni miaka 70, acha huu muda uliobaki ni-enjoy mwenyew bila stress....
Mkuu ndio ninachopitia hapa , i swear nikipona sitarudia tena nimejifunza, yani unakuwa loyal sio mambo mengi ila unavyokuja kulipwa 🙌.
 
Mungu alishasema ishini nao kwa akili mkuu pole sana Cha kukushauri endelea kutafuta pesa mapenzi huwezi kushindana nayo naamini ukiwa na pesa watakuja wenyewe
Sasa hao c ni lamba lamba kumbuka huyu mtoa mada anahitaji true love, na yeye atajitoa as mwanaume kuhudumia, what if anakuja mtu kumbe yuko kima slahi?.
 
Back
Top Bottom