Kucheza Makanisani na gospel: Ndombolo na viduku tushavichoka tuhamie kwenye mauno, Inaruhusiwa na wala sio kosa kwa kanisa

Kucheza Makanisani na gospel: Ndombolo na viduku tushavichoka tuhamie kwenye mauno, Inaruhusiwa na wala sio kosa kwa kanisa

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kucheza tutakavyo ni ruhusa, Ruhusa hii tumepewa kwa kanisa kubariki tukio la Mfalme Daudi alipocheza mpaka nguo zikamdondoka.

Tuwe huru,

Ukichukia mapendekezo haya labda uwe msabato, hakuna kucheza ni kusimama tu

Imeandikwa:
Yakobo 4:4
[4]Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.

Ye adulterers and adulteresses, know ye not that the friendship of the world is enmity with God? whosoever therefore will be a friend of the world is the enemy of God.
 
Kenge nyie Daudi hakucheza hekaluni, alicheza kwenye event ya kushangilia ushindi wa vita.
Andiko linasema alicheza mbele za BWANA..
Sasa kati ya hekalu na BWANA mkuu ni nani?
Wakicheza kwa heshima ni sawa tu.
Tatizo ni pale wanapoigiza uhuni wa mitaani kama hao hapo juu!

2 Samweli 6:14
Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.

2 Samweli 6:15
Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la BWANA kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta.

2 Samweli 6:16
Ikawa, sanduku la BWANA lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za BWANA;
 
Sijui kwanini wanawake wanapenda kujidhalilisha , mwanamke wakati wote anatakiwa awe Ander control
Na ndivyo ilivyo agizwa na Mungu, sisi ndio tukajifanya wajuaji wa haki sawa, sasa haya ndio matokeo yake!

Mwanzo 3:16

1 Timo theo 12-14
 
Na ndivyo ilivyo agizwa na Mungu, sisi ndio tukajifanya wajuaji wa haki sawa, sasa haya ndio matokeo yake!

Mwanzo 3:16

1 Timo theo 12-14

Mkuu achana na ukiritimba,uhafidhina na ushamba,dunia ya 2000s si sawa na dunia ya 2000s BC.
 
Kucheza tutakavyo ni ruhusa, Ruhusa hii tumepewa kwa kanisa kubariki tukio la Mfalme Daudi alipocheza mpaka nguo zikamdondoka.

Tuwe huru,

Ukichukia mapendekezo haya labda uwe msabato, hakuna kucheza ni kusimama tu

View attachment 2825215

View attachment 2825211

Tofautisha kanisa na Cult. Tatizo mnachukulia kila dhehebu ni kanisa. Kanisa Lina misingi yake sio hao makahaba.
 
Back
Top Bottom