KERO Kuchelewa kwa pension zinazolipwa na Hazina

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

alibaaliyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2017
Posts
623
Reaction score
576
Pension zinazolipwa na Hazina kwa Wastaafu zimekuwa zilicheleweshwa bila taarifa kwa wastaafu.

Hadi sasa tarehe 12 July 20124, pension hizi hazijapatikana.

Pension hizi huwafaa wastaafu katika maswala mbali mbali kama chakula, matibabu na nk.

Hivyo kitendo cha kuchelewesha pension hizi wanaathirika kwa mengi.

Kama kuna tatizo tuarifiwe.
 
Haya mambwa ya ccm mwisho wao hauko mbali utaona tu.
 
pension ya mwezi June mbona tulishalipwa. wewe kuna changamoto gani mpaka sasa hujalipwa? umeshafuatilia?
 
Kwa hii serikali ya Chura Kiziwi mtafika mmechoka sana
 
Katika miezi kadhaa ya hivi karibuni kumekuwa na mtindo mpya wa Hazina kulipa pension ya wastaafu ya kila mwezi tarehe 10.Ni mtindo ambao naona unazoeleka sasa.Kwa nini ni vigumu kujua,lakini kwa upande wa wastaafu,zipo sababu za msingi zifuatazo ambazo tunadhani ndizo zinazoletelea hali hiyo.
1.Kutojali maslahi ya wastaafu ambao baada ya kuitumikia serikali kwa miaka takriban 35,sasa wanaonekana hawana thamani yeyote na wanaweza kufanyiwa lolote.
2.Dharau na kutojali wazee hawa,kwa kudhani kwamba malipo wanayolipwa ni kama takrima,kwa hiyo wanaweza kulipwa wakati wowote atakapo taka mtoaji ambaye ni serikali.

Hata hivyo naomba ikumbukwe kwamba malipo haya yapo kisheria,kwa hiyo ni haki ya mstaafu,sio takrima,kwa hiyo yanapaswa kulipwa kwa wakati,ili mstaafu aweze kuendesha maisha yake, pamoja na ukweli kwamba pension hiyo ni ndogo sana,na inahitaji marekebisho.

Kama hazina ingekuwa inajali wastaafu,udogo wa pension ingekuwa sababu tosha ya kulipa wastaafu mapema,ili waweze kuitumia kujikimu.Inashangaza kwamba pamoja na udogo wa pension hiyo,bado inacheleweshwa kulipwa.Hii inadhihbitisha jinsi hazina isivyokuwa na huruma kwa wastaafu,isivyojali,na inavyowa kdharau wastaafu.
3.Uzembe:Upo uzembe wa wazi katika swala hili,kwa kuwa mbona awali iliwezekana kulipa mapema?Tunaomba hazina wawe na huruma,wakumbuke kwamba wastaafu nao ni watu,kwa hiyo wanastahili kula na kunywa kama wao.

Nimalizie kwa kusema hivi,watendaji wa hazina wakumbuke kwamba ni wastaafu watarajiwa,kwa hiyo msingi wanaouweka sasa utakuja kuwaathiri baadae. Wasilotaka kutendewa wao,wasiwatendee wenzao.
 
Zanzibar pension za Hazina zikichelewa trh 25 ya mwezi husika. Kwa upande wa ZSSF zikichelewa trh 17 ya mwezi husika. Wazee saivi wanapeta kuliko sie waajiriwa. Mwinyi Muungwana sana
 
Kwani Nini maana ya tarehe, kama mzunguko umetimia!? Say 25 Hadi 25 jumla siku 30, 10 Hadi 10 jumla siku 30, Sasa Nini chimbuko la hoja Yako!?
 
Laiti tungekuwa na Rais muungwana na strong Tanzania Bara kama Mwinyi.He is a very morally sound leader.Yaani hazina wanafanya wanavyotaka,na hakuna wa kuwakeme.No,lazima wawajibishwe ili wawajibike ipasanvyo.Walikuwa wanalipa latest tarehe 26,now all the way to the 10th,no haikubaliki.
 
Kwani Nini maana ya tarehe, kama mzunguko umetimia!? Say 25 Hadi 25 jumla siku 30, 10 Hadi 10 jumla siku 30, Sasa Nini chimbuko la hoja Yako!?
Acha ujinga wewe.Hata kama swala ni mzunguuko,mbona ilikuwa tarehe 26,isibaki hiyo hiyo.Na kama swala ni mzunguuko,kwa nini mishahara isilipwe tarehe kumi ya kila mwezi?
 
Katika miezi kadhaa ya hivi karibuni kumekuwa na mtindo mpya wa Hazina kulipa pension ya wastaafu ya kila mwezi tarehe 10.Ni mtindo ambao naona unazoeleka sasa.Kwa nini,ni vigumu kujua,lakini kwa upande wa wastaafu,zipo sababu za msingi zifuatazo:
1.Kutojali maslahi ya wastaafu ambao baada ya kuitumikia serikali kwa miaka takriban 35,sasa wanaonekana hawana thamani yeyote na wanaweza kufanyiwa lolote.
2.Dharau na kutojali wazee hawa,kwa kudhani kwamba malipo wanayolipwa ni kama takrima,kwa hiyo wanaweza kulipwa wakati wowote atakapo taka mtoaji ambaye ni serikali.

Hata hivyo naomba ikumbukwe kwamba malipo haya yapo kisheria,kwa hiyo ni haki ya mstaafu,sio takrima,kwa hiyo yanapaswa kulipwa kwa wakati,ili mstaafu aweze kuendesha maisha yake, pamoja na ukweli kwamba pension hiyo ni ndogo sana,na inahitaji marekebisho.

Kama hazina ingekuwa inajali wastaafu,udogo wa pension ingekuwa sababu tosha ya kulipa wastaafu mapema ili waweze kuitumia kujikimu.Inashangaza kwamba pamoja na udogo wa pension hiyo,bado inacheleweshwakulipwa.Hii inadhihitisha jinsi gani hazina isivyokuwa na huruma kwa wastaafu,isivyojali,na inavyodharau wastaafu.
3.Uzembe:Upo uzembe wa wazi katika swala hili,kwa kuwa mbona awali iliwezekana kulipa mapema?Tunaomba hazina wawe na huruma,wakumbuke kwamba wastaafu nao ni watu,kwa hiyo wanastahili kula na kunywa kama wao.

Nimalizie kwa kusema hivi,watendaji wa hazina wakumbuke kwamba ni wastaafu watarajiwa,kwa hiyo msingi wanaouweka sasa utakuja kuwaathiri baadae.Ni vizuri wakatambua kwamba wasilotaka kutendewa wao,wasiwatendee menzao.
Mkuu emb fafanua ni wastaafu wa mfuko gani wanaocheleweshewa pensheni zao za mwezi namna hiyo.

Maana Wastaafu wote wa hazina Tz bara wanalipwa sambamba na wafanyakazi siku ya mshahara ama kesho yake.

Mi siyo mtetezi wa Serikali ila nazungumza kwa confidance 100%.
 
Nimesema pension zinazolipwa na Hazina,sio za mifuko,za mifuko zinakuja kwa wakati.
 
Mkuu emb fafanua ni wastaafu wa mfuko gani wanaocheleweshewa pensheni zao za mwezi namna hiyo.

Maana Wastaafu wote wa hazina Tz bara wanalipwa sambamba na wafanyakazi siku ya mshahara ama kesho yake.

Mi siyo mtetezi wa Serikali ila nazungumza kwa confidance 100%.
Si kweli,ingekuwa hivyo kusingekuwa na haja ya bandiko hili.Umesema huitetei serikali,lakini kwa bandiko hili,unaitetea serikali,kwa kuwa umeandika uongo.
 
Mkuu mi ni retired. Sisemi kwa kubahatisha.

Ndiyo maana nikakuomba unitajie mfuko ili kuweka habari yako sawasawa.

Ukisema wastaafu wa nchi hii kwa ujumla wao ni uongo wa mchana kweupe.

Ukitaka nikupe uthibitisho wa tarehe za kila mwezi namna tulivyolipwa kuanzia Jan mwaka huu ninaweza.

Hakuna siku yoyote tuliyolipwa zaidi ya Trh 25 tangia mwaka huu uanze.

Enzi za Magufuli mara nyingi tulikuwa tunalipwa kabla ya mishahara kutoka.

Na mwaka huu kuna mwezi mmoja pensheni ilitoka kabla ya mishahara.

Nb. Mi pensheni yangu nachukulia hazina.
 
Mimi pia ni mstaafu,lakini pension ya mwezi uliopita wamelipa juzi Jumamosi tarehe 10!Mkuu unaweza kuwa mstaafu lakini bado ukawa chawa wa serikali.Lakini pia inawekana sio mstaafu,unatembeza uchawa tu.Na sioni uwezekano wa serikali kulipa pension in batches,wewe ni mwongo na chawa.
 
Back
Top Bottom