Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Nimeipenda hii 👇👇Tuendeleee.........
Nikajiunga preform one, nilikuwa na marafiki kadhaa preform one wenzangu na pia pale skul kulikuwa na wachache tulikuwa tunafahamiana akiwemo mtoto wa baba mdogo alikuwa ni wakiume.
Niliendelea poa tu na masomo japo mwendo wangu ndo uleule wa kilevi hatua moja mbele, tatu nyuma yani hakukuwa na aliyekuwa anajielewa.
Baba alikuwa akimpigia cm dada kumuliza naendeleaje na masomo na ananionaje kiujumla. Dada alikuwa ananiteyea sometimes lakini mda mwingine alikuwa ananambia love kwamba hadhani kama nitatoboa.
Tulifanya mtihani mwezi wa 1 mwanzoni kabisa. Mtihani nakumbuka tulifanya jmoc na matokeo yalitoka j3 ya wiki ilofata.
Tulifanya masomo ma3. Hesabu, sayansi na kingereza lakini ilikuwa 3 in one.
Siku ya j3 asubuhi dada alinituma mkaa ali aje kupika tea, njiani nilikutana na wanafunzi wenzangu tulokuwa wote preform one na paper tulipiga wote. Waschana hawa wanaitwa Maria na Neema majina yao halisi.
Tulivokutana barabarani Neema akambia matokeo yametoka akaongeza kwa kusema kwamba wao ndo wapo njiani wanapenda kuangalia. Nikawaomba waniangalizie namimi kwasabb muda ule nilikuwa bize. Maria alinijibu "kwa akili zako unadhani wewe umefaulu? Akaongeza " Wewe umefeli" nikamuitikia nikamjibu "poa"
Ile kauli iliniuma sana kwasabb niliona ni dharau kubwa mtu kunambia nimefeli wakat matokeo bado hajaenda kuangalia. Neema na dada yangu wanafahamiana kwasbb dada zake Neema wapo close sana na dada yangu.
Nilivorud home nikamwambia dada kwamba matokeo yametoka nimeambiwa na kina Neema.
Sikumwambia kuhusu unabii wa akina Neema na Maria nikamute tu.
Dada akawapigia cm dada zake Neema, dada zake Neema wakamwambia kwamba Neema na rafkiake Maria wamefeli ila mimi mdogo wake nimepasi. Dada alifurahi sana na mimi pia nilifurahi mno. Nilibahatika kukutana na Neema kesho yake na akanambia eti mimi ni mchawi nimewarogezea wao wamefeli hafu mimi kilaza nimefaulu. Nikamuitikia tu "poa" then tukaachana.
Baba baada ya kupata zile taarifa alifuarah sana na akatuma pesa ya nauli nirudi kwanza nyumbani maana aliona ni kitu kikubwa sana na nitakuwa nimemuheshimisha kwa wazee wenzake kwasbb ile skul ilikuwa unaosifika sana na ilikuwa na misimo mikali kila angle ikiwemo ufaulu.
Namimi nilikuwa na shauku sana ya kurud home kwasabb nilikuwa na mpenzi wangu wa utotoni nilikuwa tu atakuwa kapata zile taarifa maana kwa sifa ya ile skul watoto wengi walokuwa wakienda kufanya mtihani walikuwa wanafeli na baadhi walikuwa wanafanikiwa.
Huyo mpenz wangu anaitwa Stella, alikuwa form one mimi nipo primary la7, alikuwa ananipenda sana japo mapenz ya utotoni mnayajua hayakuwa na madhara.
Seee you........
Dada akawapigia cm dada zake Neema, dada zake Neema wakamwambia kwamba Neema na rafkiake Maria wamefeli ila mimi mdogo wake nimepasi. Dada alifurahi sana na mimi pia nilifurahi mno. Nilibahatika kukutana na Neema kesho yake na akanambia eti mimi ni mchawi nimewarogezea wao wamefeli hafu mimi kilaza nimefaulu. Nikamuitikia tu "poa" then tukaachana.