Kubagua Mwanza na Mbeya AFCON haikubaliki

Hii tabia ya kubagua Mikoa ya Mbeya na Mwanza kwenye mambo ya Maendeleo naona imeanza kukita mizizi.

Wakati mikoa mingine ikipendelewa sie Mwanza na Mbeya tumekuwa wahanga wa kutengwa na Kubaguliwa kwenye masuala mbalimbali ya kimaendeleo licha ya kuwa tunastahili kwa vigezo na sio kwa kuonewa huruma.

Haiwezekani na haiingii akilini eti kubagua miji hii maarufu kwa wanamichezo na badala yake wakaipendelea miji isiyo na mashabiki wala wanamichezo ya Arusha na Dodoma.

Nasisitiza tunadai haki yetu na sio favour kwa sababu zifuatazo;

Mwanza
  • Mikoa wa pili kuchangia Pato la Taifa GDP baada ya Dar.
  • Jiji la Pili kuwa na population kubwa baada ya Dar.
  • Jiji la 3 Kuchangia Mapato ya Kikodi.
  • Uwepo wa mashabiki wa kutosha na wanamichezo.

Mbeya
  • Mikoa wa 3 kuchangia Pato la Taifa nyuma ya Dar na Mwanza.
  • Jiji la 6 Kwa idadi ya watu Tanzania.
  • Jiji la 2 Kwa Wanamichezo wengi kama timu za NBC&Championship.
  • Pamoja na mtoto Wetu Songwe ni Mkoa wa 4 Kwa mapato ya Kikodi.
View attachment 2766225
Kwa vigezo hivyo pekee tunastahili kupata kitu sio kwa upendeleo bali kwa haki.

Habari za kusema hakuna hoteli au miundombinu ya kisasa na blaa blaa kama hizo zinatokana na Serikali hii ya ccm kuchukua pesa na jasho letu kwenda kujenga Mikoa mingine kama Arusha, Dodoma, Tanga, Dar nk.

Ni aidha Serikali ianze ujenzi wa viwanja vya Kisasa kwenye miji yetu kutufuta machozi na sio lazima kwa ajili ya AFCON bali kutupa heshima yetu kwenye michezo au tumwage mboga 2025.

Hali hii haivumiliki na haikubaliki, ni wakati wa watu wa Kanda ya Ziwa na Nyanda za Juu Kusini kufanya jambo la kujitambua mwaka 2025 endapo wataziba maskio.

Ni bora kumwaga mboga sio kwa sababu tunawakubali Wapinzani bali ni kwa nia ya kukomoana kwamba tukose wote, tumechoka kutengwa na tabia hii ikiendelea ipo siku tutagawana fito.
View attachment 2766050View attachment 2766051View attachment 2766052

Angalizo: Haya ni maoni na mtizamo binafsi, yasichukuliwe kama uchochezi.Nachokonoa mada Kwa maslahi mapana ya Nchi hii na watu wa Mbeya na Mwanza.
Wanasiasa wa bongo kwenye michezo kazi yao ni kutafuta political mileage tu kwa asilimia kubwa.
Mkuu uko logical hata mimi nashangaa sana katika hili jambo.
 
Mbona kama unakua mnafiki mnafiki,hujui unasimamia nini?

Kwa hio Mwanza wanapojengewa Daraja na Magufuli huo nao tuuite ubinafsi?

Serikali haifanyi jambo kwa kufuata hisia
Acha kua kigeu geu wewe kada wa ccm
 
Tuache siasa. Huko hakuna miundombinu km hotels nk
 
Mwanza kuna hoteli ngapi za kitalii?Mmoja juzi alikuwa analalamika Bureau De Change ipo moja Jiji zima.
Mkuu kwa case ya mtu mmoja unatoa conclusion ya jambo kwenye watu milioni na ushee😯
 
Mbona kama unakua mnafiki mnafiki,hujui unasimamia nini?

Kwa hio Mwanza wanapojengewa Daraja na Magufuli huo nao tuuite ubinafsi?

Serikali haifanyi jambo kwa kufuata hisia
Acha kua kigeu geu wewe kada wa ccm
🗑️🗑️🗑️
 
Ukweli ambao hamtaki kuusema Ni kwamba Arusha Ni focal point ya utalii hapa Afrika Mashariki....kutokupeleka mashindano haya huko Ni kupotrza faida kubwa kwa taifa......Hapa nakuhakikishia ktk maeneo yote Arusha ndio kutakuwa na fan base kubwa sana sababu ya utalii....hata Ile Royal Tour ingekuwa Ni upuuzi mtupu Kama Afcon haotachezwa Arusha
Wanakuja kufanya Utalii au kucheza mpira? Mashabiki hawana mda na manyani
 
Umenena mkuu, katika vigezo vya kuzingatiwa ili uwanja uwe umekidhi vigezo vya michezo ya kimataifa ni pamoja na kuwa na hoteli za kutosha za kitalii karibu na uwanja huo, hili ndio limesababisha Arusha kupewa nafasi
Hotel za huko Arusha zilishuka kama mvua au serikali ndio iliweka mazingira zikajengwa?

Tunataka mazingira hayo hayo yawekwe Mbeya na Mwanza,sisi sio Manamba.
 
Arusha tumekuwa na Tanzanite miaka yote imeendeleza mikoa mingine hatujawahi lalamika,

Mpaka mmeipeleka merarani mkoa wa Manyara tumekaa kimya na bado tunafanya vyema.

Once blessed always blessed.
Mikoa ipi iliyoendekezwa na Tanzanite? Mbeya na Mwanza tunataka stahiki zetu sio hisani,sisi sio Manamba wa kufanyia kazi Arusha,Dar na Dodoma.
 
Arusha ni part ya blue print iliyoipa ushindi bid ya pamoja.

So sahau kama itaachwa at this stage.

Wahusika wameona panafaa.

Wewe kwa hisia tu huwezi badili uhalisia.
Kila Mkoa hapa Tanzania ni blue print kama ukitendewa haki
 
Back
Top Bottom