Tuendeleee..........
Ilipokaribia mtihan wa mwsho wa form 1 nilibadirika sana kitabia.
Hii ilikuja kufuatia siku moja nilikamatwa na headmaster akanisomea makosa yangu yote yanyuma. Nilipiga sana na walimu tofaut tofaut, baada ya kutoka pale ilnilibadirika sana.
Mwez wa 11 matokeo ya mwsho yalitoka na Mungu alisaidia nikapita kwenda form2.
Tukaenda likizo, kumbuka yule bro Daniel alonihifadhi baada ya kufukuzwa na Hamad alikuwa kamaliza form 4 ule mwaka.
Nyumbani nilikuwa nishawaambia kwamba mwaka unaofuata sitakaa tena mtaani wajipange niende bweni. Lakini Baba alikuwa anagoma.
Likizo kuisha ikawa tunatakiwa kwenda kuanza form2 mimi nikagoma nikamwambia Baba ili niendelee kusoma bas anihamishie bweni.
Baba alinifokea sana tukavutana mwsho wa siku akakubali.
Nilihamia bweni, maisha yakaanza. Kujisomea kwangu kukaongezeka kidogo na ufaulu ukaanza kupanda.
Likizo ya mwez wa6 nilienda nyumbani. Tulipokuwa likizo kulikuwa na wenzangu kadhaa wa form two ambao mwaka ule tulikuwa na mtihan wa taifa kwenda form 3.
Walikuemo pia watoto wa waalim kama ilivokuwa kwangu.
Wale wanafunzi wenzangu wa form 2 walijikusanya wakaanza kusoma kwa bro flan alikuwa kamaliza chuo kikuu.
Walikuwa wanakaa barazani wanafundhishwa, kwahyo ilikuwa ni rahisi mtu akioita nje barabarani kuwaona.
Baba siku moja jioni kapita mtaa ule kakuta kundi la watoto limemzunguka jamaa wanafundishwa. Kuangalia mimi hanioni, akatoka akaanza kunitafuta sehem zangu ambazo alikuwa anajua ni rahisi kunipata.
Ilikuwa akipita sehem na akanikosa bas anawahadithia watu ujinga wangu kwamba ananisomesha kwa hela nyingi halafu mimi sizingatii masomo wala sijitumi kusoma kwahyo mimi ni mpumbavu.
Wakati huo mimi nilikwa nipo uwanjani nacheza zangu mpira, ile natoka nipo njiani kurud home nakutania na Mzee.
Baba alinivuta maskio barabaran akanambia "wew mpumbavu nakusomesha kwa gharama hafu unaleta mchezo wenzako wanafundishwa kule wew hustuki kabisa, kwanzia kesho nikuone kule ukisoma na wenzako".
Siku hiyo ndo ilikuwa mara ya kwanza kumjibu baba anapokuwa ananifokea kwasababu ya uzembe wa kusoma.
Nikimjibu "Baba nitafaulu tu" akadakia "utafaulu kwa kutokusoma wewe ni mpumbavu".
Kesho yake ili kumridhisha Mzee nikabeba kidaftar changu nikawajoini wenzangu.
Siku hiyo tulisoma geography nikamzuga zuga pale ili kumsubir Baba akipita anikute. Mara nikamuona Mzee kapita kwa mbali akaniona. Nilivojiridhisha ukaniona nikazuga afike mbali then namm nipotee.
Alipofutikia mbali namm nikachukua kidaftar changu nikapotea. Na sikuwahi kurud tena kusoma pale na wenzangu.
Likizo iliisha tukarudi skul kuendeleza gurudum.
Muda wa paper ikafika tukafanya, turud home kusubr matokeo.
Wakat wa kusubr matokeo Baba na baadhi ya watu pale kijijini wakawa wanajua kabisa miongoni mwa watakaofeli namimi nitakuemo.
Matokeo yalivotoka katika wale walokuwa wanasoma kwa yule bro wa chuo kikuu alifaulu mmoja tu na mimi pia nilipasi hvohvo kimiujiza.
Baba alipopata matokeo hakuamini na kwanzia mwaka ule baba hakuwahi kunikumbusha nisome mpka nilipomaliza chuo.
Seee you..........