Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

Nevilly

Senior Member
Joined
Jul 9, 2014
Posts
168
Reaction score
312
Habari zenu binadam wenzangu, wanajamii wenzangu, natumai ni wazima wote.

Swali linalo nisumbua na kunitesa hadi sasa ni kwanini nipo kwenye mfumo wa kuchelewa chelewa sipati jbu.

Umri wa mwanadamu wa kuishi ni miaka 60 tu, na mimi miaka 30 sasa ni Nusu ya umri wa binadam kuishi duniani ila sioni nilichofanya hadi sasa najiona nimechelewa.

Mfano halisi ,baadhi ya sehemu nilizochelewa

Mzee wangu alinipa matumaini makubwa sana ya kusapoti life pindi mafao yatakapo toka(pensheni) ila mafao yake yalipoingia tu akanipiga chini na kunifukuza home kabisa bila sababu za msingi (30yrs now) NIMECHELEWA

Sasa Nina miaka 30, ila nina miezi mitatu tu hadi sasa ya kupanga sijawahi kupanga, NIMECHELEWA

Sijawahi kuajiriwa hata siku 1. Ila nimewahi kufanya kazi chuo kikuu ya kurekebisha na kutengeneza vifaa vya maabara mfano kutengeneza test tube, kuripea burrets zilizovunjika kwa muda wa miaka 3 pale chuo kikuu (UDSM) bila malipo. (30yrs now), NIMECHELEWA

Nina majonzi ya kutengeneza app tokea nna miaka 25 ninajfunza tu ninajfunza Ila hazijanipa muelekeo wowote. (30yrs now) NIMECHELEWA

Napenda sana kufanya project zangu mwenyewe lkn Kila nikipanga mipango haitimii kwa wakati, inachelewa sana sana na haijatimia hadi sasa. (30yrs now) NIMECHELEWA

Sasa Ndugu Wameanza kunitamkia live, mbele ya sura yangu nioe wameniona ..NIMECHELEWA

Marafiki zangu wote wana watoto kasoro mimi tu, (30yrs now) NIMECHELEWA

Hadi sasa sina mpenzi wakusema huyu nifanye nae life hahaha. (30yrs now) NIMECHELEWA

Miaka 14 imepita tokea nimalize form 4, sioni jambo la msingi nililofanya (30yrs now) NIMECHELEWA

Pesa yangu siielewi inaingia kimazabe zabe, niliwatengenezea watu wawili website, mmoja ni mtu maarufu tu star mkubwa mwenye kanisa lake town hapa ila aliishia kuniahidi tu, mwisho wa siku niliambulia elfu 20 yake kutoka kwenye makubaliano ya 600,000sh nayo alinipa kwa sababu alijistukia kupoteza muda wangu.

Mwingine ametoka kunipa elfu 30 wakati alitakiwa kunipa 500,000 sh na story kibao za kuninyima haki yangu. Miaka 30 nafanya dili dhaifu kama hizi kweli NIMECHELEWA

Almost kila siku tokea mwaka huu uingie nawaza kusafisha nyota ila mwez wa kumi sasa

-------NIMECHELEWA------

Ok huku kuchelewa nakuona sio kwa kawaida

Yoyote Aseme kitu kinaweza kuwa mwanga wa safari yangu.
 
Sijaona ukilaumu umechelewa kufa maana wapo wanaokufa chini ya 30yrs.

Jifunze kushukuru kwa yote kuna watu wa umri wako hawana ulivyo navyo wewe na bado Wana matumaini.

Kwa miaka 30 bado kijana kabisa na muda wa kutimiza yote hayo bado upo.

Sijaona sehemu ulipo chelewa ni suala la muda tu mambo yatakuwa powa.
 
SI Bora ungenitengenezea Mimi app nikupe hata laki Moja duh ila asee yaani amekupa 20000,30000 tu halafu Ni ma star...wakati mm kapuku ningekuwezesha nyingi Zaidi pole Sana ndo maana naonaga Bora mtu ufanye kazi na maskini kuliko na matajiri maana Wana dharau hawalipi madeni

Miaka 30 mbona huna tofauti na Mimi 28.

Sina mke
Sina mtoto
Sina mchumba

Bht nzuri tu Mimi Nimefanikiwa kuingia Serikali mwaka huu pole tusikate tamaa, tutafute mademu wa vijijini ndo rahisi kuwazalisha Hawa wa mjini cum a Nina zao
 
kwenye maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa,kila jambo ni kwa muda wake na Mungu ndio hujua jambo gani na atupe kwa muda upi.

Hao unaowafanyia kazi uwe unaandikishana nao au kabla ya kuwafanyia kazi wawe wanakulipa 50% ya gharama na ukimaliza kazi zao wanamalizia 50% iliyobaki.

Mfano mmoja ni Biden amekua Rais wa USA akiwa na umri wa miaka 78

Babu wa Loliondo alitoboa uzeeni,
Mzee mpili kapata umaarufu uzeeni
Pierre liquid katoboa uzeeni...

Enjoy ur life bro,usisubiri kukamilisha jambo fulani ndio uwe na furaha,uhai wenyewe ni zawadi tosha kabisa,

Good luck Brother.
 
Kwenye maisha hamna kuchelewa wala kuwahi na kila jambo na majira na wakati wake ka ilivo maandiko, so usihuzunike panga mikakati ya kuvuka kwenda hatua nyingine imagine miaka hyo 30 ni wangapi hawapo duniani ka wewe.

Imagine trump kapata Urais na miaka 70s while Obama alipata Urais kwenye umri wa 50s ka sikosei, Joe biden alijaribu mara nyingi ila amekuja kupata Uraisi mda sahihi kwake huku umri ukiwa mkubwa kabisa.

So usi regret njoo na new strategy za kukuvusha mengine huchelewa kwenye maisha Ili kujifunza na tu grow kwanza ku handle situation. Pia waweza pata mafanikio ghafla lakini ukafariki mapema, tushukuru kwa kila jambo jamani
 
Sijaona ukilaumu umechelewa kufa maana wapo wanaokufa chini ya 30yrs

Jifunze kushukuru kwa yote kuna watu wa umri wako hawana ulivyo navyo wewe na bado Wana matumaini...
Naashukuru mkuu.

Ila kifo huwaga akipo kwenye list za maswala ya mafanikio au maendeleo.

Hiyo ni nature mkuu huwez ukalist kfo labda na nnge list kifo wote mgenion sio mzima

Ila ni ushaur mzur .. asante
 
kwenye maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa,kila jambo ni kwa muda wake na Mungu ndio hujua jambo gani na atupe kwa muda upi...

Da umeongea vzuri sana brother.

Sema kpengele cha kutoboa uzeen kgumu sana kukimeza.

Sidhan kama kuna mtu anataman ktoboa uzeeni.

Ila huwez kuzuia ktoboa uzeeni.

Ushauri wa 50/50 naanza kuufanyia kazi.

Shukran
 
Kijana mdogo tuliza akili, unataka kukimbilia wapi? Ongeza juhudi na mipango hujachelewa, na usikimbilie kuoa kabla hujapata ramani ya maisha.. kama shughuli unazofanya hazikuendelezi tafuta shughuli nyingine, fanya kwa bidii na jiwekee malengo utafanikiwa
 
Back
Top Bottom