A
Anonymous
Guest
Mimi ni Mtumishi wa Serikali Kada ya Afya nipo Uyui Mkoani Tabora, nina maoni ambayo pia ni kama kero kwangu na kwa Watu wengi kuhusu mchakato wa Uhamisho wa Njia ya Online kwa Watumishi wa Serikalini.
Serikali ilitambulisha mfumo wa Digitali kwa nia nzuri lakini ukweli ni kuwa umekuwa mgumu kuliko ulivyokuwa offline.
Kumekuwa na vigezo vingi sana ukitaka kukamilisha mchakato wa uhamisho, kama kuna kitu hata kidogo kikiwa hakijakaa sawa kwa amaan ya taarifa kupishana, mfumo haukubali na maombo yako yatakwama.
Jambo lingine ambali ndilo hasa linahusu kero iliyonifanya naindike hapa ni kuwa utaratibu wa uhamisho kwa waajiriwa wapya kwenye vituo kutakiwa kufanyika ndani ya miaka mitatu, inawezekana ni mzuri lakini kuna watu ambao wanataka kubadilishana kwa nia njema, mfumo haukubsli mchakato huo.
Hata inapotokea kama wahusika wote wanaotaka kubadilishana wameridhia lakini mfumo unagoma kwa kuwa umesetiwa kuwa mtumishi lazima akae kituoni kwa muda wa miaka mitatu.
Nashauri utaratibu ungebadilishwa ili kurahisisha kwa kuwa kuna wakati watu wanaweza kuhitaji kubadilishana vituo vya kazi kwa nia njema tena unakuta ni wahusika wa Kada, hapo inamaanisha hakuna kinachopungua lakini mfumo unagoma.
Hali hiyo haileti maana yoyote kwani kulazimisha Mtumishi akae miaka mitatu sehemu moja hata kama ana changamoto inayofanya kutofanya kazi vizuri, inamaanisha ufanisi hauwezi kuwa mzuri pia
Nashauri Serikali iruhusu wanaotaka kubadilishana kama ni wa Kada moja mfumo uwakubalie, vinginevyo inaweza kusababisha Watu kuacha kazi, kutokuwa na ufanisi kwenye vituo vya kazi au kuwa watoro kwenye majukumu yao.