Kuchange jina la kozi ili uombe kazi Ajita portal

Kuchange jina la kozi ili uombe kazi Ajita portal

Mkuu nisaidie kitu hapo.. Kuna Ajira za SUA zimetangazwa hvyo kozi zilizowekwa ni sawa kabisa na yangu(Equivalent) Ila nikiomba inakata nisaidie maujanja hapo ili niombe mkuu.. nofanyaje kwenye hii account yangu..?
Mimi kozi yangu ipo Mara mbali
 
Water Resources and irrigation engineering
Mwamba niliwahi sikia watu waliosoma chuo cha maji ubungo ama kozi za maji wanaajiriwa mojamoja kupitia wizara ya maji,inakuwaje wewe unahaso ivyo
 
Mwaka gani mkuu..? Ila siku hizi mbona wanatahja course husika na wanaongezea na Equivalent course..

Ushauri wangu.

Kama mkoa itakayofanyika interview hautumii pesa ya nauli kubwa fanya hicho unachosema ila kama ni mbali sishauri sana.

Mimi kozi yangu iliwekewa tangazo iandikwe kama 'Community Development' baada ya kuandika nikaja kuapply post ya Warden. Nikawa shortlisted.

Nilivyofika nikaambiwa nimeidanganya system kwakua Jina la kozi kwenye cheti haliendani na kilichoandikwa kwenye portal.

I did walichoelekeza na bado wakanikatalia.

Nikarudi home bila kufanya usaili.
 
Nilishawahi fanya kama mleta uzi kipindi cha nyuma. Mrejesho ulikuja walinitema yaani sikufit qualifications zao ilihali nilikua nimefit. Ushuhuda wa skrinshot upo chini.

Mfumo ukikukataa unakua kama ule msemo wa kimakonde "Ukisimama nchale ukichuchumaa nchale"
🤣🤣 Weka ushuhuda huo Boss
 
Back
Top Bottom