Kubagua Mwanza na Mbeya AFCON haikubaliki

Mnakuwa kama hamuijui hii nchi, yaani mpira utachezwa Dar peke yake. Na mpaka 2027 uwanja mzuri utabakia kwa mkapa peke yake.
 
Ukiamua kusemea jambo la haki basi semea wote sio unaweka ubinafsi eti Mwanza na Mbeya. Vipi kuhusu Kigoma? Kagera? Pwani? Ruvuma? Mtwara? Morogoro? Shinyanga? Kilimanjaro? Iringa? n.k. Huko hakuna watu wanaostahili kujengewa viwanja vya mpira na kutembelewa na wageni pia?

Kama unataka kulazimisha serikali ifanye maendeleo kwa kuangalia vigezo basi ndio ukubaliane na maamuzi yaliyofanyika kuhusu Afcon kwa sababu kuna vigezo wameangalia katika kuchagua hizo city.

Lakini kama unataka haki, basi kila mkoa una haki ya kufanyiwa vitu vyote vinavyofanyika kwenye mikoa mingine yote kwa sababu Tanzania ni moja na watu wake wote wana haki sawa. Hakuna mkoa wenye haki kuzidi mingine na hakuna kabila lenye haki zaidi ya mengine.
 
Mbeya tunahitaji uwanja na kama ni nafasi ya Afcon ,Mbeya ilifaa kuliko Dodoma Kwa sababu kwanza ni rahisi kufikika na Nchi jirani.

Mbeya ipewe heshima yake Kwa sababu nilizoeleza hapo Juu ,tunataka uwanja ,mashindano hayajaisha.
 
Mbeya tunahitaji uwanja na kama ni nafasi ya Afcon ,Mbeya ilifaa kuliko Dodoma Kwa sababu kwanza ni rahisi kufikika na Nchi jirani.

Mbeya ipewe heshima yake Kwa sababu nilizoeleza hapo Juu ,tunataka uwanja ,mashindano hayajaisha.
Kwenye uwanja uko sahihi 100%, mnastahili kuwa na kiwanja kizuri sawa na miji mingine, Dodoma, Arusha, Moro, Mtwara, Iringa, nk...
Ila juu ya Afcon kati ya Dodoma na Mbeya hakuna hekima itakayotanguliza Mbeya mbele ya Dodoma na Arusha.

Kusudio letu ni kuifanya Dodoma kuwa Jiji Mashuhuri, kubwa, zuri, la kisasa, nk... Tumeanza kulipromote na kwa nafasi yake sasa hivi iko nyuma ya mini michache sana Bongo. Miaka 10 mbele itabaki Dar tu hapo mbele ya Dom.

Hoja ya ukaribu si nzito, maana tungefuata kigezo hicho Dar, Dom na Zanzibar hazikupaswa kabisa kupewa nafasi.

Na sisi Morogoro tunasema, kabla hamjaboresha Mwanza na Mbeya, anzeni kwetu kwanza. Lakini pia Tujengewe Airport kubwa kabla ile ya Msalato, au maboresho ya KIA na Songwe Airports.

Ajabu mnaunga mkono wanapofanya ya kipuuzi na mnakosoa wanapofanya mazuri.
 
Umenena mkuu, katika vigezo vya kuzingatiwa ili uwanja uwe umekidhi vigezo vya michezo ya kimataifa ni pamoja na kuwa na hoteli za kutosha za kitalii karibu na uwanja huo, hili ndio limesababisha Arusha kupewa nafasi
 
Ukweli ambao hamtaki kuusema Ni kwamba Arusha Ni focal point ya utalii hapa Afrika Mashariki....kutokupeleka mashindano haya huko Ni kupotrza faida kubwa kwa taifa......Hapa nakuhakikishia ktk maeneo yote Arusha ndio kutakuwa na fan base kubwa sana sababu ya utalii....hata Ile Royal Tour ingekuwa Ni upuuzi mtupu Kama Afcon haotachezwa Arusha
 
Ninyi wenyewe mnaotoka mikoa hiyo ndo hampendi kurudi makwenu, sasa hoteli zitoke wapi
 
Arusha ni part ya blue print iliyoipa ushindi bid ya pamoja.

So sahau kama itaachwa at this stage.

Wahusika wameona panafaa.

Wewe kwa hisia tu huwezi badili uhalisia.
 
Wewe si ndio tukipindea viongozi unaleta uzwazwa...

CCM kirumba wa Mwanza ni uwanja mzuri ila umeachwa umeenda kuchukuliwa wa Arusha wenye kuhitaji ukarabati mwingi, wakati CCM kirumba ilikuwa ni pesa kidogo tu uwanja unakaa shikopa
Umeshasema WA CCM, Sasa unategemea Kodi za wananchi wote ndio ikarabati kiwanja cha jamii Fulani!?!?
 
Acha ushabiki ni kipi ambacho Mwanza inazidiwa na Arusha kwa habari ya kupokea wageni ? Arusha hata hospital ya Kanda hakuna. Sema mmependelewa kwa kuwa na makamu mwenyekiti wa chama dume. Mwanza ina population karibu mara mbili ya Arusha. Leo unatuambia eti Aruaha imeendelea zaidi wakati hotel kubwa nyingi huko Arusha ziko porini.
 
Mwanza kuna hoteli ngapi za kitalii?Mmoja juzi alikuwa analalamika Bureau De Change ipo moja Jiji zima.
 
Ukweli ulio wazi. Na hii italiingizia pato nchi kwa kiasi kikubwa maana watu wengi watatoka nje ya nchi na hivyo kusisimua uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…