Kucheleweshwa kwa Mkopo World Bank: Tumkemee Zitto Kabwe kwa pamoja

Elia F Michael,
Hicho ndo kiingereza cha ZItto? Kumbe ana mengi ya kujifunza badala ya umbea anaohangikia. Poor english language command! Sijui akizungumza hali ikoje! Kila siku ni kuzomea magufuli kumbe na wao ni hoi!

Angalia sababu anazozieleza sasa! Mara gender, mara Kabendela, mara mikutano ya siasa. Hakuna hata sehemu moja anapotetea watu kukosa maji na umeme! Anaomba mkopo usitishwe kwa sababu tu ya mambo ya kisiasa, siyo maendeleo duni ya wananchi. Rubbish!

..inawezekana masuala ya gender, uhuru wa vyombo vya habari, na demokrasia, yakawa siyo muhimu kwetu.

..lakini masuala hayo ni muhimu kwa wafanya maamuzi wa WB ambao ndio walengwa wa barua ya Mh.Zitto Kabwe.

..nadhani njia sahihi ktk hili ni serikali kuwahakikishia WB kuwa hoja za Zitto na wanaharakati zitashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
 
Barua niliyoandika Benki ya Dunia ni hii. Nipo tayari kulipa gharama yeyote kwa kuandika Barua hii. Serikali ya Rais Magufuli inapaswa kujua, naikumbusha tena, kuwa SIOGOPI lolote katika lile ninaloamini. Nataka kila Mtoto wa kike wa Tanzania awe na haki sawa ya kupata Elimu - apate Mimba ama asipate mimba. CCM waliahidi kwenye Ilani yao kuwa watoto waliopata uja uzito Wataendelea na Masomo. CHADEMA wanaamini hivyo na Act Wazalendo tunaamini hivyo. Makamu wa Rais Bi. Samiah Suluh amenukuliwa akiamini hivyo na Waziri wa Afya pia. Wizara ya Elimu ilitunga mpaka mwongozo wa kuwezesha hilo. Ni Rais Magufuli tu ndio hataki watoto wa kike warudi shuleni. Hii Nchi sio ya Magufuli peke yake. Hatuwezi kukaa kimya kumwona mtu mmoja analazimisha imani zake kwa Jamii nzima ya Watanzania.
Hongera nyingi kwa Watanzania waliohakikisha kuwa tunasubirisha Mkopo wa Benki ya Dunia mpaka hapo utakapoboreshwa na kutoa nafasi kwa watoto wa kike kupata Elimu bila ubaguzi wala unyanyapaa.

Januari 22, 2020.
Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,
1818 H Street
Washington, DC
20433
Wapendwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia,
YAH: MKOPO WA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 500 KWA AJILI YA MRADI WA UBORESHAJI WA ELIMU YA SEKONDARI NCHINI TANZANIA
Jina langu naitwa Zitto Kabwe, ni Mbunge kutoka Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania.
Ninawaandikia barua hii kuhusu kikao cha Bodi cha tarehe 28 Januari 2020, kikao ambacho Bodi itajadili mkopo wa Tanzania kiasi cha Dola za kimarekani milioni 500 kwa ajili ya Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari Tanzania.
Katika barua yangu kwenu ya tarehe 9 mwezi Septemba, niliwakumbusha kuhusu hali mbaya ya masuala ya haki za kijinsia na kibinadamu nchini mwangu. Kwa masikitiko, inaonekana kwamba hatua ya Benki ya Dunia kuidhinisha fedha za mradi ujulikanao kama "Productive Social Safety Net" mwezi Septemba iliitia makucha serikali hii. Kwa hakika, hali imekuwa mbaya mno. Mwanahabari Erick Kabendera bado anasota rumande, vyama vya siasa havina ruhusa ya kufanya mikutano ya hadhara, nao mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar ukiwa umevurugwa hali inayopelekea majaliwa ya uchaguzi mkuu wa 2020 kukosa maana.
Ni wiki iliyopita tu, vikosi vya usalama vilinizuia mimi kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wapigakura wangu. Vikwazo vya jinsi hii wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Novemba mwaka jana, vilitawala kwa vyama vya upinzani kuzuiwa kufanya mikutano isipokuwa chama tawala pekee, chama cha mapinduzi. Wakati wa uchaguzi huo wa Novemba, chama cha mapinduzi kiliwazuia zaidi ya wagombea 400,000 wa vyama vya upinzani wasigombeaa nafasi za uongozi kwa kuwa tu walionekana wasiokubaliana na matakwa ya serikali hii. Matokeo yake, takribani vyama vyote viliususia uchaguzi huo na kupelekea asilimia 99.6 ya viti vilivyokuwa vikigombewa kunyakuliwa na chama tawala.
Nazo fursa haba za kiuwajibikaji wa kikatiba zilizokuwa zimesalia kama vile uwepo wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nazo zimehujumiwa, kwani Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amefukuzwa kutoka ofisini kinyume cha Katiba mwezi Novemba mwaka jana, hali inayoweka rehani usalama wa fedha za walipakodi na uwekezaji wa benki yenu. Mwaka 2020 tunatarajia kufanya uchaguzi mkuu ambao tunaona dalili zote kwamba utavurugwa na kuharibiwa na chama tawala ili kujihakikishia ushindi wa bwelele.
Serikali hii haina tena usafi wa kujidai kuwa serikali inayowakilisha maslahi ya watu wa Tanzania, isipokuwa inajali na kulinda maslahi ya wachache. Jambo la kusikitisha ni kwamba, si hiki kikundi kidogo cha watawala wa sasa bali ni watanzania hawa kwa wingi wao ndio ambao watalazimika baadaye kulipia mkopo huu. Kubwa zaidi, hofu yetu ni kwamba kutokana na ukosefu wa misingi ya uwajibikaji, malengo ya uwekezaji wa fedha hizi yatatumiwa vibaya na chama tawala kujinufaisha kisiasa na kuharibu mchakato wa uchaguzi.
Kwa mantiki hiyo, ninakuombeni msimamishe utolewaji wa fedha hizo kwa serikali hii mpaka pale misingi ya uwajibikaji itakaporejeshwa Tanzania. Misingi hii ya uwajibikaji ninayoizungumzia ni pamoja na uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kukusanyika, chaguzi huru na za haki, sanjali na kumrejesha ofisini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Mnamo tarehe 3-8 mwezi Februari, nitakuwa Washington DC. Nitafurahi kukutana nanyi tuweze kutazama kwa yakini namna ambavyo mchango wa Benki ya Dunia unaweza kuwa wenye tija kwa maendeleo ya nchi yetu.
Ni imani yangu kuwa tutapata wasaa mzuri kujadiliana.
Wenu,
Zitto Z. Kabwe,
Mbunge,
Jimbo la Kigoma ujiji,
Kiongozi wa Chama, Alliance for Change and Transparency.
Nb: Barua hii iliandikwa katika lugha ya Kiingereza. Imetafsiriwa katika Kiswahili na Vicent Kassal
 
Watu kama huyo ndio wakuokota kwenye viroba coco beach, anajua ni athari kiasi gani huletwa na mtoto mjauzito kurudi shule? Unataka akafundishe nini wenzake walio shule? Mbona mnakaza ubongo kiasi hicho? Anyway, tumeshachoka madeni, tukaze mikanda tu..
 
Huyu mtu hana hata lepe la Uraia, si mwenzetu kabisa. Nilikuwa nakataa ila sasa nimeamini.
 
Watu kama huyo ndio wakuokota kwenye viroba coco beach, anajua ni athari kiasi gani huletwa na mtoto mjauzito kurudi shule? Unataka akafundishe nini wenzake walio shule? Mbona mnakaza ubongo kiasi hicho? Anyway, tumeshachoka madeni, tukaze mikanda tu..

Haya tumeona nenda kachukue 2,000/= yako lumumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana, tuone hela ya kampeni za kijani itatoka wapi

Mkumbuke watumishi wengi hawajalipwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uelewa wa waTanzania bado ni mdogo sana. Zitto anatakiwa kuungwa mkono na kila mTanzania mwenye kuitakia mema Tanzania ya baadae. Heko Zitto. Tumejionea wenyewe uchaguzi wa Tamisemi ulivyokuwa. Mtoto akibeba mimba ndo akili zake zimeisha? Watanzania tujitafakari bwana...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akili za Huyu bwana Zitto zimeruka kabisa..Waha wa kigoma watamuhukumu kwa upuuzi wake huu

Nikuhakikishie Kuwa hutorudi bungeni bwege wewe
 
Point yako nn hapa? Mara watu kama hawa waokotwe kwny viroba, mara mmechoka madeni, point ya msingi ni ipi?
Watu kama huyo ndio wakuokota kwenye viroba coco beach, anajua ni athari kiasi gani huletwa na mtoto mjauzito kurudi shule? Unataka akafundishe nini wenzake walio shule? Mbona mnakaza ubongo kiasi hicho? Anyway, tumeshachoka madeni, tukaze mikanda tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto ni akili kubwa huwezi fananisha na hawa waimba mapambio ya ccm,Zitto kaongea ukweli mtupu ambao sisi wengine hatuwezi ongea tumefungwa midomo,ukijaribu kuongea kidogo ukikoswa koswa kutekwa basi jiandae na kesi ya uhujumu uchumi ambao hauna mdhamana wishowe unaishia kunyea debe.Mungu akulinde Mh Zitto
 
Nawe unakuwa bwege wa wanasiasa. Zitto siyo mnafiki? Kuna mwanasiasa ambaye siyo mnafiki? Alipokuwa anapiga rushwa kwa mambo ya Buzwagi alikuwa anakutetea wewe? Shiiiit!
Zitto Kabwe alikuwa anawatafuta wampooze huku na kule. Lijamaa madili kede kede
 
Kama uliyoandika humu ni kweli nalaumu mfumo mzima wa usalama wa nchi.

Hongera uliyendika, acha chuki za kisiasa zitutafuna iko shida sana kwa black skinned race. Wazungu wajinga tu sijawahi kuwaamini wala kuwapenda nacheka nao meno tu ila moyoni siko nao hawajawahi kumpenda Mwafrika na sitajikomba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuilu hata Mimi siwapendi wazungu, Ila sio wote wenye roho mbaya.Ni kama ccm vile sio wote ni manya'ngau wapo na watu wazuri ndani ya ccm ila wameminywa.
 
..inawezekana masuala ya gender, uhuru wa vyombo vya habari, na demokrasia, yakawa siyo muhimu kwetu.

..lakini masuala hayo ni muhimu kwa wafanya maamuzi wa WB ambao ndio walengwa wa barua ya Mh.Zitto Kabwe.

..nadhani njia sahihi ktk hili ni serikali kuwahakikishia WB kuwa hoja za Zitto na wanaharakati zitashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi wa haraka.
Tatizo ni yeye mwenyewe Zitto. Baada ya kumusikiliza akitaja kwamba FDCs ni vyuo vya CCM hapo ndo nimeona ana matatizo kichwani. Nadhani hana akili ya kujifunza na hana muda wa kuuliza wengine kabla hajachukuwa maamuzi. WB nao inakuwaje hata hawaulizi? Lolote waliloelezwa na mtu wanakubali labda kuna preconceived ideas. Sasa tena ana tatizo hilo la kutumia nembo ya Bunge! chini anataja na NGO yake kana kwamba iko chini ya kivuli cha bunge!
 
Duh Mkuu Blindspot, nijibu mara ngapi na nimeishakujibu kuwa Zitto anaikosoa serikali kwa kutumia hoja zenye nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu, yuko makini sana kwenye kuchagua maneno yake na kauli zake, hivyo hawana pa kumshikia.

Mfano Tundu Lissu alipobaini kuna gari linamfuatilia, aliitisha press conference na kutangazia umma, kisha akatulia, angekuwa ni Zitto, angeanzia kuripoti kwanza polisi na kunakohusika, kisha kufanya press conference, unadhani wasiojulikana wangeendelea kumfuatilia?.

Wapinzani wengine wengi wanaingia matatizoni kutokana na uropokaji, Zitto ni mjengaji hoja mzuri na ni strategist.

Chadema, ukimuondoa Zitto na Prof. Kitila Mkumbo, haina kabisa ma strategists.

Angalia mfano mwingine huu wa Zitto alipotuhumiwa kupika data, msikilize anachosema

P
Siamini Kama aliyeharisha hapa ni P niliyemzoea!kaka P come to your sense please!nmezoea huwa unakosoa kinyumenyume,sasa bala unaonekana unasifia seriously[emoji54][emoji54][emoji54]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitakuwa wa mwisho kumuamini ZITO KABWE!
Hata chadema ikifa ntabaki kuwa mfuasi kisiasa wa Tundu antipass lissu!kama utaniuliza kwann?ntakujibu kwa sababu ya damu yake kumwagika kwa ajili yetu sote!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom