Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,169
- 3,351
Kubenea yupo nje ya nchi, na huyo niliyeongea naye ana legal authority ya kuisemea kampuni au ulimtaka Kubenea mwenyewe kama wafanyavyo akina Zitto. Wewe unachotakiwa kuona je kilichoandikwa ni uongo au ukweli? Tafuta logic then draw your own conclusion.Sasa inakuwaje kubenea anakaa kimya hadi asemewe? Hajui kuwa uongo ukirudiwarudiwa hugeuka ukweli?
Ni kweli kabisa, ningefurahi sana yule aliyeleta thread angecomment naye. Hizi ni zama za uwazi na ukweli.Tangu mwanzo mimi nilisema hili ni uwongo. Hamkunielewa. Haya unaona Bw. Aboud amekuja kuliweka wazi. Tena nawaambia mtambo wa Kubenea upo pale IPP nendeni mkauone. Yule bwana kiboko. Kama ingekuwa Kubenea kanunuliwa asingekuwa na urafiki na Mengi wala Mengi asingeweza kumuuzia mtambo. Haya uwongo una mwisho
Ni kweli mkuu, pamoja na kumtishia kumuua halafu leo 20ml imununue ni jambo lisiloingia akilini.Kubenea hana tamaa ya pesa, bali tamaa ya kupata uhuru wa kweli wa fikra, kwanza anakumbuka vizuri alivyomwagiwa tindikali na hao hao mafisadi kwa kusanua noma zao. nilijua ni uongo ndiyo maana sikuchangia ule upuuzi!
hoja inaweza kuwa nzuri ila hiyo picha japo kuna ubunifu kidogo inakuaibisha.utaonekana limbukeni na muhuni.Thanks tulijua tumepoteza ma fighter.
hoja inaweza kuwa nzuri ila hiyo picha japo kuna ubunifu kidogo inakuaibisha.utaonekana limbukeni na muhuni.
Hata angehongwa million ngapi haina tija kulingana na kazi aliyofanya ni itakuwa ni bure tu. Heshima na pesa ni vitu viwili tofauti, Lowassa ana pesa lakini hana heshima hana mbele ya jamii, umeiona hiyo mkuu?Whats a shame@! Kubenea anahongeka kwa mil 20 tu!
Sitta, Mwakyembe wametajwa sana kwa sababu wao ni waanzilishi wa CCJ. Rostam, Chenge, Lowassa hiyo haikuwa issue yao. Yao ni ufisadi tu!
Kubenea yupo nje ya nchi, na huyo niliyeongea naye ana legal authority ya kuisemea kampuni au ulimtaka Kubenea mwenyewe kama wafanyavyo akina Zitto. Wewe unachotakiwa kuona je kilichoandikwa ni uongo au ukweli? Tafuta logic then draw your own conclusion.
Nimejaribu kufanya utafiti pori. Mbele yangu nina faili zima la magazeti ya MwanaHALISI. Toleo la mwisho ambalo gazeti hili liliandika habari ya kumbamiza Lowassa ni tarehe 6 Aprili kwa kichwa cha habari: "Lowassa hasafishiki."
Baada ya hapo, matoleo yote 6 yaliyofuata ya MwanaHALISI yamekuwa na habari za kuwatetea kiaina kina RACHEL, kumwandama Kikwete na kujaribu kumgombanisha Kikwete na Sekretariati ya CCM.
Angalia kama ifuatavyo matoleo haya mfululizo ya MwanaHALISI:
1. Kikwete 'jino kwa jino' na Lowassa (13 Aprili)
Habari hii ilipotoshwa makusudi kujaribu kuonesha kuwa uamuzi wa NEC wa kuwafuta kazi mafisadi ndani ya CCM ni vita kali vya madaraka kati ya Kikwete na Lowassa na si uamuzi rasmi wa CCM kama chama.
2. Dk. Slaa amweka pabaya Kikwete (20 Aprili 2011)
Habari hii iliyokuja immediately baada ya kikao cha NEC ya CCM imesema kuwa Slaa amtaja tena Kikwete katika ufisadi. Ikaongeza kuwa avuruga mkakati wa "gamba." Habari nyingine kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hilo ikasema kuwa: Lowassa, Rostam, Chenge bado
3. Mukama amdanganya Kikwete (27 Aprili 2011)
Habari hii ikitaka kuonesha kuwa Sekretariati ya CCM mpya iliyochukua nafasi baada ya kufukuzwa kwa mafisadi haifai.
4. Kikwete mahakamani (4 Mei 2011)
Huku habari nyingine ikisema CCM yafyata kwa mafisadi
5. Nyumba ya Kikwete yazua utata (11 Mei 2011)
Gazeti hili likiwa linaendelea kumwandama Kikwete kwa tuhuma huku likikaa kimya kuhusu kina RACHEL.
6. Kikwete ndani ya CCJ (18 Mei 2011)
Huu ni muendelezo ule ule wa mkakati wa kina RACHEL wa kuibua tuhuma dhidi ya Kikwete kupitia MwanaHALISI ili wao waweze kusalimika.
Naomba kuwasilisha...
teh teh hii ndo jf bwana duKulikuwa na tetesi kwamba hata wewe umenunuliwa na Ridhiwani na baba yake mzazi kwamba uje hapa jamii forum kuhakikisha unawatetea kwa namna yeyote uwezayo lakini mimi nilipuuzia hii tetesi, lakini sasa naanza kuhisi hizi tetesi si za kuzipuuza.