Kubabaika: Kaulizwa Rais wa EU, anajibu Balozi wa Tanzania

Kubabaika: Kaulizwa Rais wa EU, anajibu Balozi wa Tanzania

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Tanzania hatujawa na njia sahihi ya kukabiliana na tuhuma mbalimbali za kimataifa tunazotuhumiwa nazo ziwe za uongo au kweli.

Hoja zilizojadiliwa juzi na Kamati ya kudumu ya Mambo ya nje ya bunge la EU chini ya Mwenyekiti wake David Mc Allister kuhusu Tanzania zilikuwa nzito kulikuwa hakuna haja ya kukurupuka na kujibiwa na balozi tena kwa kuzikana tu bila evidence yeyote.


Hata kama tuhuma ni yetu lakini hatukuulizwa sisi aliyeulizwa ni Rais wa Council wa EU bwana Charles Michel kuwa alitumia vigezo gani kuipatia Tanzania msaada wa €27m, sisi (balozi) tungesubiri majibu yao huku tukijiandaa kujibu jinsi tulivyozitumia kwa sababu vigezo walivyotumia kutupatia msaada havituhusu.

Tayari tumeshaonyesha dalili za mwanzo za kubabaika, kwanza balozi alikana kuwa hakukuwa na mjadala wowote kuhusu Tanzania baadaye akasema tulijadiliwa na wabunge watano 5 tu ambao hawawezi kutuwekea vikwazo, hii siyo sahihi ni sawa na kuingilia utaratibu wa uendeshaji wa bunge lao.

Nasikia balozi wetu nchini Ubeligiji kamwandikia barua bwana McAllister ya kuomba kukutana naye, well, je amejipanga with evidence kujibu tuhuma akiulizwa kwanini polisi ilitumika kuwaondoa mawakala wa upinzani vituoni?, Je amejipanga with evidence akiulizwa matumizi ya €27m? Je amejiandaa with evidence kusema waliokufa kwenye uchaguzi ni wawili tu na sio 20 na hao wawili waliuawa na nani na wauaji wamechukuliwa hatua gani.
 
Balozi wa Tanzania Belgium amejibu hoja kwa kujikanyaga kanyaga, kaenda off point kabisa na kuongelea yasiomuhusu na ambayo hayakujadiliwa kabisa na kamati.

Kakimbilia kusema Tanzania hatujawekewa vikwazo, kama vile watanzania hatujaelewa Kamati Ya Bunge La Eu limejadiliana kuhusu nini.

Angesimama kwenye point tatu kuu (Japo hana mamlaka ya kuzijibu na hayamhusu);

1) Vigezo vilivyotumika Tanzania kupewa EURO MILLION 27 kwaajili ya kupambana na Covid-19, wakati rais alishatangaza hakuna Covid tanzania.

2) Hela hizo EURO MILLION 27 zilitumika vipi.

3) Kwanini EU (Pamoja na wafuasi wake) wasizuie misaada yote ya hela kwa serikali, na hela hizo wasiwape na kuwafadhiliwa wanasiasa wanaotetea demokrasia & haki za binaadamu nchini Tanzania. Badala ya kuifadhili hela serikali ya Tanzania isiojali na kulinda demokrasia/haki za binaadamu.

#Aliekamata kisu cha kuichinja serikali ya tanzania ni Balozi Wa Eu nchini tanzania, hizo hoja atakavyo zijibu pindi atakapoenda Katika Tume hio ya bunge, ndio itakua hatima yetu kama taifa.
 
CHADEMA inawauma sana balozi kujibu uzushi wenu, mnataka muipangie hadi serikali nani aseme nini? Hiyo ndio kwishney, baada ya miezi mitatu hakuna atakayekumbuka ujinga wenu.
 
Mkuu labda watu hawaelewi zile ni hoja na sio maamuzi kwahiyo hoja zile zitafanyiwa kazi na watu husika yataletwa majibu bungeni,majibu kama yataonekana ni kweli ndio utaratibu utafuatwa wa kupiga kura kama tanzania iwekewe vikwazo au laaah,
Na kila vikwazo vinaukomo wa makosa
Nikiweza nda upload makosa na vikwazo unavyoweza kuwekewa kwenye makosa kama haya
 
1. Ingekuwa hoja binafsi kwa huyo Mr wa EU, isingekuwa suala la public na angepelekewa barua rasmi privately. Utasema, "Si ni mjadala bungeni?" Well, ndiyo maana ya hoja ya msingi hapa kuwa haikukusudiwa kuwa kitu personal ya huyo jamaa yenu.

2. Kubabaika na kuzushazusha na kupotoshapotosha kwa BAVICHA ndiko kumemfanya Balozi ajitokeze ili kuweka mambo sawa.

3. Lastly, wakichelewa kujibu, "WANAOGOPA HAO!" Hoja zikijibiwa kwa wakati, "WANABABIKA HAO!" Nyie veeeepe??? "Ukichimama, nchale! Ukikaa nchale! Ukiinama, ukiinuka, ukikimbia, ukitembea, nchale, nchale, nchale!!"
 
CDM inawauma sana balozi kujibu uzushi wenu, mnataka muipangie hadi serikali nani aseme nini? Hiyo ndio kwishney, baada ya miezi mitatu hakuna atakayekumbuka ujinga wenu.
Saivi mda wa kuokoteza kila hoja, wana jazba bado, mpaka Sief aingie katika SMZ na Dodoma Wabunge wao waende mwezi wa 6 baada ya njaa kali ndo watajua hawajui
 
1. Ingekuwa hoja binafsi kwa huyo Mr wa EU, isingekuwa suala la public na angepelekewa barua rasmi privately. Utasema, "Si ni mjadala bungeni?" Well, ndiyo maana ya hoja ya msingi hapa kuwa haikukusudiwa kuwa kitu personal ya huyo jamaa yenu.

2. Kubabaika na kuzushazusha na kupotoshapotosha kwa BAVICHA ndiko kumemfanya Balozi ajitokeze ili kuweka mambo sawa.

3. Lastly, wakichelewa kujibu, "WANAOGOPA HAO!" Hoja zikijibiwa kwa wakati, "WANABABIKA HAO!" Nyie veeeepe??? "Ukichimama, nchale! Ukikaa nchale! Ukiinama, ukiinuka, ukikimbia, ukitembea, nchale, nchale, nchale!!"
Bavicha wamepotosha kitu gani.
 
Back
Top Bottom