Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
China hivi karibuni imetangaza kurekebisha Kanuni za Idara za Chama cha Komunisti cha China na Serikali za Kubana Matumizi na Kupinga Ufujaji, na kufafanua kuwa idara za Chama na serikali zinapaswa kubana matumizi, ili kuhakikisha rasilimali nyingi zaidi za umma zinatumiwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya wananchi.
“Uwekevu ni mali yetu ya urithi, na hatupaswi kamwe kuzitupa wakati wowote”. Rais Xi Jinping wa China amesisitiza mara kwa mara umuhimu wa uwekevu. Marekebisho hayo yanazingatia usimamizi wa bajeti ya idara za Chama na serikali, matumizi ya fedha za umma, na hata shughuli za upokeaji wageni.
Kubana matumizi ni desturi nzuri ya Chama cha Kikomunisti cha China. Wakati mageuzi ya ardhi yalipofanywa kabla ya kuanzishwa kwa China mpya, wimbo mmoja ulisema, makada wa eneo la Sovieti wana tabia nzuri ya kikazi, wanachukua chakula chao kikavu wanapotoka nje kufanya kazi, ili wasilete usumbufu kwa watu.
Sasa China imeendelea, lakini desturi hiyo nzuri ya Chama haijapotea. Rais Xi alisema, bila kujali China itapata maendeleo namna gani, desturi ya kufanya kazi kwa bidii na uwekevu haiwezi kupotea kamwe.
Tangu kufanyika kwa Mkutano wa 18 wa Wajumbe Wote wa Chama cha Kikomunisti cha China, matumizi ya fedha za umma yamesimamiwa kwa ufanisi zaidi, na nidhamu mbalimbali zikiwemo maafisa katika ngazi mbalimbali wanaweza kuwa na ofisi na gari ya kiwango gani, kiasi gani cha ruzuku wanapewa wanapokwenda ufanya kazi nje ya maeneo yao.
Idara za Chama na serikali za China kubana matumizi ni kwa ajili ya kuwa na rasilimali nyingi zaidi katika kuendeleza nyanja zinazohusika na maisha ya wananchi.
Kwa mfano, mwaka 2024, zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya taifa ya China ilitumiwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu. Inaaminika kwamba baada ya utekelezaji wa marekebisho ya kina ya Kanuni za Idara za Chama na Serikali za Kubana Matumizi na Kupinga Ufujaji, dhana ya kubana matumizi itapokelewa zaidi na maafisa wa serikali na wanachama wa CPC, na kuhimiza zaidi uhusiano wa karibu kati ya serikali, Chama na wananchi.
Kiini cha serikali na Chama kubana matumizi ni kuimarisha uwajibikaji kwa umma. Inatoa ishara wazi kwamba, kila senti ya fedha za umma hubeba imani ya wananchi, na lazima itumike pale inapopaswa kutumika zaidi.
Wakati upangaji wa makini wa bajeti unapokuwa wa kawaida, serikali na chama tawala vitaaminika zaidi na wananchi. Na hii ndio njia endelevu ya kujiendeleza ya serikali na Chama tawala nchini China.