Kubeti sio kamari, kamari ni kama vile Tatu Mzuka (sio betting)

Mungu anabariki kazi ya mikono
Pia tumeambiwa tutakula kwa jasho
So it betting inafit hapo it's okay
Ila kiukweli siamini niliumbiwa kula kwa jasho za wenzangu
 
ZIkishuka si umepoteza... Unaweza kununua fedha fulani ukaihold ukitegemea ipande na isipande bali ishuke thamani.
 
Kumbe hata kugombea au kushiriki uchaguzi, ni ku-bet.
 
Comments reserved
 
ZIkishuka si umepoteza... Unaweza kununua fedha fulani ukaihold ukitegemea ipande na isipande bali ishuke thamani.
Hata viatu, unaweza vinunua ukitegemea utauza lakini usiuze. Ni biashara. Biashara inaongozwa na misingi ya demand and Supply. Betting si biashara, haiongozwi na misingi ya demand and supply.

HALAFU, UNAPOAMUA KUFANYA JAMBO NJE YA MISINGI YA IMANI(MAANA NAJUA WENGI HAPA NI IMANI ZA DINI KUKATAZA KAMARI NDO INALETA SHIDA) WEWE FANYA UTATUBU.

KUNA MAFISADI, KUNA WEZI, KUNA WAZINZI,WABAKAJI. MTU KUCHEZA KAMARI UNATESEEEEEEKA KUTAFUTA UHALALI. BETTING NI KAMARI.
 
Sasa hapo pa kuassume demand itakuwa kubwa uuze ni kubet
 
Mimi si bet mkuu. Ila vitu vingi ni gambling sema tu vinazidiana risk.
Gambling kwenye mambo ya kidini imekatazwa kwa sababu ya element ya ili wewe upate, lazima yule apoteze. Ili wewe ulie, lazima yule acheke hakuna mazingira ambayo wote mnaweza kucheka.

Binafsi sioni tatizo mtu kucheza betting as long as haimfanyi akapata uraibu. Ila uhalisia ni kuwa betting ni kamari.
 
Naunga mkono hoja
 
Basi hata kuishi ni kubet maana hatujui kesho
 
Basi hata kuishi ni kubet maana hatujui kesho
Hahaha. Kuishi si kamari mkuu. Kubeti lazima mwingine apoteze ili wewe upate, sasa wewe ukiishi kuna mwenzako unayekufa sababu wewe umeishi?

Yaani kamari ni kamari, kuitafutia isiwe kamari kwa kulazimisha ifanane kwa 100% na kitu kingine ni kujiambia unachotaka kusikia tu....

Betting inaweza kuwa na tupasent twa biashara ndani yake lakini pasenti kubwa inaangukia kwenye mchezo wa kamari na kuhitimisha huo mchezo kuwa kamari.
 
Unaonaje ukinunua mchele shambani 2500 na mteja wako umuuzie 2500 maana ukizidisha utakua umetenda dhambi maana wewe ulinunua 2500 na hiyo si ni kamari maana ukizidisha unachukia hela ya mtu
 
ZIkishuka si umepoteza... Unaweza kununua fedha fulani ukaihold ukitegemea ipande na isipande bali ishuke thamani.
Kwenye kununua Hapa unazungumzia biashara ambayo inakua na kutoa / kupokea huduma au/na bidhaa Kwa fedha

Sasa mkuu tusaidie kwenye betting unapokea huduma au bidhaa Gani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…