Kubezwa kwangu kulinipunguzia presha nikawa mshindi vipindi vyote

Kubezwa kwangu kulinipunguzia presha nikawa mshindi vipindi vyote

Ni yule #DeMostAdmired Wa Mercy.

Nimependa pia nishee experience hii na ninyi ndugu zangu wa JF. Nahisi tutapata vitu flani flani.

Nashea hii kujaribu kuwapa shuhuda juu ya nature ya jinsi gani sisi walimwengu tulivo na maajabu ya ulimwengu wenyewe

Nianze na kuwapa update kuhusu Mercy, Mercy yupo anaendelea vizuri na mtoto wake huko kwao ila habari za Dokta sizifahamu.

Nianzie mwaka 2006 ndo nilianza darasa la kwanza, mimi sikuanzia vidudu kwa mujibu wa wazazi na watu wenye kumbukumbu nzuri zaidi yangu ni kwamba sikusoma vidudu kwasababu nilikuwa nilipelekwa darasani chekechea basi nilikuwa napigana sana na vitoto vyenzangu na nilikuwa sikai darasani ila nilikuwa natoka namfata bro darasa la kwanza.

Mimi pia niko na baadhi ya kumbukumbu juu ya miaka hii ya 2006 kwahyo nachokieleza kinatokana na stors kutoka kwa walionishuhudia na baadhi kutoka kwangu binafsi.

Kwanzia darasa la kwanza kulikuwa na watu wachache sana ambao waliweza kunielewa. Baba yangu alikuwa mwalimu lakini ni miongoni mwa watu wengi walokuwa hawaniamini katika mambo mengi hasa swala la elimu. Waliamini mimi ni mtu wa kawaida sana na wengine walithubutu kunidhihaki na hao ndo wamenisukuma kuandika Uzi huu leo.

Nitaruka mpaka darasa la 7. To be honest nilianza na primary sikuwahi kuwa namba moja skul toka la1 mpka la7 ila nakumbuka darasa la2 ndo nilikuwa wa2.

Bro wangu yeye ndo alikuwa anatuongozea class, yeye alipenda kusoma na kujishughulisha na masomo.

Matokeo yangu yalikuwa hayatabiriki lakini sikuwahi kufeli, yani ukichora graph ya matokeo against madarasa au vidato nature ya graph utakayoipata itakuwa ni irregular sana yani itakuwa zigzag mno.

Darasa la saba wakati wa mtihan baba aliniita ilikuwa ni jpil ambayo j3 ndo paper. Alivoniita akanambia kwamba kuna msimamizi x nimemuomba akusaidie pale ambapo utaona huwez basi ugonge dawat umuite ujifanye kama kuna mahali pamekosewa au hupaelew basi yeye atakusaidia kukupa majibu ili ufaulu mwanangu sitaki ufeli.

Nilimuliza bro kama nayeye kapewa yale maelekezo akasema hapana, kwahyo nikaona kabisa hapa tayr baba kashaniona mimi sijiwezi.

Nimeweka wazi hii so kwa ubaya labda nianike hadharan exams malpractices No hapana ila nimeweka wazi ili kuonesha uhalisia wa kichwa cha Uzi na yaliyomo ndani.

Baba alifanya vile kwasababu aliamini kabisa nitaenda kufeli kwasbb sikupenda kusoma kiujumla, sikuwa mtu wa kujiwek bize na msomo au elimu ya magharibi in general.

Basi nikamuitikia mzee na j3 mtihani ukaaza. Yule msimamizi alikuwa ni wakike, alikuwa anajipitisha karibu yangu ili angalau nimuite nimuombe msaada lakini sikufanya vile alivokuwa anatarajia.

Siku ya kwanza ikapita, madam alirudisha ripot kwa baba na baba aliniita ile usiku wa siku ile na akanifokea sana mixer ma singi. Nikamuahid nitafanya kama alivonielekeza, nikimjibu vile ili kumpa moyo na kumridhisha tu lakini sikupanga kabisa kufanya vile.

Mpka mtihani unaisha yule madam hakuna nikimuomba msaada na alirudisha ripot kwa Baba. Baba alinipigia sana nakumbuka na akanambia nikifeli hatapoteza pesa kunipeleka private.

Tukakakaa kusubr matokeo, baba hakuwa na vibe na matokeo alijua kabisa kashaaibika pale kijijini lakini mimi nilikuwa najua kabisa kutoboa kupo. Results zilikuja fresh na baba hakuamini kabisa na nakumbuka alinipa hongera ya mdomo tu, hakuwa na reinforcement ya rewards kabisa.

Siku moja tupo bustanini tunamwagilia nyanya na matikiti nakumbuka ilikuwa 2012 baada ya matokeo kutoka, Baba alinambia "Sasa nataka nikupeleke pre form one skul x na ukifanya mtihani wa kujiunga ukafaulu basi utasoma hiyo shule" shule hiyo ipo wilayani mjini huko nyumbani kwetu ni skul ya kikatoliki.

Habari zile kwa bro zilimletea kama wivu flan na baba ni kama alizingua lakini nilikuja kumuelewa baadae. Aliamua kunipeleka mimi na kumuacha bro aende skul ya kata kwasbb bro alikuwa anajituma katika masomo na alikuwa hahitaji skuls za vile ili afanye vzr kwahyo kwnagubile ilikuwa ani habari nzuri lakini nilikuja kuona kama vile baba ukaniona mimi mnyonge mwenye kuhitaji skul ambaya ni nzuri ili nifanye vizr.

Ilikuwa mwez wa 12 mwanzoni kabisa nakumbuka nilifungashiwa vinguo vyangu, mahindi, maharage na mchele tayar kwenda mjini kwa ajili ya pre form one. Nilikuwa naenda kukaa kwa sister wangu maana yeye alikuwa anaishi mjini.

See you...........
2006....
Nilikuwa nina miaka 9 tangu Nimeajiriwa kwenye utumishi wa umma
NIlikuwa Tayari Senior officer.......
Mwandamizi wa utumishi wa umma
 
Tuendeleee.........

Nikajiunga preform one, nilikuwa na marafiki kadhaa preform one wenzangu na pia pale skul kulikuwa na wachache tulikuwa tunafahamiana akiwemo mtoto wa baba mdogo alikuwa ni wakiume.

Niliendelea poa tu na masomo japo mwendo wangu ndo uleule wa kilevi hatua moja mbele, tatu nyuma yani hakukuwa na aliyekuwa anajielewa.

Baba alikuwa akimpigia cm dada kumuliza naendeleaje na masomo na ananionaje kiujumla. Dada alikuwa ananiteyea sometimes lakini mda mwingine alikuwa ananambia love kwamba hadhani kama nitatoboa.

Tulifanya mtihani mwezi wa 1 mwanzoni kabisa. Mtihani nakumbuka tulifanya jmoc na matokeo yalitoka j3 ya wiki ilofata.

Tulifanya masomo ma3. Hesabu, sayansi na kingereza lakini ilikuwa 3 in one.
Siku ya j3 asubuhi dada alinituma mkaa ali aje kupika tea, njiani nilikutana na wanafunzi wenzangu tulokuwa wote preform one na paper tulipiga wote. Waschana hawa wanaitwa Maria na Neema majina yao halisi.

Tulivokutana barabarani Neema akambia matokeo yametoka akaongeza kwa kusema kwamba wao ndo wapo njiani wanapenda kuangalia. Nikawaomba waniangalizie namimi kwasabb muda ule nilikuwa bize. Maria alinijibu "kwa akili zako unadhani wewe umefaulu? Akaongeza " Wewe umefeli" nikamuitikia nikamjibu "poa"

Ile kauli iliniuma sana kwasabb niliona ni dharau kubwa mtu kunambia nimefeli wakat matokeo bado hajaenda kuangalia. Neema na dada yangu wanafahamiana kwasbb dada zake Neema wapo close sana na dada yangu.

Nilivorud home nikamwambia dada kwamba matokeo yametoka nimeambiwa na kina Neema.
Sikumwambia kuhusu unabii wa akina Neema na Maria nikamute tu.

Dada akawapigia cm dada zake Neema, dada zake Neema wakamwambia kwamba Neema na rafkiake Maria wamefeli ila mimi mdogo wake nimepasi. Dada alifurahi sana na mimi pia nilifurahi mno. Nilibahatika kukutana na Neema kesho yake na akanambia eti mimi ni mchawi nimewarogezea wao wamefeli hafu mimi kilaza nimefaulu. Nikamuitikia tu "poa" then tukaachana.

Baba baada ya kupata zile taarifa alifuarah sana na akatuma pesa ya nauli nirudi kwanza nyumbani maana aliona ni kitu kikubwa sana na nitakuwa nimemuheshimisha kwa wazee wenzake kwasbb ile skul ilikuwa unaosifika sana na ilikuwa na misimo mikali kila angle ikiwemo ufaulu.

Namimi nilikuwa na shauku sana ya kurud home kwasabb nilikuwa na mpenzi wangu wa utotoni nilikuwa tu atakuwa kapata zile taarifa maana kwa sifa ya ile skul watoto wengi walokuwa wakienda kufanya mtihani walikuwa wanafeli na baadhi walikuwa wanafanikiwa.

Huyo mpenz wangu anaitwa Stella, alikuwa form one mimi nipo primary la7, alikuwa ananipenda sana japo mapenz ya utotoni mnayajua hayakuwa na madhara.

Seee you........
 
Back
Top Bottom