Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Kubenea wa MWANAHALISI amenunuliwa na mafisadi?

Sasa inakuwaje kubenea anakaa kimya hadi asemewe? Hajui kuwa uongo ukirudiwarudiwa hugeuka ukweli?
Kubenea yupo nje ya nchi, na huyo niliyeongea naye ana legal authority ya kuisemea kampuni au ulimtaka Kubenea mwenyewe kama wafanyavyo akina Zitto. Wewe unachotakiwa kuona je kilichoandikwa ni uongo au ukweli? Tafuta logic then draw your own conclusion.
 
Tangu mwanzo mimi nilisema hili ni uwongo. Hamkunielewa. Haya unaona Bw. Aboud amekuja kuliweka wazi. Tena nawaambia mtambo wa Kubenea upo pale IPP nendeni mkauone. Yule bwana kiboko. Kama ingekuwa Kubenea kanunuliwa asingekuwa na urafiki na Mengi wala Mengi asingeweza kumuuzia mtambo. Haya uwongo una mwisho
Ni kweli kabisa, ningefurahi sana yule aliyeleta thread angecomment naye. Hizi ni zama za uwazi na ukweli.
 
Kubenea hana tamaa ya pesa, bali tamaa ya kupata uhuru wa kweli wa fikra, kwanza anakumbuka vizuri alivyomwagiwa tindikali na hao hao mafisadi kwa kusanua noma zao. nilijua ni uongo ndiyo maana sikuchangia ule upuuzi!
 
Kubenea hana tamaa ya pesa, bali tamaa ya kupata uhuru wa kweli wa fikra, kwanza anakumbuka vizuri alivyomwagiwa tindikali na hao hao mafisadi kwa kusanua noma zao. nilijua ni uongo ndiyo maana sikuchangia ule upuuzi!
Ni kweli mkuu, pamoja na kumtishia kumuua halafu leo 20ml imununue ni jambo lisiloingia akilini.
 
quote_icon.png
Originally Posted by Mu-sir
Thanks tulijua tumepoteza ma fighter.

hoja inaweza kuwa nzuri ila hiyo picha japo kuna ubunifu kidogo inakuaibisha.utaonekana limbukeni na muhuni.


tatizo unaangalia kwa macho ya kengeza, hebu iangalie vizuri hiyo avatar kama ina shida. tatizo umeshayapeleka mawazo yako mafupi ukadhani na makalio ya mwanamke. hiyo ni kifua cha mwanaume
 
:target::target::target::target:
images



SI RAHISI KUBENEA KUNUNULIWA KATOKA MBALI
NA VITA HIVYO ALIPO NI USHINDI TOSHA

images


images


images


WALISHINDWA HAPA SASA HAWATAWEZA DAIMA
images


KAZA BUTI KUBENE
 
Whats a shame@! Kubenea anahongeka kwa mil 20 tu!
Hata angehongwa million ngapi haina tija kulingana na kazi aliyofanya ni itakuwa ni bure tu. Heshima na pesa ni vitu viwili tofauti, Lowassa ana pesa lakini hana heshima hana mbele ya jamii, umeiona hiyo mkuu?
 
Kwahiyo kama 6 na Mwakwembe walitaka kuanzisha CCJ hiyo kweli si habari tunayotakiwa kuipata kama watanzania? Wewe mtoa mada fikiria tena. Mapenzi yako kwa wapambanaji na Chuki yako kwa mafisadi isikufanye kuwa kipofu!

Hata kama ni wapambanaji inatakiwa ijulikane kuwa wao ndiyo waliokuwa waanzilishi wa CCJ, kwani tatizo ni nini? Labda nitasikitika kama itakutikana Kubenea anawasingizia katika habari hii...!
 
aliyeleta thread arudi uwanjani ajib hoja sio kukaa kimya ametumwa na akina RACHEL
 
hahahaha...yule yule katumwa na hapa hapati mtu....kubenea hawez labda akatwe kicha na cyo tindikali kama walivyofanya wao
 
Sitta, Mwakyembe wametajwa sana kwa sababu wao ni waanzilishi wa CCJ. Rostam, Chenge, Lowassa hiyo haikuwa issue yao. Yao ni ufisadi tu!

...Kwa hiyo katika wakati huu tulio nao issue ya kutaka kuanzisha Chama ya akina Mwakyembe na Sitta ni muhimu zaidi inayostahili ukurasa mzima kuliko issue ya Ufisadi ya Rachel? Really? Kabisa umekaa hapo unaamini unachokiandika??

 
Kubenea yupo nje ya nchi, na huyo niliyeongea naye ana legal authority ya kuisemea kampuni au ulimtaka Kubenea mwenyewe kama wafanyavyo akina Zitto. Wewe unachotakiwa kuona je kilichoandikwa ni uongo au ukweli? Tafuta logic then draw your own conclusion.

...So kwa sababu Bwana Legal Authority wa Mwanahalisi amesema kuwa kitu kama hicho si kweli baada ya kumsomea thread nzima ya shutuma hizi (You seem to have plenty of Time and Airtime, Brother!) kama ulivyosema basi ni lazima wote mara moja tuamini kwamba shutuma hizi si kweli?
Ulitegemea ukimpigia Bwana Legal Authority akuambie "Ndio, tuhuma hizo ni za kweli na tumemenuliwa mtambo wa kuchapia magazeti ila sio kwa shilingi Milioni 20 kama inavyodaiwa bali ni kwa shilingi Milioni 200"! I am just thinking aloud. I am a big fan of Kubenea myself but knowing that almost everyone in the World has a Price, I am keeping my mind open...! Will advice others to do so simply because Lisemwalo Lipo na kama halipo basi Linakuja.
 
Nimejaribu kufanya utafiti pori. Mbele yangu nina faili zima la magazeti ya MwanaHALISI. Toleo la mwisho ambalo gazeti hili liliandika habari ya kumbamiza Lowassa ni tarehe 6 Aprili kwa kichwa cha habari: "Lowassa hasafishiki."

Baada ya hapo, matoleo yote 6 yaliyofuata ya MwanaHALISI yamekuwa na habari za kuwatetea kiaina kina RACHEL, kumwandama Kikwete na kujaribu kumgombanisha Kikwete na Sekretariati ya CCM.

Angalia kama ifuatavyo matoleo haya mfululizo ya MwanaHALISI:

1. Kikwete 'jino kwa jino' na Lowassa (13 Aprili)

Habari hii ilipotoshwa makusudi kujaribu kuonesha kuwa uamuzi wa NEC wa kuwafuta kazi mafisadi ndani ya CCM ni vita kali vya madaraka kati ya Kikwete na Lowassa na si uamuzi rasmi wa CCM kama chama.

2. Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete (20 Aprili 2011)

Habari hii iliyokuja immediately baada ya kikao cha NEC ya CCM imesema kuwa Slaa amtaja tena Kikwete katika ufisadi. Ikaongeza kuwa avuruga mkakati wa "gamba." Habari nyingine kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ikasema kuwa: Lowassa, Rostam, Chenge bado

3. Mukama amdanganya Kikwete (27 Aprili 2011)

Habari hii ikitaka kuonesha kuwa Sekretariati ya CCM mpya iliyochukua nafasi baada ya kufukuzwa kwa mafisadi haifai.

4. Kikwete mahakamani (4 Mei 2011)

Huku habari nyingine ikisema CCM yafyata kwa mafisadi

5. Nyumba ya Kikwete yazua utata (11 Mei 2011)

Gazeti hili likiwa linaendelea kumwandama Kikwete kwa tuhuma huku likikaa kimya kuhusu kina RACHEL.

6. Kikwete ndani ya CCJ (18 Mei 2011)

Huu ni muendelezo ule ule wa mkakati wa kina RACHEL wa kuibua tuhuma dhidi ya Kikwete kupitia MwanaHALISI ili wao waweze kusalimika.

Naomba kuwasilisha...

we ulitaka waandike nini?
 
inawezekana kabisa wadau,hii ndo tz bana kila m2 anaangalia usawa wake tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kulikuwa na tetesi kwamba hata wewe umenunuliwa na Ridhiwani na baba yake mzazi kwamba uje hapa jamii forum kuhakikisha unawatetea kwa namna yeyote uwezayo lakini mimi nilipuuzia hii tetesi, lakini sasa naanza kuhisi hizi tetesi si za kuzipuuza.
teh teh hii ndo jf bwana du
 
Hata mimi ni msomaji wa muda mrefu wa MwanaHalisi, Kiukweli hawa jamaa wamebadilika sana, tetesi hizi zinaweza kua na ukweli ndani yake. Kwasiku za karibuni wamekua wakiwateta watuhumiwa wa ufisadi ndani ya magamba! zile title kali kali za mbele hazipo tena, toleo la leo kuna makala inasema " Ni JK anayetesa taifa, si urais 2015" ukiisoma kwa makini utakuta utetezi wa wanaotaka uraisi na kumpoda JK. Jambo jingine ni jinsi ghafla walivyowageuka akina Sitta na wapambanaji wenzake, Mtakumbuka kua hawa jamaa ndio waliokua wanaongelea issue za Richmond na Dowans kwa undani zaidi, na kuwaendorse akina six! Najipa wiki mbili zaidi za kulichunguza nikiona ni kweli nalipotezea kama nilivyoyapotezea mengine!
 
Back
Top Bottom