Changalucha
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 508
- 593
Kwa lipi mnalochangia hapa Tanzania? Mwanza na Mbeya hatuombi hisani Bali tunadai Haki na stahiki zetuNa sisi huku NTWARA tusemeje?
Imagine Zambia akifuzu ,Mbeya itafurika Mashabiki wao lakini huko Dodoma sijui Arusha ni upuuziNi mikoa iliyokaa kistrategia pia kwa kuwa ni rahisi kupata mashabiki wa nchi jirani nyingi kwa gharama nafuu kiusafiri. Ni rahisi kuifikia Mwanza kwa mashabiki kutoka Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo DRC (upande wa Kaskazini Magharibi na hata baadhi ya maeneo ya Tanganyika Province), Sudani ya Kusini. Kadhalika ni rahisi kwa mashabiki kutoka Zambia, Malawi, Kongo DRC Mashariki, Zimbabwe, Msumbiji, Namibia, Botswana, na hata Afrika Kusini.
😀😀 Yaani mara hapendi Mwanza mara anaipenda na kuipambania! Arusha imesalitiwa tena leo!Huyu jamaa ChoiceVariable haeleweki kama Demu aliyekula Nauli
Hadi Sasa zipo.Tuna timu 2 Ligi kuu na timu 4 championship lakini Serikali ya ccm haioni hilii kuwa ni muhimu.Mbeya kwa kweli wanatakiwa kupewa uwanja mpya maana huko kunakuwaga na timu nyingi za mpira
Nani atautumia Mwanza?Unajenga uwanja Arusha na Dom baada ya Afcon atatumia nani wakati hawana mzuka na mpira?
Sijawahi kuwa chawa na Sina Mpango wa kuwa chawa na Wala silipwi na yeyote.ChoiceVariable Sio chawa ana Akili timamu kbs sema Kuna mda tu plagi hazichomi
Mwanza Ina events nyingi za michezo, population yake tuu ni mtaji tosha.Hata kama sio kujenga basi wafanye Maboresho makubwa ccm kirumba.Nani atautumia Mwanza?
Unadhani miundombinu unayoita Bora huko Arusha ilishushuka na mvua? Ni upendeleo ule ule wa kuchukua pesa zetu kwenda kujenga huko.Arusha ni mji bora na uliondelea kuliko mwanza. na ni mji wenye infrastructures bora kuliko Mwanza na mbeya combined.
Mimi nilitamani iwe Arusha, Dar na Zanzibar. Hiyo mikoa mingine imekaa kushoto.
Toa mfano wa events ambazo Arusha haina.Mwanza Ina events nyingi za michezo, population yake tuu ni mtaji tosha.Hata kama sio kujenga basi wafanye Maboresho makubwa ccm kirumba.
Mna hata timu championship nyie? Kavuteni bangi hukoToa mfano wa events ambazo Arusha haina.
Vitachezea mechi ya ligi kuu ya ndani au FA baada ya Afcon kumalizika.Ukweli ni kuwa hivyo viwanja vitageuka magofu
Game nyingi sana za maana zimechezwa Arusha, na ule mji umeandaa mashindano na events kubwa za kimataifa na watu wake wamekuwa wenyeji wa matukio mengi sana ya kimataifa na mji ule unaweza hata sasa hivi kupokea wageni wengi wa caliber ya juu.Unadhani miundombinu unayoita Bora huko Arusha ilishushuka na mvua? Ni upendeleo ule ule wa kuchukua pesa zetu kwenda kujenga huko.
Kuna siku tutaikomesha hii tabia.By the way baada ya Afcon uwanja utabakia pambo,wavuta bangi na mpira wapi na wapi?
Mwisho Kwa Sasa wanaweza Jenga ila hata wa watu 20,000 Kwa Arusha ingewafaa.
Sisi tunataka viwanja vikubwa vya watu kuanzia 30,000-50,000 maana tuna mashabiki wenye wazimu wa soka na tuma Vijana wenye vipajo vya michezo.Tunahitaji viwanja sio Kwa Ajili ya Afcon Bali michezo.
Umeongea ukweli mkuu.Hii tabia ya kubagua Mikoa ya Mbeya na Mwanza kwenye mambo ya Maendeleo naona imeanza kukita mizizi.
Wakati mikoa mingine ikipendelewa sie Mwanza na Mbeya tumekuwa wahanga wa kutengwa na Kubaguliwa kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo licha ya kuwa tunastahili kwa vigezo na sio kwa kuonewa huruma.
Haiwezekani na haiingii akilini eti kubagua miji hii maarufu kwa wanamichezo na badala yake wakaipendelea miji isiyo na mashabiki wala wanamichezo ya Arusha na Dodoma.
Nasisitiza tunadai haki yetu na sio favour kwa sababu zifuatazo;
Mwanza
- Mikoa wa pili kuchangia Pato la Taifa GDP baada ya Dar.
- Jiji la Pili kuwa na population kubwa baada ya Dar.
- Jiji la 3 Kuchangia Mapato ya Kikodi.
- Uwepo wa mashabiki wa kutosha na wanamichezo.
Mbeya
- Mikoa wa 3 kuchangia Pato la Taifa nyuma ya Dar na Mwanza.
- Jiji la 6 Kwa idadi ya watu Tanzania.
- Jiji la 2 Kwa Wanamichezo wengi kama timu za NBC&Championship.
- Pamoja na mtoto Wetu Songwe ni Mkoa wa 4 Kwa mapato ya Kikodi.
Kwa vigezo hivyo pekee tunastahili kupata kitu sio kwa upendeleo bali kwa haki.
Habari za kusema hakuna hoteli au miundombinu ya kisasa na blaa blaa kama hizo zinatokana na Serikali hii ya ccm kuchukua pesa na jasho letu kwenda kujenga Mikoa mingine kama Arusha, Dodoma, Tanga, Dar nk.
Ni aidha Serikali ianze ujenzi wa viwanja vya Kisasa kwenye miji yetu kutufuta machozi na sio lazima kwa ajili ya AFCON bali kutupa heshima yetu kwenye michezo au tumwage mboga 2025.
Hali hii haivumiliki na haikubaliki, ni wakati wa watu wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini kufanya jambo la kujitambua mwaka 2025 endapo wataziba maskio.
Ni bora kumwaga mboga sio kwa sababu tunawakubali Wapinzani bali ni kwa nia ya kukomoana kwamba tukose wote, tumechoka kutengwa na tabia hii ikiendelea ipo siku tutagawana fito.
View attachment 2766050View attachment 2766051View attachment 2766052
Angalizo: Haya ni maoni na mtizamo binafsi, yasichukuliwe kama uchochezi.