Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

Kuchelewa kwangu kunanitisha sana

Habari zenu binadam wenzangu, wanajamii wenzangu, natumai ni wazima wote.

Swali linalo nisumbua na kunitesa hadi sasa ni kwanini nipo kwenye mfumo wa kuchelewa chelewa sipati jbu.

Umri wa mwanadamu wa kuishi ni miaka 60 tu, na mimi miaka 30 sasa ni Nusu ya umri wa binadam kuishi duniani ila sioni nilichofanya hadi sasa najiona nimechelewa.

Mfano halisi ,baadhi ya sehemu nilizochelewa

Mzee wangu alinipa matumaini makubwa sana ya kusapoti life pindi mafao yatakapo toka(pensheni) ila mafao yake yalipoingia tu akanipiga chini na kunifukuza home kabisa bila sababu za msingi (30yrs now) NIMECHELEWA

Sasa Nina miaka 30, ila nina miezi mitatu tu hadi sasa ya kupanga sijawahi kupanga, NIMECHELEWA

Sijawahi kuajiriwa hata siku 1. Ila nimewahi kufanya kazi chuo kikuu ya kurekebisha na kutengeneza vifaa vya maabara mfano kutengeneza test tube, kuripea burrets zilizovunjika kwa muda wa miaka 3 pale chuo kikuu (UDSM) bila malipo. (30yrs now), NIMECHELEWA

Nina majonzi ya kutengeneza app tokea nna miaka 25 ninajfunza tu ninajfunza Ila hazijanipa muelekeo wowote. (30yrs now) NIMECHELEWA

Napenda sana kufanya project zangu mwenyewe lkn Kila nikipanga mipango haitimii kwa wakati, inachelewa sana sana na haijatimia hadi sasa. (30yrs now) NIMECHELEWA

Sasa Ndugu Wameanza kunitamkia live, mbele ya sura yangu nioe wameniona ..NIMECHELEWA

Marafiki zangu wote wana watoto kasoro mimi tu, (30yrs now) NIMECHELEWA

Hadi sasa sina mpenzi wakusema huyu nifanye nae life hahaha. (30yrs now) NIMECHELEWA

Miaka 14 imepita tokea nimalize form 4, sioni jambo la msingi nililofanya (30yrs now) NIMECHELEWA

Pesa yangu siielewi inaingia kimazabe zabe, niliwatengenezea watu wawili website, mmoja ni mtu maarufu tu star mkubwa mwenye kanisa lake town hapa ila aliishia kuniahidi tu, mwisho wa siku niliambulia elfu 20 yake kutoka kwenye makubaliano ya 600,000sh nayo alinipa kwa sababu alijistukia kupoteza muda wangu.

Mwingine ametoka kunipa elfu 30 wakati alitakiwa kunipa 500,000 sh na story kibao za kuninyima haki yangu. Miaka 30 nafanya dili dhaifu kama hizi kweli NIMECHELEWA

Almost kila siku tokea mwaka huu uingie nawaza kusafisha nyota ila mwez wa kumi sasa

-------NIMECHELEWA------

Ok huku kuchelewa nakuona sio kwa kawaida

Yoyote Aseme kitu kinaweza kuwa mwanga wa safari yangu.
Ukweli ni kwamba bado hujachelewa! Kuna watu nimesoma nao degree ya kwanza walikuwa in their 40’s na mwingine 45 leo maisha yao yapo vizuri tu.

Wengine tupo 45 sasa hatujaoa na yatakuwa mazuri tu japo kuna shida zake.

Ni vizuri mno umeshtukia hali yako mapema kwani itakusaidia usiingie kwenye kuchelewa kubaya.

Nakushauri rekebisha hulka yako ya kufanya maamuzi, usisubiri sana upate hela ndio uoe.

Pia fuatilia sana masuala yako ya kiroho. Ee bwana kucheleweshwa kupo na heri wewe umeshtukia mapema!

Fanya sala, mwombe Mungu, nenda kwa watumishi wa kweli anza kushughulikia jambo hilo, ukweli kuchelewa ni kubaya mno!
 
Back
Top Bottom