Kubeti sio kamari, kamari ni kama vile Tatu Mzuka (sio betting)

Kubeti sio kamari, kamari ni kama vile Tatu Mzuka (sio betting)

Vichekesho

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
66
Reaction score
3,277
1. Mkulima anayekwenda shambani kulima akitegemea mvua ambayo haiko ndani ya uwezo wake anabeti.
2. Mfanya biashara anayenunua maparachichi na nyanya kwa mkulima akitegemea kuuza kwa mteja ambaye hamjui anabeti.

3. Serikali inapopitisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha na kupanga matumizi ya fedha ambazo hawajui kama zitapatikana au la inabeti.

4. Mimi ninaposema timu ya Yanga itaifumua timu ya Simba nabeti.

5. Suala la ndoa ni kubeti.

6. Kununua hisa za makampuni na kufanya uwekezaji wowote ule ni kubeti.
.........................
Kamari ni ile wewe unaweka 1000 unategemea kupata mamilioni bila kujua kompyuta inatumia hesabu gani ili kuchagua mshindi. Na kwakuwa hujui basi huna uwezo wa kudai ushindi.

Kwenye betting timu uliyosema kuwa unadhani itashida ikishinda kweli na usipopewa chako unaweza kudai na utalipwa maana kanuni ya kupata mshindi inajulikana.

NB: Nina mpango wa kufungua chama cha kubeti Tanzania (CCKT) na kitatoa fursa za vijana kushirikiana kutoa odds zakibabe na kushiriki kwenye mikutano mbalimbali ya wawekezaji kwenye sekta ya betting ambao pia ni walipakodi walio nyooka.
 
Uko sahihi. Unapo-bet fedha kwa kutumia mashine unaweza kufanyiwa udanganyifu kwani matokeo yake halisi huwezi kuya-confirm kuwa hayakufanyiwa udanganyifu.
 
Every Punter (anayecheza na sio kuchezesha) anabet (Na sio betting pekee bali ni kwamba anamtajirisha mchezeshaji) In the end THE HOUSE ALWAYS WINS..., Kwanini ? Sababu the Odds are on their Favor..., hence you can not consistently overcome this mathematical fact....
 
Kubeti ni kamari, ina sifa zote za kamari na sifa chache mno za biashara.

Kwenye biashara kuna nahitaji fedha nina maharage, anayehitaji maharage ana fedha.

Kamari ni nahitaji fedha nina fedha nani yupo tayari kupoteza fedha yake ili niichukue au yeye achukue ya kwangu? Halafu kunatafutwa jambo la kushindana kunyang'anya fedha. Hiyo ni kamari, hakuna kubadilishana bidhaa kuna kunyang'anyana fedha.

Biashara ina sifa ya win-win, si lazima mmoja akose ili mwingine apate, wote mnaweza kupata ila si kamari, kamari haina win-win lazima mmoja aumie ili mwingine apate.
 
Kuuza na kununua fedha (forex) ni kamari? Kununua hisa ni kamari?
Hapana. Si kamari. Ukinunua hisa husubiri yoyote apoteze ili upate fedha, unasubiri watakaohitaji hisa ulizonazo wawe wengi ili uziuze kwa bei kubwa. Hakuna kunyang'anyana fedha kwenye hisa.

Forex inategemeana. Hizi za kimshale ni kamari, ila ukinunua fedha za kigeni ukasubiri zipande thamani kisha ukaziuza hiyo si kamari.

In short jambo lolote ambalo haliitaji kuweka fedha, halafu wengine waweke fedha kisha mzigombanie ndani ya muda fulani si kamari.
 
Ukikosa unakuwa umepoteza pesa ulizotumia kuprocess maombi,
Hapana, litazame hili suala kwa akili kidogo mkuu, mbona ipo wazi.

Gharama za kuprocess maombi ya tenda unaweza zifananisha na gharama za kulipia transaction fee ya kuweka pesa ya kubeti.

Mfano, ili ubeti 1000, si ni lazima uweke pesa kwenye akaunt ya kubet? Ile gharama ya kuweka pesa kwenye akaunt ya kubet ndo unaweza ilinganisha na gharama ya kuombea tenda na haihusiani na mtaji wa kubet kama ambavyo application fee ya tenda haihusiani na mtaji wa kuihudumia hiyo tenda.

Sasa ukishaomba kubet kwa kulipia gharama za kuweka fedha ya kubet, ukabet ukaliwa inamaana pesa yako yote kaichukua aliyepata au kaichukua mwenye kampuni. Umepoteza fee za kuweka pesa ya kubeti na umepoteza mtaji. Lose-Lose.

Kwenye tenda, ukiomba ukakosa mtaji wako haujachukuliwa na yoyote japo umepoteza app fee.

ukiomba VISA pia unalipia gharama ubalozini, unaandaa documents na unanyimwa hiyo pia ni kamari?
Hapana, ukiomba VISA ukanyimwa hujapoteza pesa ambayo ungeitumia kusafiri, umepoteza pesa ya maombi tu.
ukibet ukaliwa umepoteza vyote, transaction fee na umepoteza fedha uliyobetia.

Kwanini unafananisha fees and capital? Kwani mfano ukienda sokoni kununua nyanya ukakosa nyanya unapoteza pesa ya kununulia nyanya au umepoteza nauli yako?
Ukituma maombi chuoni unasifa zote, na unakosa simply because nafasi zimejaa na hurudishiwi application fee je hii pia ni kamari?
NO NO NO. ingekuwa hayo maombi unatuma na ada yote kisha ukikosa ada imeliwa ndo ingekuwa kamari.

KAMARI NI KAMARI SABABU UKIPOTEZA UNAPOTEZA VYOTE ILI MWINGINE APATE.

YAANI UMETOKA HAPA KWENDA KUFANYA BETTING, UMEWEKA ELFU MBILI KWENYE SIMU, UKAKATWA HAMSINI KAMA TOZO ZA MHAMALA HALAFU UKABETI 1950 IKILIWA UMEPOTEZA 2000.

UMETOKA HAPA UNAENDA KUOMBA CHUO, GHARAMA ZA KUOMBA CHUO NI ELFU MOJA, ADA NI ELFU HAMSINI, UMEKOSA CHUO UMEPOTEZA ELFU MOJA.
 
Una kichwa kigumu sana, kwa taarifa yako watu hukosa visa na kujikuta wamepata hasara kubwa kupita kiasi achilia mbali fedha za dockment, je nao wamebeti?
KUDADADEKI KAMA UNALINGANISHA GHARAMA ZA KUTUMA MAOMBI NA KUBETI BADALA YA GHARAMA ZA KUTUMA MAOMBI NA GHARAMA ZA MIAMALA ILI UBETI WE JIAMBIE LILE UNALOONA LINAKUPA AMANI YA KUBETI.
 
Hata mkulima anayelima kuna muda hukumbwa na ukame, mafuriko, magonjwa nk na kunamuda hupata neema. Kilimo kinahitaji timing, betting inahitaji timing pia.
Ukame, Mafuriko na magonjwa ni predictable na ukifuata ratiba nine out of ten times utanufaika (huwezi kupanda Bangi ukavuna mchicha)..., pili kama wewe unalima vitunguu mwaka huu kwa kutegemea bei za mwaka jana wala hauna masoko ya uhakika hapo utakuwa unacheza kamari....

Tukija kwenye betting; Bookies (Mchezeshaji) ana guarantee ya kula pesa ya (punter) anayecheza sababu odds zinamlinda na game haipo fair kwa anayecheza (na kila ukipata mathematical loophole bookies wataifunga)...

Kwahio tuseme Barcelona kwa msimu huwa anashinda mechi tisa kwenye kila mechi kumi; kwa haki ingebidi bookies akupe hata odds za 0.1 kwahio ukicheza mara kumi angalau upate faida ya 10 tshs au ukishinda kumi ukapoteza ya kumi na moja angalau utakuwa ume break even..., ila kinachotokea utapewa odds za 0.09 hence mwisho wa siku pesa unazoshinda leo kesho utazirudisha...
 
Kubeti ni kamari, ina sifa zote za kamari na sifa chache mno za biashara.

Kwenye biashara kuna nahitaji fedha nina maharage, anayehitaji maharage ana fedha.

Kamari ni nahitaji fedha nina fedha nani yupo tayari kupoteza fedha yake ili niichukue au yeye achukue ya kwangu? Halafu kunatafutwa jambo la kushindana kunyang'anya fedha. Hiyo ni kamari, hakuna kubadilishana bidhaa kuna kunyang'anyana fedha.

Biashara ina sifa ya win-win, si lazima mmoja akose ili mwingine apate, wote mnaweza kupata ila si kamari, kamari haina win-win lazima mmoja aumie ili mwingine apate.
Kwenye betting kuna cash out pia
 
Back
Top Bottom