Kubadili Usukani wa gari kutoka kushoto kwenda kulia

Inawezekana. Cheki na mkuu Isanga family amekushauri vizuri.
 
Naona Uko North Korea huko😅😅😅
 
Niliona Rwanda wanafanya sana
 
Inawezekana, ila ni Sawa na kubadilisha jinsia! Gari itakuwa trans! Vitu vingi na mifumo mingi itakuwa ya kuchonga, na LAZIMA itaketea shida na ile natural feel ya gari itapotea!

Ushauri:
1. Endesha hivyo hivyo ikiwa LHD
2. Uza masoko ya Rwand na Burundi ..ununue RHD
 
Nipo SA naweza kubadilisha hilo kazi nafanyia Arusha..
Utanunua dashboard na mfumo wa waya wa umeme wa dashboard ukiwa serious nitafute nikupe idadi ya vitu vyote utatakiwa kununua hapa vinapatikana ila litakugharimu sana ni Jeep hilo..

Huu ni uoga, sisi wa Tanzania tunaweza nini ama udaku tu?
Mbona Jeep Wrangler zipo kibao tu za right hand. Sioni sababu ya kuingia gharama kubwa hivyo.
 
Bora uchukue right hand ya petrol halafu hizo gharama za kubadilisha usukani kwenda kulia utafidia kwenye mafuta.
Right hand zina engine ya 3.6 v6, very powerful and reliable.
 
Mwaka 2006/2007 mzee wangu alinunua LandCruiser, ilikuja hvi hvi kma unavyosema, Alienda kuibadilishia dsm hapo na ilichukua kama week hivi.

Bahati mbaya sana ni kua mshua kashafariki, So sina pa kukuelekeza au kukupa mchakato kamili na bei zake.

Lengo la ku-comment hapa ni kukwambia kua inawezekana sana tu kwa hapa dsm ila ndio vile unatakiwa kujiandaa vizuri kiuchumi na pia komaa utafute Garage nzuri, Kama ni german Car, fika garage za german cars, Watakupa majibu mazuri na ya uhakika pamoja na ushauri mzuri.

Humu ndani utajibiwa kwa kupayuka na stori za kitaa.

Tafuta muda tembelea hizo garage kadhaa zenye huduma za kueleweka, then compare majibu na gharama za pande tofauti, halafu fanya maamuzi.

Kila la kheri.
 
Saafi, shukran sana, wewe umenipa mwanga mkali.

Lakini baada ya kuibadilisha si ulitulia fresh tu haikuwa na Shida yoyote?
 
Gari lolote linalo-katwakwatwa linakuwa sio bora tena....linakuwa dhaifu.
 
Ukiweza kupata "donor car" kwenye scrap yards kama tandale, itapunguza gharama kwa kiasi fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…