Kubeba majeruhi kwenye gari za wazi (Pickup) badala ya gari za wagonjwa (ambulance) kwenye tukio la kuanguka ghorofa K/Koo ni sahihi?

Kubeba majeruhi kwenye gari za wazi (Pickup) badala ya gari za wagonjwa (ambulance) kwenye tukio la kuanguka ghorofa K/Koo ni sahihi?

Nadhani wewe ndo huna Ubongo.
Mwenzako kasema Waheshimiwa wamekuja na V8 ina maana hadi wanafika Gari la wagonjwa linashindwaje kufika.

Hivi Kutoka hapo unajua hazifiki hata 3km kutoka Muhimbili au 3 kutoka Aman hospitali.
Hizo gari za wagonjwa zinasubiri nini muda wote huo?

Gari la wagonjwa lenyewe tayari lina First Aid hivyo linaanza toa huduma wakati mgonjwa yuko njiani huwezi fananisha na Gari la kawaida.

Pia Gari la wagonjwa ni jepesi kufika kwa muda kwani halikai foleni lile. alafu wewe unatetea kuwa hujaona tatizo hapo?
Asante kiongozi umenisaidia kupa ngumi za chembe moyo 😄 🤣 😂
 
Majeruhi karibu wote waliokolewa wapatao 40 mpaka sasa kwenye tukio la kuanguka kwa ghorofa mitaa ya Kariakoo jijini Darisalama wamepelekwa hospitali ya Muhimbili wakiwa wamepakiwa kwenye gari za wazi nyuma maarufu kama Pick Up badala ya gari maalum za wagonjwa ambulance

Sasa najiuliza Kariakoo ni karibu kabisa na hospitali ya Amana na Muhimbili na hospitali nyingi tu za binafsi kama Rengency zipo mitaa hiyo kwanini ambulance za hospitali hizo hazikutumika kuja kuchukua majeruhi hao baadala yake wametumia Pickup za polisi na watu binafsi?

Matokeo yake kaja Dkt. Janabi, Mkuu wa Mkoa na Waziri Mkuu na magari ya kifahari aina ya landcruiser V8 ambayo pia hayakutumika kubeba majeruhi hao bali yamepaki yanawasubiri waheshimiwa

Polisi siku zote wanazuia gari za wazi kupakia abiria nyuma kwa sababu za kiusalama pindi ikitokea ajali wataumia sana

Comasava
Nani kama mama.. Maam
 
Linapokuja suala la uokozi wa watu na mali zao katika majanga yoyote yale, kila aina ya mbinu inapaswa kutumiwa kwa Uharaka.

Mfano katika lile janga la ndege kuzama majini kule Mwanza tulimuona ndugu Majaliwa alivyopambana akiwa wenzie na wakaokoa watu

Hata ukienda Nchi zilizoendelea, mbinu hazisubiri vyombo husika,
bali vyovyote vile unavyoweza fanya ilimradi usiongeze kiwngo cha.madhara
 
Majeruhi karibu wote waliokolewa wapatao 40 mpaka sasa kwenye tukio la kuanguka kwa ghorofa mitaa ya Kariakoo jijini Darisalama wamepelekwa hospitali ya Muhimbili wakiwa wamepakiwa kwenye gari za wazi nyuma maarufu kama Pick Up badala ya gari maalum za wagonjwa ambulance

Sasa najiuliza Kariakoo ni karibu kabisa na hospitali ya Amana na Muhimbili na hospitali nyingi tu za binafsi kama Rengency zipo mitaa hiyo kwanini ambulance za hospitali hizo hazikutumika kuja kuchukua majeruhi hao baadala yake wametumia Pickup za polisi na watu binafsi?

Matokeo yake kaja Dkt. Janabi, Mkuu wa Mkoa na Waziri Mkuu na magari ya kifahari aina ya landcruiser V8 ambayo pia hayakutumika kubeba majeruhi hao bali yamepaki yanawasubiri waheshimiwa

Polisi siku zote wanazuia gari za wazi kupakia abiria nyuma kwa sababu za kiusalama pindi ikitokea ajali wataumia sana

Comasava
Kipaumbele chetu ni hiki kwanza
Screenshot_20241116-162911.jpg
 
Unajua kwamba matibabu huanzia ndani ya ambulance?
Kama haipo so wasubiri hadi wafike. Sisi hata mtu akizidiwa home tunamkimbiza hospital wenyewe sio kupiga simu ambulance ije kumfuata bado tunaishi zama za giza. Ambulance kwa tz ni anasa gharama ya kumkimbiza mtu kwa ambulance ukiambiwa unaweza kudhani anapanda yatch luxury.
So, ninashangaa kuona mnashangaa watu kukimbizwa na pickup.
Narudia, la msingi ni wawahishwe hospital wafike wakiwa hai watibiwe mengine hayana maana...
 
Kwahiyo ulitaka wapoteze maisha kisa kusubiria ambulance?!
Ajali imetokea saa 3 asubuhi...zaidi ya masaa mawili hawajaokolewa. Ambulance zingekuwa zimeshafika. Ni sahihi kubebwa na gari yoyote kama ambulance hazipo. Lakini ni vyema tukajiuliza kwanini ambulance hazikuwepo? Ni jambo la kushangaza.
Tukubaliane tu kwamba mwenye suala la uokoaji tupo nyuma sana.
 
Back
Top Bottom