Kubezwa kwangu kulinipunguzia presha nikawa mshindi vipindi vyote

Sintokaa nkabishana na mtu tena humu jf!!!

2006??? Standard one?[emoji740][emoji740][emoji23][emoji23]

Kwahil ..huenda hata vichaa wakawa Wakutosha humu!
 
Tuendeleee.......

Ilipofika mwez wa 5 mwaka ulofata yani 2017 selections za advance zikatoka.

Zilitoka nikiwa mjini kwani kuna washkaji zangu walikuwa wanapiga skuls za serikali za pale mjini waliniomba nirudi town ili niwaboost kwenye masomo ya science walikuwa wa2 wote walikuwa form 4. Kwahyo tukawa tunapiga mapindi kimtindo pale magetoni.

Siku selections zinatoka nilikuwa na washkaji zangu tulomaliza nao olevel ile skul nilosomea mimi. Basi kuna mshikaji alitoa wazo kwamba twende kwao kuna laptop tukaangalie selections.

Tulienda kwao tukiwa kama washkaji wa5, tulipofika tuliwakuta wazaz wa yule mshkaji pamoja wa watu kadhaa pale kwao. Jamaa alileta laptop akaunganisha na cm ili apate internet access katika Ile PC.

Tulipofungua mkeka wa selections washkaji zangu wote wa4 walikuwa wamechaguliwa skuls nzuri nzuri na zenye CV nzuri kuzid skul ambayo nilichaguliwa. Wawili walichaguliwa lymungo, mwingine Tanga tech na hiyo wa4 alipelekwa old moshi.

Kuja kuangalia mimi nimetupwa skul moja hivi ipo kigoma, skul skuwahi na hakukuwa na hata mmoja mwenye alikuwa anaifaham.
Pale seburen wote walicheka mpka wazazi wa yule jamaa.
Wale washkaji wakanambia "we jamaa huko kigoma unaenda kupotea kabisa skul gani hiyo ulopelekwa"

Nilifreez kwa muda nikaanza kupata mawazo mengi tofauti tofaut. Mawazo mengine ya kuachana na elimu, mengine ya kwenda chuo yani nilivurugwa kweli.

Baadae nilimchek bro nikamueleza akanipa moyo kwamba kufaulu advance kwa asilimia kubwa kunachangiwa na juhudi binafsi kwahyo nisizingatie sana status ya skul. Nilimchek pia baba akanipa moyo pia mama naye hakuwa na la kusema ila kunipa Baraka zake.

Nilienda kuripot nakumbuka ilikuwa mwez wa 7, kigoma hiyo mabas ya Saratoga na nbs ndo yalikuwa yameshika hatam kwa kiasi kikubwa miaka ile.

Nilifika skul ilikuwa saa12 jioni, nikashuka stend uzuri skul haipo mbali sana na stand. Kulikuwa n washkaji kadhaa ambao ni ma bro zangu waliniacha form3 olevel kwahyo nilipata kampani ya kuniondolea wenge.

Nilichelewa kuripot kama wiki moja hivi, usiku wa siku ile nilioripot niliamua kwenda kuzuga class baada ya kuset mazingira ya kulala bwenini.

Nilipoingia class nilikuta washkaji (skul ilikuwa ya boys only advance ila olevel mchanganyiko na walikuwa wanatokea nyumbani).
Nilikuta wajuba wapo bize na misuli kuna vitabu vinaitwa Chand, BS, Understanding, n.k.
Hivi vitabu najua wengi wanavifaham ni vitabu vikuwa kimuonekano na vinaleteana woga kwa mara ya kwanza mtu kuvitumia hasa kama haukuwa umesoma tuition.

Mimi mtaani sikutoka nimemsoma tuition yani nilitoka na scientific calculator na madaktari mapya.
Ile siku kiukweli nilipata woga sana kwasabb nikllikuwa sijui nianzie wapi na nilijikuta nafikiria kwamba wale walokuwa wanasovu na kusoma mavtabu makubwa kama yale basi wao ndo tyr washatoboa na mimi nipo katika probability ya 0.1 ya kufaulu na 0.9 ya kufeli.

Sikukaa hata dk20 nikawa nimetoka nikajisemea "liwalo na liwe" nikatoka nikarud dom nilikuwa na kisim changu nikarud kuchat na yule mke wa boss wa kampuni ya magari ya abiria kwenye Uzi wa Mercy nilimuelezea huyu mama.

Muda ulikuwa umeenda sana kwahyo hata yule mama sikumpata hewani nikaamuwa kumchek mchuchu mwingine nikapotezea muda then nikalala.

Kesho yake ilikuwa siku yangu ya kwanza ya masomo advance.


Seee you.........
 
Mungu ampe mzee wangu Maisha marefu sana. Alininunulia vitabu vyote kuanzia Physics. Chemistry and Biology. Hivyo Chand, BS mpaka leo vipo tu home.
 
Jamii forum hivi hata hiyo jf expert member mnawapa na watoto pia.....๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜ƒ
 
Nitag kwenye uzi wa Mercy niupitie Mkuu
 
Tuendeleee........

Kesho yake nikaamka nikajiandaa kwenda class, nilipigilia sare zangu vzr tukaingia skul.

Siku zile za mwanzo class nilikuemo kimwili tu ila kiakili sikuwa sawa kabisa kwasababu nilikuwa kama nishajikatia tamaa. Sikuwa naelewa chochote wenzangu mda huo wanaendelea na disc, mapindi na kusov individually mimi natoa macho tu sielewi.

Siku moja tulikuwa prepo za usiku nilikuwa na washkaji kama wa2 namm wa3, hao jamaa ni waha wa kigoma huko. Tulikuwa tunadscuss kitu flan kwenye biology sasa wao walikuwa Wana idea na Ile kitu wakanitaka nitoe mchango wangu nini nachokielewa. Nilivotoa nilichokiwa nakielewa jamaa walicheka sana wakadai nimekosea pakubwa yani nimemix pilau na mlenda. Jamaa mmoja akasema "we jamaa tushakupoteza tayar".

Hii kauli ilinikata sana na nikakosa confidence kabisa. Nkazuag zuga kama dk 15 nikawaaga naenda kulala.
Nilipofika bwenini nikachukua kicm changu nikamvutia waya father nikamwambia sitaki tena kusoma nataka kurudi home. Baba aliniuliza shida nini nkamwambia mimi huku sielew chochote na tuition sikusoma ndo kabisa sijui nianzie wapi.

Baba aliniita sana moyo sana sana alitumia kama dk30 kunifariji na kunipa ujasiri wa kuendelea. Hatimaye nilimuelewa nikarud bwenini nikapiga mbonji.

Siku zilisonga kibabe hivohivo huku nawaza nini cha kufanya ili nikae sawa.

Nilipata wazo la kuwafata ma bro wa form 6 ili wanipige msasa angalau ili nipate pakuanzia.

Nakumbuka kuna huyo bro tulikuwa tunakuita Ngosha na mwingine Malila. Hawa jamaa nilikuwa nawahusuda sana kwasabb walikuwa poa sana class na walikuwa wanajali wenye kuhitaji katika kufundishwa.

Nilikuwa napigiwa mapindi na hawa jamaa halafu nawafata ma bro wengine wananitungia mitihani nakuwa anafanya.
Nakumbuka chem paper la kwanza kabisa nilipata 17/100 ๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€. Hii kitu ilinipunch kiasi ila nikajisemea fresh tu ngoja nikaza.

Nilimpigia mapindi kama mwez na nusu hivi nikaanza kuona mabadiriko makubwa na mitihani nikaanza kuipiga vizur vzur ukilinganisha na mwanzo.
Hapa nikaanza kuona kwamba kumbe kufaulu inawezekana ngoja nikaze zaidi.

Upande wa chem nilikuja kugundua kuwa nlbado sipo vzr. Nilichokifanya nilidedicate wiki nzima kwenye chem.
Nilirudisha materials ya masomo yote bwenini class nikabak na materials ya chem tu. Materials mengine nilikuwa nakuja nayo class kutokea dom kwa ajili ya vipindi vya darasani na walimu.

Ile wiki nzima nilikuwa nawaza na kusoma chem tu. Hii kitu ilizaa kitu kikubwa sana kwasababu nilijikuta Siri ya kufaulu chem naipata na kwanzia hapo nikawa moto upande wa chem.
Baada ya hapo yale materials mengine nikayarudisha class nikaendelea na ratiba kama kawaida.

Kazi nyingne ikaja kwenye BAM, hii nilikuwa sina ujanja ikanibidi nitafute ufaulu wa kawaida tu mrad nisipate F sikutaka minimize sana akili.


Sasa wale washkaji zangu wa2 nilokuwa napenda kusoma nao na kufanya nao disc nikawa naenda nao sawa katika discussions maana mwanzo nilikuwa nipo nipo tu ila Sasa nikaanza kwenda na beat namimi.


See you..........
 
Tuendeleee........

Siku zilisonga na mambo yangu katika masomo yalizid kuwa mazuri hvohvo kadri siku zilivokuwa zinaenda.

Pale skul kulikuwa na utaratibu wa talent day yani siku ya kuonesha vipaji, muziki ulikuwa unapigwa hafu mwishoni ni disco.
Kumbuka Toka olevel nilikuwa napenda music dancing kwahyo siku hiyo nilikuwa na vibe sana japo sikujua naanzia wapi.

Kulikuwa na washkaji wa3 walikuwa tayar washajigroup ili waende kuonesha talent yao ya kucheza mziki. Nilivowaona wanajiandaaandaa ile hasubuhi nikawafata nikawaomba nijoin group.
Jamaa hawakuwa na hiana wakanikubalia tukaanza kupanga scenes pale.
Nilionesha uwezo mzuri jamaa wakanielewa na tukapanga kabisa show nzima itakuwaje.

Muda wa show ulipofika tuliingia tukatoa show moja kali sana kias kwamba wanafunzi wote na walimu walitukubali na tulitunzwa pesa nzur tu.
Group letu tulilipa jina flan sitalitaja, group hilo lilikuwa maarufu sana sio skul ile tu bali mpka skuls za pembeni pale mjini.

Ile kitu ilinipa umaarufu sana pale skul. Wakati huo tulikuwa tushafanya mtihani mmoja ulikuwa ni mtihani wa mwezi wa 9 na performance yangu ilikuwa ya kawaida tu.
Siku moja ticha wa chem alitoa test nikapata 30/100 Sasa wakat wa kugawa karatas akaropoka "wewe kucheza unajua ila darasani chenga, wew usipoangalia utafeli"
Yale maneno yalinigusa japo mimi ndo nilikuwa najua hali halisi juu ya kufeli kwangu kwahyo haikunipa stress sana kivile.

Siku zilisonga ikafika siku ya graduation ya form 4, kama kawa tuliibuka sisi kama group tukafanya yetu tukauwa siku hiyo tukipata maokoto mengi sana.

Mwez wa 11 ilifika tukafanya paper la kumaliza muhula wa kwanza wa form5. Baada ya paper tulifunga tukarud home, mpka tulipofungua mwez wa1 mwaka ulofata.
Tulipofungua tukakuta matokeo tayari yameshatayarishwa na kulikuwa na utaratibu wa kusoma matokea parade yani wanasomwa best ten students.

Siku hiyo ilikuwa siku muhim sana kwasabb nilikuwa najua kabisa ni lazima ningekuwemo kati ya wale wanafunzi 10 bora japo asilimia 90 ya wanafunzi na walimu pale skul walikuwa hawaoni kama mimi ningekuwa mwanafunzi wa aina ile.

Academic teacher alisimama akaanza kusoma majina, kasoma wakwanza na wa2 then wa3 akataja jina langu shule nzima wanafunzi wakaguna "mmmmmh" mimi nikaenda zangu nikapewa zawad yangu nikatulia pale mbele na wenzangu.

Zoez likikamilika na katika lile group letu aliyetajwa nilikuwa ni mimi tu. Kule kuguna kwa wanafunzi kulinifanya nijihisi mtu wa kutokuaminiwa katika jamii kwasbb tangu primary hali ilikuwa ni ile tu yani nabezwa kutokana na lifestyle yangu najikuta watu wanaona kama vile siwez chochote cha maana.

Baada ya pale wanafunzi wakaanza kuniheshimu na kuniangalia kwa jicho la kipekee kidogo na pia walimu walianza kunichukulia serious.

Wale ma bro ambao waliniacha olevel wao hawakuwa wanashangaa sana kwasabb walikuwa wananifaham kwan hata olevel maisha yangu yalikuwa ni ya vilevile.

Mwez wa 3 ikafika tukafanya mtihani wa kid term....

See you...........
 
Basi itakuwa ulikuwa kilaza promax kama mwaka 2012 dingi alikuwa anawazia wewe kufeli mtihani. Inasikitisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ