Hata waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliugua covid akawekwa kwenye ICU na oksijen kibao na alikuwa taaban mpaka watu wakadhani jamaa atachomoka lakini bahati yake baada ya zaidi ya wiki 2 au 3 akapona lakini mke wake ambaye alikuwa ni mja mzito aligunduliwa naye ameambukizwa lakini hakupata shida yeyote ile, wala hakulazwa hospitali hata siku moja, huu ugonjwa ni wa ajabu sana, kwahiyo usidhani kila mtu atakayeambukizwa atalazimika kwenda hospitali, wengine wanapata covid mpaka inaisha bila kujua kama aliugua, lakini wengine wakiupata moto unamuwakia, Sasa kwa kuwa hatujui nani akipata itamdhuru na nani hats akipata haitamdhuru ndio maana tunahamasishana tuende tukachanje bandugu