Kubeba majeruhi kwenye gari za wazi (Pickup) badala ya gari za wagonjwa (ambulance) kwenye tukio la kuanguka ghorofa K/Koo ni sahihi?

Hua nasoma mijadala na comments kwenye mitandao kama linkedline yaan had mtu unafurahia watu wanavyo jikita kwenye maada tu tena kwa kirefu.

Hata hapa jf ni hivyo kwa baadhi ya wachangiaji wachache. Ila wengi humu ni watu wasio penda kabisa kufikiri kabla ya kutenda. Wanachangia utazani ni lazima wachangie ili waendelee kubaki jf.

Vifaa vya uokozi vinahusisha mitambo kama greda za aina mbali mbali, winchi, magari ya zima moto, magari ya wagonjwa pamoja na watu wenye utaalamu unaohusiana na janga husika.

Mleta maada yeye kauliza kutokuwepo kwa ambulances, lakini ukisoma nyuzi zingine kuna watu wamehoji juu ya uhaba wa vifaa vya uokozi. Kwahiyo kwaujumla timu ya uokoaji haitoshi na haijitoshelezi ki vifaa hadi kuna memba kwenye uzi mmoja humu kapendekeza raia wapange mistari mirefu wakiwa na ndoo wajaze vifusi kwenye maroli!!!

Eneo lililo katikati ya jiji kama kariakoo kukosa vifaa vya uokoaji ni aibu!! Ilitakiwa soko kama soko tu, wawe hata na ambulance 10 za soko tu! Wawe na magari ya kuzima moto hata mawili, lile ni moja ya masoko makubwa Afrika mashariki lazima lijiweke tayari kujisaidia kabla halijasaidiwa.

Kama kkoo wahanga wanakosa ambulance jiulize wewe hapo ukipata shida kwako unaweza kuipata ambulance kweli?? Hapa ilitakiwa watz tuungane tupige kelele moja na si kutofautiana namna hii.

Muda mwingine ni bora kukaa kimya ili watu wawe wanahisi hisi tu kua huenda wewe ni mjinga, kuliko kuongea ongea hovyo hata usiyo yajua maana hapo utakua una wathibitishia watu kua wewe NI MJINGA KABISA
 
Miaka 60 ya uhuru umri wa mtu mzima aliyestaafu kazi sema nchi ni masikini lakini sio changa
Hicho ni kizazi kimoja tu. USA ina 248. Na tatizo sio nchi kuwa changa tu wala umasikini. Bali lack of experience with disastrous problems. Wenzetu Asia wanaodeal na Matetemeko, Maporomoko, Volcanos, Vimbunga na ma-Tsunamies kila siku. Hili ni tatizo la la masaa 5 pekee.
 
Aisee! Una IQ pengine isiyofika hata 0+
Sio kwa fikra hizi.
Wewe ndiye mwenye IQ ndogo unaijua tanzania ilivyo, hata mtu akizidiwa home tunamkimbiza wenyewe hospitali kwa magari binafsi, bajaji na bodaboda, sasa leo ujifanye emergence watu kibao wanahitajikufika hospital eti ndo usubiri ambulance.... utaendelea kusubiri sana na IQ yako kubwa.
 

Mkuu,
Utamaliza nguvu zako kubishana na Vichaa.
 


Si-mleta Uzi, Si-mimi, wala yeyote mwingine anaekupinga aliesema kuwa wagonjwa wasipelekwe kwa Gari zilizopo.

UELEWE KWANZA HOJA, SIO KUKURUPUKA.

Watu walalama,wanahoji na kudadisi kutokuwepo kwa GARI MAALUM ZA WAGONJWA kuifanya shughuli hiyo ikitiliwa maanani kuwa hapa ni Dar na zama hizi.

Usipoelewa hapo, naagiza ukamatwe uwekwe ndani ya Tanker la mafuta Breki ya kwanza MILEMBE.
 
Wala mimi sijapinga kuwa haiko sawa, nilichosema sasa hivi kinachojalisha ni hao wafike hospitali salama iwe kwa guta au meli ili mradi wafike hospital wapate matibabu. Hayo mengine kwa sasa hayana maana.... Uelewa wako mdogo zaidi ndio maana hukuelewa hata nilichosema.
 
Kwahiyo ulitaka wapoteze maisha kisa kusubiria ambulance?!
Mkuu wa mkoa na Dr Janabi na waziri mkuu wamefikaje Kariakoo na V8 kwa nini Ambulance isifike kwa wakati pumbavu
 
Letaa yakoo
 
Kunatokea ajalinmwenge unasubiri ambulance kweli???
 
Kunatokea ajalinmwenge unasubiri ambulance kweli???
Sasa hii haikutokea Mwenge imetokea Kariakoo kwenye ukaribu wa hospitali kubwa na nyingi kwa nini zisifike kuchukua majeruhi kutokana na umuhimu wake kuna first aid humo?
 
Asante mkuu kwa kuliona hilo hata miye huwa nawashangaa watu wengine baadala ya kujenga hoja kwenye mambo nyeti kama haya ili Serikali ijifunze kitu wanajenga vioja pwagu na pwaguzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…