Katika miezi kadhaa ya hivi karibuni kumekuwa na mtindo mpya wa Hazina kulipa pension ya wastaafu ya kila mwezi tarehe 10.Ni mtindo ambao naona unazoeleka sasa.Kwa nini,ni vigumu kujua,lakini kwa upande wa wastaafu,zipo sababu za msingi zifuatazo:
1.Kutojali maslahi ya wastaafu ambao baada ya kuitumikia serikali kwa miaka takriban 35,sasa wanaonekana hawana thamani yeyote na wanaweza kufanyiwa lolote.
2.Dharau na kutojali wazee hawa,kwa kudhani kwamba malipo wanayolipwa ni kama takrima,kwa hiyo wanaweza kulipwa wakati wowote atakapo taka mtoaji ambaye ni serikali.
Hata hivyo naomba ikumbukwe kwamba malipo haya yapo kisheria,kwa hiyo ni haki ya mstaafu,sio takrima,kwa hiyo yanapaswa kulipwa kwa wakati,ili mstaafu aweze kuendesha maisha yake, pamoja na ukweli kwamba pension hiyo ni ndogo sana,na inahitaji marekebisho.
Kama hazina ingekuwa inajali wastaafu,udogo wa pension ingekuwa sababu tosha ya kulipa wastaafu mapema ili waweze kuitumia kujikimu.Inashangaza kwamba pamoja na udogo wa pension hiyo,bado inacheleweshwakulipwa.Hii inadhihitisha jinsi gani hazina isivyokuwa na huruma kwa wastaafu,isivyojali,na inavyodharau wastaafu.
3.Uzembe:Upo uzembe wa wazi katika swala hili,kwa kuwa mbona awali iliwezekana kulipa mapema?Tunaomba hazina wawe na huruma,wakumbuke kwamba wastaafu nao ni watu,kwa hiyo wanastahili kula na kunywa kama wao.
Nimalizie kwa kusema hivi,watendaji wa hazina wakumbuke kwamba ni wastaafu watarajiwa,kwa hiyo msingi wanaouweka sasa utakuja kuwaathiri baadae.Ni vizuri wakatambua kwamba wasilotaka kutendewa wao,wasiwatendee menzao.