Hii tabia ya kubagua Mikoa ya Mbeya na Mwanza kwenye mambo ya Maendeleo naona imeanza kukita mizizi.
Wakati mikoa mingine ikipendelewa sie Mwanza na Mbeya tumekuwa wahanga wa kutengwa na Kubaguliwa kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo licha ya kuwa tunastahili kwa vigezo na sio kwa kuonewa huruma.
Haiwezekani na haiingii akilini eti kubagua miji hii maarufu kwa wanamichezo na badala yake wakaipendelea miji isiyo na mashabiki wala wanamichezo ya Arusha na Dodoma.
Nasisitiza tunadai haki yetu na sio favour kwa sababu zifuatazo;
Mwanza
- Mikoa wa pili kuchangia Pato la Taifa GDP baada ya Dar.
- Jiji la Pili kuwa na population kubwa baada ya Dar.
- Jiji la 3 Kuchangia Mapato ya Kikodi.
- Uwepo wa mashabiki wa kutosha na wanamichezo.
Mbeya
- Mikoa wa 3 kuchangia Pato la Taifa nyuma ya Dar na Mwanza.
- Jiji la 6 Kwa idadi ya watu Tanzania.
- Jiji la 2 Kwa Wanamichezo wengi kama timu za NBC&Championship.
- Pamoja na mtoto Wetu Songwe ni Mkoa wa 4 Kwa mapato ya Kikodi.
Kwa vigezo hivyo pekee tunastahili kupata kitu sio kwa upendeleo bali kwa haki.
Habari za kusema hakuna hoteli au miundombinu ya kisasa na blaa blaa kama hizo zinatokana na Serikali hii ya ccm kuchukua pesa na jasho letu kwenda kujenga Mikoa mingine kama Arusha, Dodoma, Tanga, Dar nk.
Ni aidha Serikali ianze ujenzi wa viwanja vya Kisasa kwenye miji yetu kutufuta machozi na sio lazima kwa ajili ya AFCON bali kutupa heshima yetu kwenye michezo au tumwage mboga 2025.
Hali hii haivumiliki na haikubaliki, ni wakati wa watu wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini kufanya jambo la kujitambua mwaka 2025 endapo wataziba maskio.
Ni bora kumwaga mboga sio kwa sababu tunawakubali Wapinzani bali ni kwa nia ya kukomoana kwamba tukose wote, tumechoka kutengwa na tabia hii ikiendelea ipo siku tutagawana fito.
View attachment 2766050View attachment 2766051View attachment 2766052
Angalizo: Haya ni maoni na mtizamo binafsi, yasichukuliwe kama uchochezi.