Kubadilishiwa majukumu kutokana na ugonjwa

Omba itabadilishwa kazi ambayo wewe utaimudu.kuna Jamaa yangu alikuwa afisa elimu wa mkoa aliugua kama wewe akaomba akafundishe darasani shule ya msingi na akaimudu ile kazi anaendelea.ila alikuwa anahudhuria hospitali kwa matibabu zaidi na akagunduliwa kuna mshipa shingoni ulikataa mawasiliano.akapata tiba yuko vizuri.nawe nenda hosp Kutana na dkt bingwa wa uti wa mgongo
 
Asante nitajaribu ila vipi haiwezi kuniletea shida wakati wa kithibitishwa kazini au nisubiri kwanza nipate barua yakuthibitishwa ndioniwashirikishe
Tatizo unaangalia sana kazi kuliko afya yako.

Tambua ya kwamba uoga wako ndio utakuongezea matatizo zaidi ushindwe kufanya kabisa hiyo kazi unayoipigania.
 
Hiyo lazma itakuwa kuna shida kwenye pingili za uti wa mgongo. Hta mimi nlikuwa na shida hyo ila nliendaga kwa mzee mmoja anatibia mifupa kwa miti shamba, alinikagua akaipata pingili yenye shida na akaninyooshaga, nilipona kabisa asee, ila sharti alonipa n kwamba nisifanye kaz ngumu zenye kushughulisha mgongo sana, na kunyanyua vitu vizito ndani ya huo mwezi mmoja ili kuupa mgongo utulivu ila baada ya mwezi niendelee na shughuli zangu maana ntakuwa nishapona. Bahat mbaya nlijisahau nikaendekeza kunyandua maumivu ykarud jpo sio makali km ya awali. Jpo ni muda mrefu umepita ila Nitarud tena kwa yule mzee InshaAllah
 
Kwa nature ya napofanyia kaz hakuna majukum mengine yakupewa labda nibadilishiwe sehemu yakaz sababu kiuhalisia nishakata tamaa mpaka nataman niache tuu kazi kunamdaa najilazimisha tuu ila nivile nipo mwenyew
 
Pole sana mkuu
 
Naomba nikuulize haya mambo inbox. Nina haja ya kumjua huyo mzee aliyekusaidia mahali alipo na gharama zake.
 
Duh, pole sana najaribu kuvuta hisia jinsi unavyopata shida maana na mimi hali ya lower back pains ilinikamata kwa miaka 5 ni hatari sana! Nilikuwa hata siwezi kukaa muda wa saa 1 mfululizo kwenye kiti mpaka ikabidi kusitisha masomo ya kozi yangu pendwa maana ilikuwa inanitaka nikae kwenye kupiga msuli muda mrefu. Lakini baadaye nilikuja kupona kimiujiza baada ya kuwa nimetumia madawa ya kila aina mpka kwa mganga wa kienyeji alikuwa anaitwa Chifu nani? Yule Msukuma alikuwa mle ndani ya uwanja wa nane nane pale Morogoro. Sasa najiuliza kwa hali yako huyo umeshaongea na mkuu wako wa idara anasemaje? Umeshaongea na Afisa utumishi anasemaje? Umeshaongea na mkurugenzi wako anasemaje? Kama hao wote hujapata majibu yao itakuwa ngumu sana na utaendelea kujiumiza na mwisho wa siku utaondolewa kabisa kazini.
 
Pole sana kiongozi! Najua mziki wa lower pain. Mimi ilifika mahali hata kukaa kwenye kiti nashindwa natamani tusikilize lectures nikiwa nimesimama, nikiwa home napiga msuli nimelala chali! Mbona nilirudisha mpira kwa kipa!
 

 
Nimetafuta matibabu ila nikaambiwa nikwepe kazi zakuinama nakubeba vitu vyenye uzito zaidi ya 10kg nanilipatiwa dawa ila nimemaliza doz bado sijapona na kukwepa kazi nikitu ambacho haiwezekani sababu nipowenyewe
Hospital gani ulienda,au uliishia hospital za wilaya
 
Ndugu zangu, dawa ipo kama hujafanyiwa operation. Wengi tumepona kwa hiyo Tiba Mbadala.
 
1. Pole kwa changamoto inayokusumbua kiafya.
2. Tafuta kujua undani wa changamoto inayokusumbua na matibabu yake {inaezakua changamoto ya muda mfupi unayoweza kutibiwa na kupona au ikawa ya muda mrefu lifetime}.
3. Nenda kwa Msimamizi wako wa kazi ukiwa na viambata vya kuonyesha changamoto hiyo pamoja matibabu pendekezwa kutoka kwa wataalamu wa afya, na mwisho nenda kwa mwajili wako ukiwa na taarifa zote zilizokamirika,.. i hope utapata msaada. Ahsante.
 
Naomba tafuta vithibitisho vya hospital ya serikali peleka halmashauri unapotanya kazi mwandikie barua Hr kwenda kwa mkurugenzi wataangalia wakupe masijala au hata ofisi kuu ukae masijala au maulizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…