Nimejaribu kufanya utafiti pori. Mbele yangu nina faili zima la magazeti ya MwanaHALISI. Toleo la mwisho ambalo gazeti hili liliandika habari ya kumbamiza Lowassa ni tarehe 6 Aprili kwa kichwa cha habari: "Lowassa hasafishiki."
Baada ya hapo, matoleo yote 6 yaliyofuata ya MwanaHALISI yamekuwa na habari za kuwatetea kiaina kina RACHEL, kumwandama Kikwete na kujaribu kumgombanisha Kikwete na Sekretariati ya CCM.
Angalia kama ifuatavyo matoleo haya mfululizo ya MwanaHALISI:
1. Kikwete 'jino kwa jino' na Lowassa (13 Aprili)
Habari hii ilipotoshwa makusudi kujaribu kuonesha kuwa uamuzi wa NEC wa kuwafuta kazi mafisadi ndani ya CCM ni vita kali vya madaraka kati ya Kikwete na Lowassa na si uamuzi rasmi wa CCM kama chama.
2. Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete (20 Aprili 2011)
Habari hii iliyokuja immediately baada ya kikao cha NEC ya CCM imesema kuwa Slaa amtaja tena Kikwete katika ufisadi. Ikaongeza kuwa avuruga mkakati wa "gamba." Habari nyingine kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ikasema kuwa: Lowassa, Rostam, Chenge bado
3. Mukama amdanganya Kikwete (27 Aprili 2011)
Habari hii ikitaka kuonesha kuwa Sekretariati ya CCM mpya iliyochukua nafasi baada ya kufukuzwa kwa mafisadi haifai.
4. Kikwete mahakamani (4 Mei 2011)
Huku habari nyingine ikisema CCM yafyata kwa mafisadi
5. Nyumba ya Kikwete yazua utata (11 Mei 2011)
Gazeti hili likiwa linaendelea kumwandama Kikwete kwa tuhuma huku likikaa kimya kuhusu kina RACHEL.
6. Kikwete ndani ya CCJ (18 Mei 2011)
Huu ni muendelezo ule ule wa mkakati wa kina RACHEL wa kuibua tuhuma dhidi ya Kikwete kupitia MwanaHALISI ili wao waweze kusalimika.
Naomba kuwasilisha...