Chura
JF-Expert Member
- Sep 22, 2009
- 1,385
- 2,402
29.1.2023 Necta imetangaza rasmi matokeo ya kidato cha nne (CSEE) 2022, matokeo haya yamekuja na utaratibu mpya ambapo hakuna kutajwa nafasi ya shule kitaifa na kimkoa maana yake pia hakuna utaratibu wa kutaja shule zilizoongoza kitaifa sanjari na hayo NECTA imefuta utaratibu wa kutaja wanafunzi waliofanya vizuri kitaifa maana yake zile mbwembwe za kwenda kupongezwa bungeni na kuitwa TO zimezikwa rasmi.
Vijana wa shule kama Mzumbe, Ilboru, Kibaha na nyinginezo watakuwa hawasomi kwa mzuka tena ili kuibuka kipanga wa TAIFA(TO). Moja ya sababu iliyotajwa ni kuwa NECTA imeona kwa kutangaza shule zinazofanya vizuri inazipa promo la bure shule hizo, hapa sijui wanataka shule zianze kulipia matangazo 🤣 anyways ya NECTA tuwaachie wenyewe.
Taratibu mpya za utangazaji matokeo za NECTA hazijafanya jitahada za baadhi ya shule zisijulikane, hapa nazungumzia maajabu yaliyofanywa na shule kutoka mkoani BUKOBA ijulikanayo kama KEMOBOS, shule ya KEMOBOS kama ingetokea NECTA imetangaza shule 10 bora za mwaka 2022 bila shaka hii ingeibuka kidedea. Iko hivi ndugu zangu.
KEMOBOS ilikua na watahiniwa 68 katika hao watahiniwa 68, watahiniwa 65 wamepata daraja la kwanza la alama saba(1.7) maana yake wanafunzi 68, 65 wamepata A saba na kuendelea kwenye jumla ya masomo yao.
Watahiniwa wawili ambao kwa shule hiyo tunawachukulia kama watahiniwa wenye uwezo wa wastani wamepata daraja la kwanza la alama nane( 1.8)
Mtahiniwa mmoja ambaye kwa KEMOBOS unaweza sema ndo mtahiniwa mwenye uwezo dhaifu/mdogo au wa chini amepata daraja la kwanza la alama 9 (1.9)
Maajabu hayajaishia hapo katika watahiniwa wote 68 zaidi ya watahiniwa 32 wamenyoosha A kwenye masomo yote waliyoyafanya yani madogo hawa wamekung'uta A kuanzia hesabu hadi Kiswahili.
TETESI: Tetesi Hizi nimezipata kutoka kwa watu wa karibu kabisa wanaohudumu kwenye taasisi hii inayohusika na mitihani ya TAIFA tetesi zinadai matokeo yalikua yatangazwe siku moja baada ya yale ya kidato cha pili 2022 kutangazwa, ila yakasogezwa mbele kwa sababu zifuatazo,
1. Mtihani wa taifa 2022 hakukua na mwanafunzi wa serikali hata mmoja aliyeingia 10 bora. Wote walitoka shule binafsi(private) ambapo watano KEMOBOS, watatu Saint Francis, na wawili Fedha schools.
2. Katika mtihani wa taifa 2022 hakuna shule ya serikali imegusa top 10 kinyume chake shule 10 za mwisho zilizoshika mkia ni shule za serikali sasa hii inaweza haribu sifa ya ana upiga mwingi.
Baada ya kujadili haya ambayo yangesababisha ikaonekana shule za umma hazina elimu bora hivyo kuibua mambo kadha kwa kadha kama mafao duni ya waalimu ikiwemo mishahara na nyenzo mbovu za kufundishia serikali ikaona ije na swaga kwamba "kutaja wanafunzi na shule bora hakuna tija"
3. Kuna siasa za kibiashara zimeingia zenye lengo la kuhujumu shule fulani fulani, kuna baadhi ya matajiri wa mashule wamewalipa watendaji wakuu wa Taasisi hii ili kuvuruga utaratibu ambao umeonekana unazipaisha shule fulani kibiashara .
Mtizamo wangu: Serikali isitumie nguvu nyingi kuficha madhaifu ya shule za umma lazima iyakubali ili zitafutwa mbinu za kusaidia mfano shule za private zina kanuni uwepo wa mtumishi unategemea na anavyofaurisha zaidi ya hapo hana kazi ndo sababu waalimu wa private lazima amalize topic zote zinazomhusu na ataoe mitihani mingi kuwaandaa wanafunzi hali hii ni tofauti kabisa na shule za serikali mwalimu kuingia darasani ni ishu, siku mbili bado NECTA unakuta hata nusu topic wanafunzi hawajafika.
Serikali inatakiwa iangalie namna nzuri ya kuhamisha uendeshaji wa shule za private kwenda shule za umma na sio kuficha takwimu.
UPDATES:
Kama serikali ingetangaza 10 bora kwa shule ziizofanya mtihani wa taifa 2022, kwa kuzingatia GPA 10 bora ingekua kama ifuatavyo
1.KEMEBOS - 1.0670
2.GRAIYAKI SEC- 1.1164
3.ST FRANCIS -1.1449
4.FEZA BOYZ- 1.1506
5.WAJA BOYS -1.1742
6.CANOSSA SEC-1.2028
7.TWIBHOKI SEC -1.2222
8.AHMES SEC - 1.2229
9.BRIGHT FUTURE GIRLS SEC -1.2287
10.MARIAN BOYS -1.2376
*Kwenye attachment nimekuongezea shule 4 maana yake nimekupa 14 bora kitaifa kwa kuzingatia GPA kama NECTA wangetoa takwimu